Kama Serikali haijali kilimo, kuna haja gani ya kuwa na Wizara ya Kilimo?

lingamba lidodi

JF-Expert Member
Nov 15, 2018
964
1,137
Rais Magufuli, Rais wa wanyonge, watu tuna maswali mengi juu ya serikali yako.

Kama serikali haijali sekta ya kilimo ambayo imeajiri wanyonge kwa 75% kuna haja gani ya kuwepo Wizara ya kilimo na umwagiliji?

Tanzania tuna mito inayotiririsha maji mwaka mzima na mingine wakati wa masika. Wizara husika haijui hilo?

Kwanini tutegemee mvua huku ikifahamika kuwa uharifu wa mazingira umesababisha upungufu mkubwa wa mvua?

Pesa zilizonunulia ndege zingepelekwa kujenga miundombinu ya umwagiliaji leo hii tungekuwa tunazungumzia mvua chache kwa kilimo na kwamba kutakuwa na njaa?

Huoni kuwa mmewaingiza hao wanyonge kwenye janga la njaa huku wakishangilia kwa lazima ndege zikiruka angani?

UKWELI HALI NI MBAYA MASHAMBANI.

KAMA KILIMO HAKINA TIJA KWA TAIFA, FUTA WIZARA YA KILIMO INATAFUNA PESA ZA WAVUJA JASHO BILA FAIDA.

Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom