Kama Serikali ingekuwa inajali watu wake kama inavyosema, sehemu zinazoua sana kama Wami, Mbalizi zingerekebishwa haraka, bibi kijijini angepata maji

Drone Camera

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
13,903
2,000
Umeongea jambo la msingi sana. Kuna vijiji vingi sana - na hata wilaya, ambazo zina vyanzo vizuri vya maji na kuwapa access ya maji wala isingekuwa tatizo, lakini hatufanyi hilo.

Juzi juzi hapa nilipewa taarifa za ngazi za wilaya ambazo watu wanashindwa kuelewa ni jinsi gani serikali imeshindwa kubororesha huduma za maji na ilionekana ni sababu ya uzembe tu wa kiuongozi. Ilitokea mradi mkubwa wa maji kanda ya ziwa uliofanikiwa kwa mabilioni ya fedha kulinganishwa na huduma ya naji wilaya ya Rungwe (Tukuyu). Engineer mmoja alita taarifa kwamba ni uzembe tu Rungwe hawana maji kwa kuwa ni wilaya mojawapo Tanzania ambazo unahitaji kuwekeza vitu viwili ili wapate maji - tanki na mambomba, na akasema hii ni kwa sababu vyazno vya maji viko mlimani kwa hiyo huhitaji pampu wala umeme kuwapatia maji. Angalia kwamba Rungwe ndiko alikotoka Prof Mwandosaya alikuwa Waziri wa Maji na ndiko anatoka Tulia naibu spika wa sasa - lakini bado wanachi wake wanapata shida ya maji hadi ngazi ya wilayani mjini. Sembuse huko kwingine!

Kuna sehemu nyingi Tanzania unaweza kusambaza maji kwa gravity na hii haitahitaji fedha nyingi, lakini hilo halifanyiki kwa ajili ya uzembe tu!
Hapo sawa naanza kukuelewa.
 

Tanzanianist

Member
Apr 25, 2020
60
125
Maoni yako ni mazuri ila unaonekana huna uelewa kuhusu kinachoendelea nchini. Kwanza wami kuna daraja linajengwa kwa sasa, afu kuhusu maji serikali hii imejitahidi sana tofauti na awamu zilizopita fikiria kupeleka maji tabora kutoka ziwa Victoria, mradi wa maji arusha na halimashauri zingine nyingi miradi ya maji mingi inatekelezwa tafuta hotuba ya wazi wa maji bungeni 2020 utaona miradi hiyo yote. Kuhusu dar jam ilikuwa ina sababisha hasara ya mabilion ya fedha kutokana na kuchelewesha watu kuwahi katika shughuli zao, hivyo kujenga flyovers kutasave pesa ambazo zitaenda kwa huyo babu yako unaemsema huko kijijini.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom