Kama serikali imeruhusu mbegu za mahindi za GMO, watanzania tutegemee maradhi yasiyotibika

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
KAMA SERIKALI IMERUHUSU MBEGU ZA MAHINDI YA GMO YATUMIKE NCHINI TANZANIA BASI TUTEGEMEE WA-TANZANIA WENGI BAADA YA MIAKA 5 IJAYO WATAKUWA NA MARADHI SUGU YASIYOWEZA KUTIBIKA MAHOSPITALINI NA KUSABABISHA MTU KUPATA KIFO. MARADHI YA SARATANI, MARADHI YA KISUKARI, MARADHI YA PRESHA, MARADHI YA HEPATITIS B VIRUS. NI HATARI SANA. SIJUWI WAKEMIA WETU WAMELALA WAPI JAMANI?

Mbegu za mahindi ya GMO kumfikia mkulima mwaka 2021

By Calvin Gwabara, gwabarajr@gmail.com

MAHINDI YA GMO.jpg

Mahindi ya kutengenezwa kwa GMO ni Hatari kwa afya ya binadamu.

Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika ambazo matatizo ya mabadiliko ya tabia ya nchi, yameathiri uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwamo mahindi.

Sambamba na hilo, tatizo la magonjwa ya mimea na wadudu nalo limekuwa likichangia hasara kwa wakulima wengi, hali ambayo imekuwa ikiwasababishia hasara hasa wanapokosa mbinu za kukabiliana nao.

Mwishoni mwa mwaka jana, watafiti wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ushirikiano na Tume ya Taifa ya Sayansi na teknolojia (COSTECH) walipanda mahindi ya majaribio, yaliyozalishwa kwa njia ya uhandisi jeni (GMO).

Majaraibio ya mahindi haya yanayovumilia ukame, yalifanyika katika kituo cha utafiti wa kilimo cha Makutupora mkoani Dodoma.

Utafiti huo ambao ni moja ya juhudi za kufuta suluhisho la changamoto ya ukame na mvua kidogo inayowakumba wakulima wengi wa mahindi nchini, umevuta hisia za watu wengi hususani wakulima wa zao hilo, wengi wakitaka kujua maendeleo yake na namna wanavyoweza kunufaika na matokeo ya utafiti huo hasa upande wa mbegu.

Kila aliyefika kituoni hapo na kujionea jinsi mahindi hayo yanayostahimili ukame yalivyostawi na kuvumilia ukame wa mkoa wa Dodoma, amekuwa na shauku ya kutaka kujua ni lini mbegu zitawafikia wakulima, wanaopata tabu kutokana na tatizo la ukame katika maeneo mengi.

Hali inakuwa ya kukatisha tamaa pale wanapoambiwa kuwa utafiti huo unaendeshwa kwa sheria kanuni na taratibu za nchi yetu ambazo kiutekelezaji mbegu hizo zinaweza kuwafikia wakulima mwaka wa fedha wa 2021/2022.

Dk Alois Kulaya ni mtafiti mshauri wa mradi wa mahindi yanayotumia maji kwa ufanisi (WEMA), anasema baada ya kupata takwimu kwenye maeneo ya wakulima watalinganisha takwimu walizozipata kwenye maeneo hayo na zile walizozipata awali kwenye kituo cha utafiti wa kilimo Makutuporana. Na endapo zitakuwa sawa ndipo wataanza mchakato ili ziweze kupitishwa kama mbegu.

Anasema wakati utafiti huo ukiendelea kwenye mashamba ya wakulima, wao kama watafiti wataanza uzalishaji wa mbegu za awali ili pale zitakapopitishwa tayari wawe na mbegu mama za kuanzia ambazo zitapewa kampuni ya uzalishaji wa mbegu kwa ajili ya kuzalisha mbegu

Mtafiti huyo anaongeza kuwa baada ya wao kumaliza majaribio yao mwaka 2020, wataikabidhi Taasisi ya udhibiti wa mbegu nchini (TOSCI).

Taasisi nayo itatakiwa kupanda msimu mmoja ili kujiridhisha kama taarifa zilizotolewa na watafiti ni sawa na kisha kuiruhusu kuwa mbegu.

‘’Baada ya kujiridhisha sasa ndio mbegu hizo bora za mahindi yanayostahimili ukame na kupambana na bungua wa mahindi zitaruhusiwa kuwa mbegu mwaka 2012/2022, ‘’ anasema.

