Kama Serikali itashindwa kuwaongezea mishahara watumishi wa umma 2020 vyama vya wafanyakazi vifutwe

Black Mirror

JF-Expert Member
Oct 17, 2019
836
1,044
Salaam mabibi na mabwana, yapita miaka takribani 4, watumishi wa umma chini ya Mh Rais Magufuli na serikali yake imeshindwa au imekataa kujali maslahi ya watumishi wa umma. Mbali na kukataa kuwajali haswa kuwaongezea mishahara na kuwapandisha madaraja watumishi hawa wana vyama vyao ambavyo kazi kubwa ya vyama hivi ni kuwatetea watumishi hawa serikali na kwingineko.

Mbali ya kwamba kazi kuu ya vyama hivi ni kuwatetea watumishi wa umma katika masuala yote ya kazi na si mshahara tu lakini lililo kubwa kwa mtumishi ni maslahi yake. Chini ya TUCTA vyama kama TUGHE, CWT, na vingine vyote vimeshindwa kuwatetea watumishi wa umma kwa serikali kibaya zaidi vinakata pesa ya watumishi bila sababu.

Hamna jambo la maana vinafanya tofauti na kula pesa yao tu. Kwakuwa serikali ndiyo inatoa maamuzi yoote juu ya mtumishi wa umma basi vyama hivi havina kazi bora vifutwe kabisa ili serikali iendelee kufanya maamuzi kama inavyo fanya leo hii. Mfano;

1) Serikali iliamua kuongeza makato kutoka 8%-15 kwa wanufaika...vyama vilishindwa kusimama kidete kulikataa jambo hilo alafu vinaendelea kukata pesa ya watumishi wa umma.

2) Serikali imeunganisha mifuko ya jamii bila ushirikishwaji wa wachangiaji vyama viko kimyaa..wao ni kukata tu pesa.

3) Sera ya bima ya afya ilibadirishwa mtumishi analazimika kuwapa bima watu ambao ni mke/mme, baba,mama na watoto basi. Hii si sawa maana kuna mtumishi anao ndugu wa muhimu na pengine anapaswa kuwasaidia lakini haruhusiwi vyama vimekaa kimyaaaa.

4) Wanasiasa wamekuwa wadhalilishaji wakubwa wa watumishi wa umma lakini vyama vinachekelea tu kazi kukata pesa za watumishi.

5) Mtumishi wa serikali analipa kodi kubwa sana lakini vyama hivi viko kimya kabisa...vinakata pesa tu.

6) Kwenye utumishi wa umma kuna upendeleo mkubwa sana, kuanzia kwenye mishahara, marupurupu na ofa nyingine...vyama viko kimya tu vinakata pesa ya watumishi.

Mh Rais Magufuli alitangazia watumishi wa umma kuwa kabla ya muda wake kuisha lazima atawaongezea mishahara tena mizuri tu na kuwataka waendelee kuwa wavumilivu.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, muda wa Mh Magufuli unaisha October 2020, japo anaruhusiwa kuongeza kipindi kingine cha miaka 5, hivyo basi endapo muda huu utaisha na serikali ikashindwa kutimiza adhima ya Mh Rais Magufuli ya kuwaongezea mishahara watumishi wa umma basi vyama vya wafanyakazi VIFUTWE kabisa kwani vitakuwa havina la ziada tena ili watumishi wafikirie njia nyingine ya kupata mtetezi wa maslahi yao kwa serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyuu jamaa sijui hela anapelekaga wapi. Hizoo za miradi Ni za kukopa.kwanni hawaongezei watumishi mishahara
watumishi wenyewe hawajielewi! vyama vyao vyenyewe vinawanachama chini ya 10% ya watumishi, kila siku solidarity wakati hawapo katika umoja!!bora waendesha daladala na bodaboda wana-umoja
 
Black Mirror,
nimewaambia viongozi wa chama changu napofanyia kazi najitoa mwezi wa tatu amna wanachofanya aisee wananikata 30,000 jinga sana
 
Back
Top Bottom