JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 6,835
- 14,196
Kuna maendeleo gani makubwa Rwanda,Burundi?hizi nchi ni ndogo kuriko Mkoa wa Kagera.Kinachoikwamisha Zanzibar ni huu Muungano usio na faida ,unajua hata hii Mikoa kama ingeweza kujitawala yenyewe mbona kuna Mikoa ingekuwa haikamatiki kwa maendeleo na ukuaji wa uchumi wake.
Ruanda Burundi ni vinchi vidogo sana pengine hata baadhi ya mikoa yetu ni mikubwa sana,leo hao wanyaruamda na waburundi ingawa kuna mpito wa shida na vifo lakini mbele yao wanaiona nuru,
Hapa tunawekwa na ahadi hewa na mikakati ya mwisho wa dunia.Tupo katika kipindi cha kukabana aka kuekana jela na vizuizini kama nchi iliyofanya Mapinduzi ,
Huyu Samia kama ni mwerevu anaweza kabisa kuipapatua Zanzibar na jinamizi hili liitwalo Muungano.
Faida ya Muungano kusema kweli sijaiona kabisa kabisa. Zaidi ya kusimika viongozi wajaza matumbo yao. Wananchi wanashida wamejaa magonjwa yasiyoelezeka ambayo serikali ingeweza kabisa kuwatibu.leo raia wema hichohicho kiduchu wanachangishana kuwapatia huduma za afya.
Kuna YouTube channel zinaumbuwa serikali zetu ,ukiangalia wananchi wanatia huruma kabisa kabisa,inaonyesha wazi kabisa kiundani uongozi na serikali haziwajali wananchi .
Ni bora ili kujipapatua Serikali itangaze matibabu bure kwa waTanzania wote,kama haina dawa japo vipimo viwe vya bure.
Zanzibar ilikuwa na elimu bure yenye tija nzuri kabisa ,halikadhalika hospitali ilikuwa bure lakini leo ndani ya Muungano kila kitu kimevurugika. Bora ya jana.
America ina majimbo Mengi makubwa,jimbo moja ni Sawa na nchi kama TZ,mbona Kuna maendeleo makubwa?
Ukubwa wa nchi na udogo wa nchi sio kigezo Cha maendeleo,China,Korea,ni nchi kubwa kwa eneo na zimeendelea,
Inawezekana kwako wewe muungano hauna maaana,lakini kawaulize wazenj wenye biashara zao za hotel,kuanzia Dodoma,Mafinga,Njombe,Dar ndio wapo kibao wanaendesha maisha,
Huku Dodoma ni jirani zangu,wamenunua viwanja,wamejenga,wapo na familia zao,wengine wameoa na kuolewa huku,