Mahindi hayo ambayo sasa utafiti wake unaendelea nchini , kwa nchi kama Afrika ya Kusini wakulima wake tayari wameshaanza kuyalima na kuyatumia kama chakula.

Kimsingi, mahindi ya GMO yameonyesha kuwa na uwezo wa kutoa mavuno asilimia 14 hadi 29 zaidi kuliko mahindi ya kawaida ambayo hayakuboreshwa

Wakati wakulima wakitaka mbegu hizo kupatikana kwa haraka, watafiti wanasema kufupisha muda wa utafiti inawezekana, kwani kwa mujibu wa sheria za nchi za jumuiya ya SADC ambayo Tanzania ni mwanachama, zinaruhusu utafiti kufanyika kwenye mazingira ya nchi hizo na kisha kutumika nchi yoyote kama nchi husika itahitaji.

Calvin Gwabara ni mwandishi mwandamizi wa masuala ya kilimo Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo, Morogoro. gwabarajr@yahoo.com, gwabarajr@gmail.com

Chanzo.Makala | Gazeti la Kiswahili linaloongoza Tanzania
 
KAMA SERIKALI IMERUHUSU MBEGU ZA MAHINDI YA GMO YATUMIKE NCHINI TANZANIA BASI TUTEGEMEE WA-TANZANIA WENGI BAADA YA MIAKA 5 IJAYO WATAKUWA NA MARADHI SUGU YASIYOWEZA KUTIBIKA MARADHI YA SARATANI, MARADHI YA KISUKARI, MARADHI YA PRESHA, MARADHI YA HEPATITIS B VIRUS. NI HATARI SANA. SIJUWI WAKEMIA WETU WAMELALA WAPI JAMANI?

Mbegu za mahindi ya GMO kumfikia mkulima mwaka 2021

By Calvin Gwabara, gwabarajr@gmail.com

View attachment 536310
Mahindi ya kutengenezwa kwa GMO niHatari kwa afya ya binadamu.

Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika ambazo matatizo ya mabadiliko ya tabia ya nchi, yameathiri uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwamo mahindi.

Sambamba na hilo, tatizo la magonjwa ya mimea na wadudu nalo limekuwa likichangia hasara kwa wakulima wengi, hali ambayo imekuwa ikiwasababishia hasara hasa wanapokosa mbinu za kukabiliana nao.

Mwishoni mwa mwaka jana, watafiti wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ushirikiano na Tume ya Taifa ya Sayansi na teknolojia (COSTECH) walipanda mahindi ya majaribio, yaliyozalishwa kwa njia ya uhandisi jeni (GMO).

Majaraibio ya mahindi haya yanayovumilia ukame, yalifanyika katika kituo cha utafiti wa kilimo cha Makutupora mkoani Dodoma.

Utafiti huo ambao ni moja ya juhudi za kufuta suluhisho la changamoto ya ukame na mvua kidogo inayowakumba wakulima wengi wa mahindi nchini, umevuta hisia za watu wengi hususani wakulima wa zao hilo, wengi wakitaka kujua maendeleo yake na namna wanavyoweza kunufaika na matokeo ya utafiti huo hasa upande wa mbegu.

Kila aliyefika kituoni hapo na kujionea jinsi mahindi hayo yanayostahimili ukame yalivyostawi na kuvumilia ukame wa mkoa wa Dodoma, amekuwa na shauku ya kutaka kujua ni lini mbegu zitawafikia wakulima, wanaopata tabu kutokana na tatizo la ukame katika maeneo mengi.

Hali inakuwa ya kukatisha tamaa pale wanapoambiwa kuwa utafiti huo unaendeshwa kwa sheria kanuni na taratibu za nchi yetu ambazo kiutekelezaji mbegu hizo zinaweza kuwafikia wakulima mwaka wa fedha wa 2021/2022.

Dk Alois Kulaya ni mtafiti mshauri wa mradi wa mahindi yanayotumia maji kwa ufanisi (WEMA), anasema baada ya kupata takwimu kwenye maeneo ya wakulima watalinganisha takwimu walizozipata kwenye maeneo hayo na zile walizozipata awali kwenye kituo cha utafiti wa kilimo Makutuporana. Na endapo zitakuwa sawa ndipo wataanza mchakato ili ziweze kupitishwa kama mbegu.

