leonaldo
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 2,583
- 3,181
Ni wazi kuwa mgogolo wa UDA haujaanza leo umelitesa sana bunge lilopita bila kupata ufumbuzi wa kudumu katika jambo hili.
Juzi juzi nilimsikia mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano akisema kwa u uchungu kabisa kuwa hawezi kuruhusu ujanja ujanja uliokuwa umefanywa dhidi ya UDA uendelee na kwamba watu walitaka kujimilikisha hisa hata za serikali kwa njia za udanganyifu. Pili asingekubali watanzania wabebeshwe deni la zaidi ya bilioni 300 kama mkopo kujenga barabala za mmabasi ya haraka harafu afaidike kampuni binafsi Simon group (UDA) sasa maswali ya kujiuliza
Nawashauri kama ndugu itafuteni haki ya wana wa Dar es salaam msipoitafuta hiyo kiki mnayoiogopa ukawa wataipata mahakamani na hiyo itakuwa ni bonge la kiki hakuna mahali uvunjaji wa sheria unaweza kuhalalisha matoke ndio maana mmezipata za kwenu zingekuwa halali hata hizo angekatalia. Kuna wingu la utapeli mkubwa kwa mda mrefu sana sasa tunataka ifike mwisho.
Nawasilisha

- Endapo simon group walifanya jaribio la kutaka kujimilikisha share 100% kwa njia zisizo halali ni nini kitatufanya tuamini kuwa 51% ya jiji waliipata kwa njia halali?
- Kama utaratibu wa kuuza share haukufuatwa kwa nini tuchukulie kuwa share 49% sio halali na 51% ni halali
- serikali inadai kuwa hakuna kikao cha baraza la mawazili kilipitisha uuzaji wa shirika la UDA kama sheria na taratibu zinavyotaka, je kama sheria haikufuatwa ni nini kinahalalisha ubinafsishaji huo kama mfulu anavyodai.
- Toka lini meya wa jiji yuko juu ya sheria kwamba maamuzi yake hata kama yatavunja sheria za nchi au jiji basi ihesabike kuwa ni maamuzi halali?