Kama si Muungano Zanzibar ingekuwa mbali sana

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,363
2,000
Kinachoikwamisha Zanzibar ni huu Muungano usio na faida ,unajua hata hii Mikoa kama ingeweza kujitawala yenyewe mbona kuna Mikoa ingekuwa haikamatiki kwa maendeleo na ukuaji wa uchumi wake.

Ruanda Burundi ni vinchi vidogo sana pengine hata baadhi ya mikoa yetu ni mikubwa sana,leo hao wanyaruamda na waburundi ingawa kuna mpito wa shida na vifo lakini mbele yao wanaiona nuru,

Hapa tunawekwa na ahadi hewa na mikakati ya mwisho wa dunia.Tupo katika kipindi cha kukabana aka kuekana jela na vizuizini kama nchi iliyofanya Mapinduzi ,

Huyu Samia kama ni mwerevu anaweza kabisa kuipapatua Zanzibar na jinamizi hili liitwalo Muungano.

Faida ya Muungano kusema kweli sijaiona kabisa kabisa. Zaidi ya kusimika viongozi wajaza matumbo yao. Wananchi wanashida wamejaa magonjwa yasiyoelezeka ambayo serikali ingeweza kabisa kuwatibu.leo raia wema hichohicho kiduchu wanachangishana kuwapatia huduma za afya.

Kuna YouTube channel zinaumbuwa serikali zetu ,ukiangalia wananchi wanatia huruma kabisa kabisa,inaonyesha wazi kabisa kiundani uongozi na serikali haziwajali wananchi .

Ni bora ili kujipapatua Serikali itangaze matibabu bure kwa waTanzania wote,kama haina dawa japo vipimo viwe vya bure.

Zanzibar ilikuwa na elimu bure yenye tija nzuri kabisa ,halikadhalika hospitali ilikuwa bure lakini leo ndani ya Muungano kila kitu kimevurugika. Bora ya jana.
 
utah jazz

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
875
1,000
Yaani haka kakisiwa watu wake wanajisikia sana
Tanganyika imewabeba miaka yote lkn bado mnaleta chokochoko
Ebu fikiria Zanzibar haina hata barabara za lami hapo mtailamu Tanganyika? Mnataka Tanganyika iwakusanyie kodi?
 
utah jazz

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
875
1,000
Hawa watu wa visiwani ni vituko ukiwakuta kwenye gahawa wao ni kuilaumu Tanganyika tu kodi wanakusanya wao na matumizi wanapanga wao ila hata miundombinu ya barabara wamesubiri hadi rais amewapa fungu
Bila Muungano mmengeuana kama kuku na akili zenu za sisi Wapemba wao Waunguja.
Mabaguzi sana nyie mijitu.
 
Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,363
2,000
Yaani haka kakisiwa watu wake wanajisikia sana
Tanganyika imewabeba miaka yote lkn bado mnaleta chokochoko
Ebu fikiria Zanzibar haina hata barabara za lami hapo mtailamu Tanganyika? Mnataka Tanganyika iwakusanyie kodi?
Zanzibar ,waulize hawa wasanii wakata viuno wanaenda kufanya nini huko Zanzibar ? Na hata wamasai wengi wamejificha Zanzibar na wanakula raha hakuna anewanyukua,ila ni kuzidisha njaa tu maana maendeleo yamekanyagwa na kudumazwa na Muungano.
 
Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,363
2,000
Hawa watu wa visiwani ni vituko ukiwakuta kwenye gahawa wao ni kuilaumu Tanganyika tu kodi wanakusanya wao na matumizi wanapanga wao ila hata miundombinu ya barabara wamesubiri hadi rais amewapa fungu
Sio wamepewa fungu Serikali ya Zanzibar inaidai Serikali hii kandamizi ya Muungano zaidi ya deni lao la Taifa,makato na riba na faida ya kuunganisha mabenki.Mbona hamlipi ???
 
utah jazz

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
875
1,000
Tukianza kuwasafisha wapemba na wamakunduchi waliojimlikisha mahekari ya ardhi uku bara sijui mtawahifadhi wapi
Zanzibar ,waulize hawa wasanii wakata viuno wanaenda kufanya nini huko Zanzibar ? Na hata wamasai wengi wamejificha Zanzibar na wanakula raha hakuna anewanyukua,ila ni kuzidisha njaa tu maana maendeleo yamekanyagwa na kudumazwa na Muungano.
 
Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,363
2,000
Ubinafsi ni kitu kibaya sana
Kweli kabisa ubinafsi ni mbaya hasa pale unapoungana na mwenzako kama nchi zilizosawa halafu unaanza kualamika mimi eneo langu kubwa nahitaji hela nyingi,hivi kuna usawa hapo ? Almasi yangu Mafuta yetu ,kuna usawa hao, we wacha tu Zanzibar leo ingekuwa ni heaven ya Africa.
 
utah jazz

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
875
1,000
Mnataka Tanganyika iwe inawakusanyia kodi ?
Sio wamepewa fungu Serikali ya Zanzibar inaidai Serikali hii kandamizi ya Muungano zaidi ya deni lao la Taifa,makato na riba na faida ya kuunganisha mabenki.Mbona hamlipi ???
 
Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
56,616
2,000
Kuna mapato ambayo Zanzibar inayachangia kwenye serikali ya Muungano?
 
Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,363
2,000
Tukianza kuwasafisha wapemba na wamakunduchi waliojimlikisha mahekari ya ardhi uku bara sijui mtawahifadhi wapi
Aloo kama mnaweza hilo itakuwa mmefanya jambo la maana sana sana,msiishie hapo mrudishe na kilomita kumi za ukanda wa pwani,kudadadeki ,yaani asubuhi yake mtasikia chereko chereko ,Zanzibar hioo inapaa mnabaki midomo wazi.
 
Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,363
2,000
Kuna mapato ambayo Zanzibar inayachangia kwenye serikali ya Muungano?
Itowe wapi wakati mmewekeza mirija kila kona,ndio ikasemwa huu Muungano ni Muungano kandamizi.
unanyonga halafu unamwambia unaemnyonga mbona huvuti puumzi ?
 
EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
14,321
2,000
Kanchi kenyewe kanazidi kupungua kutokana na kina cha maji kuongeze, uvunjike tu tuwarudishe kwenu wooote mliopo bara mkabanane na ardhi yenewe hakuna, tuone mtalima wapi au biashara mtauzia wapi?

wazanzibara hawataki hata kusikia muungani kuvunjika. Wapemba pale kariakoo wote tunawafukuza na wabara waliopo huko wanarudi halafu kila mtu ajitegemee, ushawahi kuwaza hilo?? Bahresa abebe malori yake aje nayo zenji.

shenzi type vunjeni muone kama tutatetereka.
 
Mtambwe

JF-Expert Member
Apr 14, 2014
737
1,000
Yaani haka kakisiwa watu wake wanajisikia sana
Tanganyika imewabeba miaka yote lkn bado mnaleta chokochoko
Ebu fikiria Zanzibar haina hata barabara za lami hapo mtailamu Tanganyika? Mnataka Tanganyika iwakusanyie kodi?
Ukisikia Ujinga ndio huo wako wewe. Nani aliekuambia kuwa Wazanzibari hawalipi Kodi? Tena wazanzibari wanalipa kodi mara mbili. Na mukishazichukua Kodi zetu kuzirudisha inaonekana kama kwamba tunezoea kuomba. Hio ni haki yetu
 
Lecheminduroi

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
908
1,000
Hoja ingekuwa Tanzania ingefuata mfumo wa majimbo ingeendelea sana ningekuelewa, Wazenji wabaguzi sana halafu hamchangii chochote kwenye serikali ya muungano

Cha ajabu zaidi mna hadi bunge lenu au mmeligeuza sehemu ya kula urojo na kukaa vikao vya umbeya baadala ya kupanga bajeti zenye tija kwa Mzanzibari mwenye kipato cha chini!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom