Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,632
- 697,751
Wote tunajua maumivu ya kukamatiwa mali hasa na serikali ama taasisi baada ya kushindwa kulipa deni ama madai fulani... Tunawajua madadali wetu maarufu kina MAJEMBE na YONO...
Mali yako inapokamatwa ngarama zifuatazo zitahusika
-Deni halisi unalodaiwa
-Faini yake
-Riba yake
-Gharama za ukamati
-Gharama za uhifadhi
-Gharama za utaifishaji(kuuza mali husika kufidia deni)
Kama sheria zikifuatwa hata kwenye muda, bado nina mashaka, tunaweza kupoteza bombadia yetu(ni yetu kwakuwa imenunuliwa kwa kodi zetu wananchi) sio ya serikali
Nina hakika baada ya kukamatwa huko ughaibuni tuliletewa notice ya madai yenye mchanganuo wa gharama zote pamoja na masharti na muda wa kulipa.... Na kwa vyovyote kuna sentence inasema.... FAILURE TO DO THAT AT GIVEN TIME......!
Vema serikali ikaweka siasa kando na kuanza kutafuta mchawi.. Tunahitaji weledi, hekima, tafakuri, ukweli na diplomasia kuweza kuokoa mali yetu hiyo!
Tusishupaze shingo... TUTAPOTEZA!!!!
Sent using Jamii Forums mobile app