Anasema wakati utafiti huo ukiendelea kwenye mashamba ya wakulima, wao kama watafiti wataanza uzalishaji wa mbegu za awali ili pale zitakapopitishwa tayari wawe na mbegu mama za kuanzia ambazo zitapewa kampuni ya uzalishaji wa mbegu kwa ajili ya kuzalisha mbegu

Mtafiti huyo anaongeza kuwa baada ya wao kumaliza majaribio yao mwaka 2020, wataikabidhi Taasisi ya udhibiti wa mbegu nchini (TOSCI).

Taasisi nayo itatakiwa kupanda msimu mmoja ili kujiridhisha kama taarifa zilizotolewa na watafiti ni sawa na kisha kuiruhusu kuwa mbegu.

‘’Baada ya kujiridhisha sasa ndio mbegu hizo bora za mahindi yanayostahimili ukame na kupambana na bungua wa mahindi zitaruhusiwa kuwa mbegu mwaka 2012/2022, ‘’ anasema.

Mahindi hayo ambayo sasa utafiti wake unaendelea nchini , kwa nchi kama Afrika ya Kusini wakulima wake tayari wameshaanza kuyalima na kuyatumia kama chakula.

Kimsingi, mahindi ya GMO yameonyesha kuwa na uwezo wa kutoa mavuno asilimia 14 hadi 29 zaidi kuliko mahindi ya kawaida ambayo hayakuboreshwa

Wakati wakulima wakitaka mbegu hizo kupatikana kwa haraka, watafiti wanasema kufupisha muda wa utafiti inawezekana, kwani kwa mujibu wa sheria za nchi za jumuiya ya SADC ambayo Tanzania ni mwanachama, zinaruhusu utafiti kufanyika kwenye mazingira ya nchi hizo na kisha kutumika nchi yoyote kama nchi husika itahitaji.

Calvin Gwabara ni mwandishi mwandamizi wa masuala ya kilimo Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo, Morogoro. gwabarajr@yahoo.com, gwabarajr@gmail.com

Chanzo.Makala | Gazeti la Kiswahili linaloongoza Tanzania
Sheikh & Mzee mwenzangu wa Dawa za Kisunni mboni unaniangusha? Mbona kichwa cha habari haviendani na maudhui ya post yenyewe?
 
Hii ni hatari GMO inaleta madhara makubwa ya kiafya na mazingira.Madhara ya kiafya ni mengi organ disruption,cancer na pia kuna uhusiano mkubwa kati ya GMO seed na autism,watoto wanazaliwa na ulemavu wa ubongo.Serikali haijajiandaa kutatua matatizo yanayoletwa na GMO,haina health facility,hakuna wataalamu,hatuna elimu ya GMO,hatuna sera za kuilinda jamii na madhara ya Sayansi zilizokwama kama nchi za wenzetu.Hatuna vituo vya tafiti zetu za kujitegemea tunategemea msaada kutoka nje. GMO ni business na ipo kwa ajili ya financial interest so sisi tunafanywa kama soko tu kwa ajili ya hizi kampuni.Kwa matatizo yote tuliyonayo GMO haiwezi kutusaidia bali itatuongezea matatizo mapya ambayo hatunayo sasa hivi.Na pia sasa hivi nchi zilizoendelea zinafanya campaign kubwa kupinga mbegu za GMO iweje leo hii tuone ni suluhu.Viongozi wetu hebu kaeni mfikirie upya tena ,you still have time please no GMO.
 
hao wasomi SAA nyingine ni majanga makubwa yaani wanashindwa kutambua madhara ya hii kitu kwanza Tanzania hatuna uhaba wa chakula kama wanavyotuaminisha kuna sehenu vyakula vinaharibika wa kukosa usafiri na masoko
 
Jaman kama ni kweli hizi ni hatar tuungane kwa pamoja wanajf kupiga kauli mbiu kupinga mpango wa serikali kupitisha mbegu hizo...tusizungumzie hawa wasomi maana tayar wameshapewa semina na marupurupu kipao kiasi kwamba jambo la kweli linakuwa la uongo na la uongo ndo linakuwa la kweli...mungu atunusuru na impact ya wasomi aina hii.
 
Mchele na mayai ya plastic, madawa hatarishi ya kilimo na binadamu ukigeuka huku ukutane na GMO....twafaaaa

Ila wasomi wetu na viongozi watambue maisha ni zaidi ya fedha na utajiri.

No to GMO please!

Mungu tupiganie waja wako maana wewe wajua dhamiri za walioko nyuma ya mpango huu.
They will never succeed in the name of the Most High.
 
Back
Top Bottom