Kama Sheikh Yahya anauza fimbo za utajiri ni sawa, Ambikile akiuza dawa serikali/wananchi nongwa?

tetere

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
963
430
Mjadala wa dawa ya Loliondo umefika mahali umekuwa mjadala wa kisiasa. Nafasi ya waganga, serikali na wananchi haiko wazi tena. Serikali inalaumiwa kwa nini haijaingilia/haijasema chochote/haijazuia kwa wakati. Ati serikali inapaswa itoe kibali au iruhusu dawa hii ithibitishwe kwanza ndio iruhusu itumike.
Wananchi wanaongelea tiba hii wakitaka kujua kama kweli inatibu kweli au la. Na wengi wameshakunywa lakini wanasubiria testimony watoe wengine. Waliotoa testimony tunaona kama hazitoshi, tunahitaji nyingi zaidi.
Babu hana maelezo ya ziada zaidi ya aliyokwisha kuyatoa. Na hajasema zaidi ya aliyodai aliambiwa kuyafanya. Babu hajasema dawa yake inatibu vipi. Anachosema yeye ni kuwa dawa hii inatibu.

Wanaokunywa dawa hii hawalalamikii matibabu ya babu, wanachoonyesha ni adha ya kipata dawa hii. Wengi wa wanaoongelea zaidi dawa hii ni watizamaji.
Sasa basi:
1.Dawa hii inaponyesha kwa imani- tutaichunguza au kuihakiki vipi dawa hii kwa kutumia conventional approach. Ni upotevu wa muda.
2.Wanaokwenda kwababu wanasukumwa zaidi na shida walizo nazo na pia jitihada ambazo walikwishazifanya huko nyuma hazikuwapatia matokeo waliyoyahitaji ie. Kupona!
3.Kuna waganga wengi Tanzania ambao wanadai wanatibu maradhi mengi sana. Hili tumeweza kuishi nalo na hata walipowaua zeruzeru tunajua tulivyofanya, ila hatukuuliza maswali mengi. Hakuna mganga wa kienyeji/anetibu kwa imani anaeweza kueleza anaponya vipi. Faith healing in Tanzania is a vibrant industry which nobody has ever try to scrutinize it. Ama kwa kuwa wengi wetu ni wateja. Ndio maana Sheikh Yahya akiuza vifimbo vya utajiri hata rais wetu alimlipia nauli ya kwenda kutibiwa India. Sio kwa sababu sheikh Yahya ana sura nzuri, la hasha! kwa kuwa hata rais wetu anajua kuwa ni mtu mzuri, ni mtu wa watu, anasaidia yasiyosaidika pengine popote.
4. Kama ukihoji matibabu ya babu wa Loliondo lazima uhoji pia matibabu mengine kama hayo. Kuna mashehe wanakusomea dua, wachungaji wanatoa mapepo,waganga wanaweza kurudisha waliokufa mfano ni makanisa yaliyoko Dar yanayorudisha misukule - hawa utawaelezea vipi? Kuna magomvi ya kila siku ya kuloga/kulogwa kwenye familia zetu. Zote hizi ni matokeo ya imani zetu, wakati mwingine zinatutia nafuu wakati mwingine imani hizi ni mzigo mkubwa ila wakati mwingi zinatutia gharama kubwa hasa kupoteza nafasi, mali au uhai.
5Babu is responding to our needs. He is responding to our fear. He is not calling on anybody but as a matter of fact people are calling on him. And probably these are people who have tried for treatment in so many other places as I said earlier but could not find solution to their issues. And in some cases these are not poor people who've had no much choices in life.Some of them are wealthy people (naskia wakubwa wankwenda usiku)

Sasa basi- nini kwa nini serikali inajiingiza katika masuala ambayo hawana nia ya kuyatatua bali wanataka waonekane kama wanajali. I think they are responding to the diplomatic preasures as they are being asked what are they doing regarding the issue in question. Lakini serikali inapaswa iandae sera ambayo iko clear juu ya nafasi ya watu kama hawa. Na serikali inapoingilia ifanye hivyo kwa wote wanaofanya shughuli kama hizo.

Viongozi wengi wamekunywa dawa hii, hata kama inaponya lakini bado kuna haja ya kuweka bayana nafasi za waganga wa kienyeji/imani nk.
*Pia kuna haja ya kuweka wazi kama wataendelea na hawa watabibu, wanaotibiwa nao waandikwe majina ili wafuatiliwe afya zao. Haitoshi tu kupiga kelele tukisema kuwa dawa haitibu wakati inatibu au tukisema inatibu wakati haitibu. Its a waste of time if we are not going to get serious with these issues!
 
Hao wote uliowataja wana leseni ila Babu hana. Mwambie Babu achukue leseni tu kelele zote zitaisha.
 
Back
Top Bottom