Kama serikali itang'ang'ania kuwalipa DOWANS; CHADEMA kuitisha maandamano ya nchi nzima

hata aking'oka haitatosha. mie natamani ingefanyika ufilisi kama ule wa enzi za nyerere. kila kitu kichukuliwe tuanze upya!
Hamjafahamu mwita25 anatumia lugha ya tafsida. Anyway, tunasubiri maandamano ya nchi nzima, safari hii hadi JK ANG'OKE kama hatoshtuka mapema.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimesema kitaandamana nchi nzima endapo serikali itaailipa kampuni feki ya Richmond a.k.a Dowans. Kauli hiyo ni imetolewa na Mnyika makao makuu ya CDM jijini Dar- Es - Salaam. Hii ni mara ya pili kwa CDM kusema kuwa itaandamana nchi nzima endapo serikali itailipa Dowans.
Swali la msingi je maandamano yatasaidia Dowans kutolipwa?
Source ITV Habari.

katika utawala wa sheria na nchi inyokubaliana na haki za binadamu imekuwa ikisisitizwa hata mhalifu ana haki zake zinazostahili kulindwa na wakati mwingine kuheshimiwa. na ktk msingi huo inatamkwa uwepo wa vyombo mbalimbali na umuhimu wake kama vile chombo cha kutunga sheria "bunge", kusimamia sheria (serikali), kutafsiri sheria yaani (mahakama).

kwa msingi huo chombo kimoja mfano cha kutunga sheria kinapochukua jukumu la serikali na wakati huo huo kuchukua nafasi ya mahakama kama ilivyosasa tunakwenda wapi? hii imekuwa ikinisumbua sana kwani unapozungumzia juu ya kulipa ama kutolipa hayo mabilioni ya shiling kwa nchi kama yetu inayoamini ktk msingi wa utawala wa sheria suala hilo lingeachwa mikononi mwa mahakama kuona uhalali wake, na kwa kufanya hivyo ingeweza kutoa na sababu zake, kitu ambacho watungaji wetu wa sheria wangepata somo na namna mpya ya kukabiliana na tatizo husika, lakini na pili kuona waliotufikisha hapo wanachukuliwa hatua.

kumbuka mahakama ikiamuru malipo hayo yalipwe kwa lugha rahisi (malipo ya kisheria / statutory expenses). ombi langu wananchi wenzangu uzembe wetu katika mikataba kama huu ni sehemu ya fundisho kwetu kwa ngazi zote, hivyo ni vema kuishinikiza serikali kuwajibika kwa uzembe huo hasa ukizingatia nafasi aminiwa (trusted) na wananchi kutumika vibaya na si kwa misingi ya kushinikiza kutolipa tungali tukijua uzembe wa kisheria/kimuundo ambao umepelekea hata nafasi muhimu kama hizi kupewa watu kwa misingi ya maandamano, yaani pasipokuzingatia uwezo na elimu husika na hii ni kwa ngazi zote yaani za kisiasa/kiutendaji.
 
Sasa kama kuilipa nilidhani ilitakiwa kulipwa Richmond sasa ata mrithi nae Anatakiwa kulipwa!
Inajulikana wazi sheria za nchi zilivunjwa kwenye kuipata richmond na kwa kesi serikali ilikuwa inanyuti makusuddi bse watu wana mafungu yao
Nguvu ya umma ikitumika inaweza saidia
 
Unataka kuandamana kupinga hukumu ya ICT au unaandamana nini?

Halafu unajidanganya eti CDM waandamane Dar? Labda wafanyie maandamano yao Kimara Temboni au Kimara Bonyokwa.
Kama unataka kuchezea rungu za FFU njoo ulete maandamano posta uone Jeshi la polisi linavyojibika kulinda raia na mali zao

dogo masaburi yanakuwasha.
 
Je! Maandamano yatasaidia kupindisha sheria?

Hapa ndo tunapochemka kwelikweli. Tunahangaika na mti bila kushughulikia mizizi inayoupa chakula na maji.
Kwani tatizo ni dowans? Hivi tusipolipa ndo madawa hospitalini yatapatikana, madawati mashuleni yatapelekwa?

Bei ya wizi ya umeme itashushwa?
Katika ukweli ni kuwa hakuna kitakachobadilika katika utawala huu iwe kwa dowans kulipwa au no.

Kama kuandamana isiwe kupinga malipo halali kisheria ya dowans, bali hawa waliotufikisha kwenye matatizo yote. Yaani mgao wa ghali wa umeme, kukosekana kwa sukari na hyking price yake, wizi wa raslimali zetu na many other imperishing factors.

Hawa ndio adui wetu wa kwanza.
Mbona hatukuandamana kupinga ubadhilifu wa karibu trilioni kutoka stimulas package? Au trilioni ni ndogo kwa bilion? Tena huko hakukuwa na uhalalishwaji wowote hata wa mahakama ya mwanzo.

Siungi mkono malipo ya dowans, ila siungi mkono maandamano ya dowans.

Dowans haikuigusa moja kwa moja asilimia karibu 80 ya watanzania, lakini stimulus package ni kila mtanzania kaguswa. Wanyamamwitu wale wametugusa hadi mayai yaliyomo viunoni mwetu.

Sukari kila mtu kaguswa. Mbona huku kulikuwa kimya tu? Hebu kama tunaandamana tuseme tunaitoa rasmi CCM
 
hata aking'oka haitatosha. mie natamani ingefanyika ufilisi kama ule wa enzi za nyerere. kila kitu kichukuliwe tuanze upya!

huo ni udikteta. zama hizi si rahisi kihivyo. Nchi yetu ina heshimu utawala wa sheria.
 
Chadema ni wazee wa matamko. Hata hili litapita kama mengine yalivyopita. Nawashauri wawe makini na matamko yao, wayachunguze kwanza kama wataweza kuyafanikisha. Wanatuchosha kwa matamko.
 
Unataka kuandamana kupinga hukumu ya ICT au unaandamana nini?
Halafu unajidanganya eti CDM waandamane Dar? Labda wafanyie maandamano yao Kimara Temboni au Kimara Bonyokwa.
Kama unataka kuchezea rungu za FFU njoo ulete maandamano posta uone Jeshi la polisi linavyojibika kulinda raia na mali zao

UMEWEKA WAZI jinsi ccm inavyomaanisha. Kwamba watu ni wale wateule wachache wanaofaidi rasilimali zetu wanaopatikana posta ila kimara, tandika, mbagala nk huko ni nini vinavyoishi?
 
i am not amused....

kama ni priority, basi ningezungumzia umeme, chakula, mafuta, sukari kabla ya kuangalia dowans...

LETS PUT OUR PRIORITIES RIGHT!!!!

TUGOME KWA DIRECT SUFFERING TUNAZOPATA KWANZA

MTM maandamo kawaida huwa yanaanza na spark ndogo sana, sababu yaweza kuonekana ndogo lakini hasira za watu juu ya mambo mengi yanayowakera wananchi yakawasha moto mkubwa wa mabadiliko.

Kumbuka serikali ya CCM imeshawaona watanzania ni watu wa kupandiwa mpaka kichwani, pamoja na shida zote za umeme, maji, sukari na maisha kwa ujumla kuwa magumu wanataka tena kutuletea adha ya kulipa deni kubwa linalotokana na ufisadi wao.

Nashauri hili la Dowans liwe spark tu lakini wote wanaoathirika na shida zinazoletwa na CCM wataingia kuuwasha moto kwenye maandamano hayo hayo.

Unakumbuka kulichotokea Tunisia, ilikuwa ni jambo dogo tu la mmachinga kumwagiwa mboga zake mtaani lakini kumbe watu walikuwa na machungu moyoni ambayo yaliwasha moto wa mabadiliko.

This to me looks like a good move ambayo itaingiza kila kitu humo ikiwezekana kupelekea kuundwa kwa katiba ya wananchi sio hii ambayo inakuwa engineered by CCM.
 
Je! Maandamano yatasaidia kupindisha sheria?

Loads of rubbish! Maandamano ya umma kupinga udhalimu hayana kitu kinaitwa sheria, Gadafi alikuwa kisheria, serikali ya makaburu wa Afrika ya kusini ilikuwepo kisheria, Mubarak wa Misri alikuwa kisheria.

Maandamano ya umma sio tu yamepindisha sheria ila yameiturn it upside down. You must now learn to think outside the box.
 
maamuzi ya mahakama ni ya mwisho!! nyie mkiingia barabarani mnachotafuta ni kichapo tu, na ffu wapo tayari kwa hilo, maji ya washawasha yamechanganywa na upupu na yanasubiri wavunja sheria kama nyinyi. kumbukeni nchi hii inawenyewe na wenyewe ni ccm milele!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mbona unaogopa maandamano kaka, acha maji ya washawasha watu wanaandamana wakati ndege za kijeshi zinapita juu na bado hiyo serikali inaondoka madarakani.

Tutaandama halafu watumwagie hayo maji ya washawasha hapo ndipo watakapajua kuwa kumbe wananchi ni wengi kuliko askari. Kumbuka haya ni maandamo ya nchi nzima na kwa wakati mmoja, sasa mtatuambia hayo maji ya washawasha serikali ya CCM inayo mangapi, je yapo wilaya na mikoa yote Tanzania, na yanaweza kuhimili maandamo ya siku au wiki kadhaa kwa mfululizo?

Perform an analysis ya uwezo wa askari wako kuwadhibiti watu wenye hasira for many days then come back here.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimesema kitaandamana nchi nzima endapo serikali itaailipa kampuni feki ya Richmond a.k.a Dowans. Kauli hiyo ni imetolewa na Mnyika makao makuu ya CDM jijini Dar- Es - Salaam. Hii ni mara ya pili kwa CDM kusema kuwa itaandamana nchi nzima endapo serikali itailipa Dowans.
Swali la msingi je maandamano yatasaidia Dowans kutolipwa?
Source ITV Habari.

Maandamano yanaweza yasipelekee Dowans kutolipwa, hata hivyo hilo sio lengo pekee la maandamano yapo mengi ikiwemo kwa serikali sikivu kuweza kuisoma response ya watu wake wanaiambia nini juu ya suala fulani, lakini pia ni nguvu ya kisiasa inayoweka upinzani sehemu nzuri kwa wananchi kuona huo kama utetezi wao na kwamba wanao watetezi, lakini pia ni shule kwa wananchi kuwa serikali isiwaburuze, lakini si tumeona pia serikali zikin'gatuka kwa maandamano kumbe yaweza kuwa zaidi ya malipo ya Dowans, Tumechokaaaaa!!
 
Mimi na wewe sijui nani mwenye akili fupi.
Hivi unaleta mambo yako ya Kibosho, kwenye mambo ya sheria?
Hivi unajua International Court Abitration, ni nini? Kwa taarifa yako ili deni ni la kimataifa hata serikali wasipo lipa leo watalipa CDM siku wakichukuwa nchi ata kama tukiwa tumeishakufa.

kama deni lataongezeka itabidi kampuni inayotudai tuipe mgodi wachimbe miaka 90 mpaka pesa yao itakapotimia.
Pro-CDM Jf mnafuta mkumbo tu

ndio mzee wako alivyokudanganya.. Tuombe uhai tutapata ukweli japo najua wewe hautakwepo tz mana 2015 mtakimbia tz.
 
fanya tathmini ya idadi ya watanzania wako wangapi then angalia hao ffu, polisi na hata jeshi wako wangapi ndio uje na huo upupu wenu...woga wako ndio umasikini wako nyama mbofu wewe



maamuzi ya mahakama ni ya mwisho!! nyie mkiingia barabarani mnachotafuta ni kichapo tu, na ffu wapo tayari kwa hilo, maji ya washawasha yamechanganywa na upupu na yanasubiri wavunja sheria kama nyinyi. kumbukeni nchi hii inawenyewe na wenyewe ni ccm milele!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kama serikali ni ya kifisadi kwa kiasi ambacho Chadema wanawahakikishia wananchi. Kumbe maandamano kupinga malipo ni kupoteza muda, kwa sababu hata wasipolipa bado hakuna hakika kama hiyo pesa itatumika kwa maslahi ya umma.

As for me, thats pure politics jamaa. Kutumia kila kete itakayoweza kukusaidia kuchukua madaraka, wananchi tunaweza kunufaika lakini siyo kwa "nia njema" ya wanavyama. Hawajawahi kuwa na nia njema, hawana na hawatowahi kuwa...
 
Back
Top Bottom