Kama serikali ina nia ya kutokomeza UJANGILI ifanye yafuatayo:...

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,180
2,000
Ni wazi kwamba tatizo la ujangili ni sehemu tu ya tatizo kubwa la maisha ya holela vijijini Tanzania. Tatizo linaloonekana leo ni la ujangili lakini siku sio nyingi matatizo ya migogoro ya ardhi nayo yatasababisha mauaji (kama inavyotokea katika mapigano ya wakulima na wafugaji) na tusishangae siku si nyingi, mawaziri wengine wakalazimika kuwajibika katika hili...

Ili kuepukana na matatizo haya yanayojirudia kila leo, serikali idili nayo yote kwa mara moja kwa kufanya yafutayo:

1. Isajili wakulima wafugaji wote Tanzania ikiweka rekodi mahali alipo mfugaji, aina na idadi ya mifugo aliyo nayo

2. Ipime maeneo yote ya ufugaji, kila mfugaji awe na eneo lake lenye ukubwa kutokana na idadi ya mifugo aliyo nayo. Upimaji wa maeneo ya wafugaji ufanywe kwa GPS

3. Maeneo yote yalipimwa na kuidhinishwa kuwa ya ufugaji yaendelezwe kwa kuchimba visima na kujenga majosho na malambo, kuunganishwa na barabara na kupewa huduma za kijamii kama shule na zahanati

4. Serikali ipime na kuyawekea uzio maeneo yote ambayo ni ya hifadhi. Ipimaji ufanywe kwa GPS, na kwa kuanzia uzio wa seng'enge utumike, kisha zio za miiba kama mikonge na mingine zipandwe

5. Serikali ianishe upya umuhimu wa maeneo ya hifadhi na ukubwa unaotakiwa. Katika hili serikali iangalie upya ulazima wa 25% ya ardhi Tanzania kufanywa sehemu za hifadhi wakati wananchi hawana sehemu za kutosha kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji

6. Kwa mara ya kwanza wafugaji waingie kwenye mpango wa serikali wa kupewa ruzuku. Ruzuku itolewe kwa kuwapa wafugaji pembejeo kama matibabu lakini pia mbegu na aina bora za mifugo. Sera ya kutoa ruzuku izingatie kuwa ili mfugaji apewe ruzuku lazima aendeleze ardhi yake ikiwemo kuondoa vichaka na kufuga idadi isiyozidi uwezo wa mazingira

7. Mtu yeyote atakayetaka kuingia upya katika ufugaji (ambaye hakusajiliwa mwanzo) ajisajili kwanza serikalini, eneo lake lipimwe na aingie katika orodha ya wafugaji wanaotambulika na kufaidika kutoka kwa serikali

8. Maeneo ya wakulima nayo yapimwe na yasajiliwe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom