Kama serikali itang'ang'ania kuwalipa DOWANS; CHADEMA kuitisha maandamano ya nchi nzima

Hongera CDM tunahitaji uzalendo kama muliuonyesha leo kwa kueleza Fedha ya watanzania isilipe mafisadi. Tuuze kampuni zao na mijumba yao iliyojaa mji mzima tuwalipe Dowans.
 
KATIBA.. KATIBA JAMANI KATIBAAAAAAAAAAAAA... 2015 HIYOO IMENUKIA TUTAIVAA BILA KATIBA MPYA HIVI-HIVI. Mambo ya Dowans hayo kwa wananchi wa kawaida hayana saaana mvuto, mwananchi anajua hata kama huyo jini dowans hatalipwa bado jini magamba atazitafuna hizo hela, mambo ya umeme, sukari, mishahara na kupanda kwa gharama za maisha ndiyo yenye mvuto.. Graduate anaajiriwa serikalini kwa mshahara wa 320,000 kwa mwezi? kwa maisha haya? ila mwanawane yupo tu maskini ya mungu, wala hana wa kumtetea.. sasa huyu akipata nafasi ya kuwa GAMBA kwanini asinyonge badala ya kuchinja? bado hatujasema walimu ambao mbali na kamshahara ka 120,000 bado ana mkopo kwenye benki mbili tatu na last kwa mwezi anapokea take-home 15,000 mwanawane wa watu.. Do TZ?

wewe ni mchochezi ila huna hoja..kwa hiyo km dowans haina mvuto ndo unawavuta watu kupitia umeme,maisha magumu na mishahara ya walim?acha uzandiki ww kwan kukopa benki unalazimishwa?
 
i am not amused....

kama ni priority, basi ningezungumzia umeme, chakula, mafuta, sukari kabla ya kuangalia dowans...

LETS PUT OUR PRIORITIES RIGHT!!!!

TUGOME KWA DIRECT SUFFERING TUNAZOPATA KWANZA
 
Tamko hilo limetolewa na ndugu John Mnyika
Amesema cdm inaitaka serikali kutoa tamko la kutolipa pesa hiyo ndani ya siku 30 zaidi ya hapo yataitishwa maandamano ya nchi nzima!

in blue...
nafikiri ndicho kilichobakia, hii kitu huwa naikubali kiukweli inafanya kazi...
 
mpaka kieleweke, hakuna kulala, tumeteseka vya kutosha, hapa naona umeme tangu last week kumbe ni kwa ajili ya motihani ya form four, na wakimaliza mgao kama kawa, kumbe watoto wanasoma wakati wa mitihani?? ha ha ha! maandamano lazima!!
 
Nani wa kuingia mtaani?
Hayo ni maneno tu.

Swali hilo unalouliza ni la kifisadi na la kijinga; ni sawa mwenzako nape kwenye hotuba yake leo manzese kasema nchi inawenyewe, nao ni magamba, swali ccm inawanachama wangapi?je watanzania wote ni wana ccm?

kukataa kutetea haki na kuwaachia mafisadi walipwe kwa kuwa ni wana ccm huo pia ni ufisadi na si uzalendo .Kutetea mafisadi wasilipwe ndo mshikamano wa watanzania unaotupa kuwa wamoja.Maandamano ndo nguvu ya wanyonge na ni haki kukusanyika maake katiba inaruhusu.

Ni vyema wazalendo tuungane kupinga hoja ya kulipwa mafisadi kwa kuuingia mitaani na maandamano ya nguvu ndo silaha liyobaki maaake ****** yeye ni kutabasamu tu kasahau nchi imekuwa ya mafisadi.
 
CDM wanafanya maandamano kupiga maamuzi ya mahakama ya kimataifa au maandamano ni nini?
 
Hapa dawa na watanzania wote tuingie barabarani tu
si suala la kuwaachia chadema pekee yao
tunaoathirika ni sote
 
maamuzi ya mahakama ni ya mwisho!! nyie mkiingia barabarani mnachotafuta ni kichapo tu, na ffu wapo tayari kwa hilo, maji ya washawasha yamechanganywa na upupu na yanasubiri wavunja sheria kama nyinyi. kumbukeni nchi hii inawenyewe na wenyewe ni ccm milele!
 
Hakuna kitu kinachoweza kupinga amri ya mahakama kwenye utawala wa Demokrasia.
Sasa CDM mnasema mna wasomi wengi tena wanasheria wameshindwa kuelewa sheria za kimataifa na za kitaifa
 
CDM wanafanya maandamano kupiga maamuzi ya mahakama ya kimataifa au maandamano ni nini?

Ndio, sasa wewe unataka nini? tutapinga tu kwani hio makahaba au mahakama ya kimataifa si inaongozwa na watu pia?
 
Lazima ifikie wakati wote tuwe na kauli moja ya kwamba tumechoshwa na kuibiwa huku tunaona ,mimi pia nipo tayari kuandamana mpaka kieleweke.
 
Mambo ya kisheria hasa yaliyofika mahakamani yanapingwa kwa sheria mahakamani..si kwa umbea mitaani...hii ya mnyika mi naiona ni umbea tu!cdm tuna wanasheria makini waliobobea imekuwaje wameshindwa kutoa ushauri na mwongozo wa kitaalam??au tunataka tu umaarufu kwa kuingia mitaani kwa maandamano ili wananch waone tunawajali?mi nasema hatutafanikiwa km hatutabadilika.
 
Ndio, sasa wewe unataka nini? tutapinga tu kwani hio makahaba au mahakama ya kimataifa si inaongozwa na watu pia?

Kwa hiyo na wewe utajitokeza kwenye maandamano au utakuwa unaleta Update kupitia simu yako ukiogopa rungu za FFU
 
Katika mazingira ambapo mafisadi,serik ali,vyombo vya dola,mahakama,Rais ni kitu kimoja ambapo wako kwa ajili ya kulinda masilahi yao na familia zao the only solution NGUVU YA UMMA MAANDAMAMANO.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Ikiwa hili ndiyo suluhisho basi linahitaji uratibu wa hali ya juu maana shaka yangu polisi inaweza kutumia nguvu nyingi sana ili kulinda maslahi ya serikali.
 
Hakuna kulala mpaka kieleweke upo nyuma ya Laptop? Ingia barabarani ukapambane na FFU

wenye akil fupi hao. Yaelekea akil yako ipo kinyumenyume mana hata kwenye laptop yako wabofya ukiwa nyuma yake na sio mbele... Kwel we are dfa. Tek care dogo usiwe mvivu wa kufikiri kama dngi ako.
 
Back
Top Bottom