Kama sheria haijapitishwa na Bunge na haijafuata Katiba, Sheria hiyo ni batili. Kanuni mpya za mitandao ni batili

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
(1) Katiba hutoa madaraka kwa Bunge kupitisha sheria. SHERIA lazima iwe within 4 walls ya katiba-la sivyo sheria ni batili. Sheria inatoa madaraka kwa Waziri au taasisi nyingine (k.m TCRA) kutunga KANUNI. Kanuni lazima ziwe within 4 walls ya sheria mama na Katiba-la sivyo ni batili.

(2) Sheria/Kanuni batili haziwi batili mpaka zimebatilishwa na Mahakama. Maana yake, moja, shauri ipelekwe mahakamani, pili, Mahakama ziwe huru kufanya maamuzi kwa mujibu wa sheria na sio vinginevyo.Wananchi wangapi wanauwezo wa kwenda Mahakamani? Kwa kiasi gani Mahakama ziko huru?

(3) Kwa kiasi fulani dosari la kwanza lilijibiwa na tafsiri ya kimahakama ya Katiba kwamba mtu/taasisi yoyote, hata kama sio mwaathirika mojakwamoja ya sheria batili, anaweza kupeleka shauri mahakamani kupinga sheria/kanuni batili. Sheria iliyopitishwa 2019 imefuta uwezekano huu!

(4) RESULT: kuna uwezakano mkubwa wa sheria/kanuni batili kuendelea kuwa na nguvu za kisheria na kuendelea kufanya kazi kwa sababu hazijapingwa mahakamani na kubatlishwa.
 
Sasa ya Mwakyembe anatumia ubabe. Ajitokeze mmoja akapinge mahakamani. Hii ndio Bongo, nchi ya Wabongo inaendeshwa kibongobongo.
 
Back
Top Bottom