Kama Saudi Arabia na Vatican wameweza kufanya ibada majumbani sisi tuliopokea dini toka kwao tunashindwa nini?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,850
141,769
Jana nilimsikia Prof Lipumba akisema yeye ameanza kuswalia nyumbani ili kuepuka misongamano inayoweza kusababisha maambukizi ya Covid 19.

Binafsi nikawa nimemwelewa vilivyo.

Ndipo nikaanza kutafakari, kama Waislamu kule Saudia wanaswalia nyumbani Bakwata wanashindwa nini?

Kama Wakristo kule Vatican, UK na Germany wanasalia majumbani hawa Katoliki, Anglican na KKKT wanafeli wapi?

Kama Walokole huko USA wanasalia majumbani hawa kina Kakobe, Gamanywa, Gwajima, Mwingira wanashindwa nini?

Kuna wakati yatupasa kutumia busara hata kama mamlaka za juu zimewaachia hiyo fursa bado mnatakiwa kutumia hekima ya Mungu kutenda jambo sahihi.
Serikali haiwezi kuwakataza directly lakini nyie mmebarikiwa macho ya rohoni na mwilini na hata hao wagonjwa 88 waliotangazwa hadi sasa ni waumini wenu.

Hekima ya Mungu wa mbinguni na iwe juu yenu!
 
Ninachokijua tu ni kwamba ukiwa na Imani ya kweli kwa Mwenyezi Mungu / Allah hata ukisalia Sebuleni au Chumbani Kwako au Bustanini Kwako au hata Stoo basi Dua yako inakubaliwa na unabarikiwa vizuri tu. Huko kwenda Makanisani na Misikitini mara nyingine huwa ni Mbwembwe tu zilizochanganyika na Unafiki mwingi ndani yake.

Kama kuna Jambo ninaloilaumu Serikali yetu na sipendezwi nalo hata kidogo ni Kitendo cha Kuruhusu Ibada za Misikitini na Makanisani iendelee. Nina uhakika kama wasipoliangalia hili kwa marefu na mapana yake Waumini wengi wanaojazana huko / humo wataanza Kufa Siku si nyingi. Yaani Serikali inashindwa Kuzuia Ibada huko katika Nyumba za Ibada kwa sasa kwasababu inahofia Kuchukiwa na Kupoteza kama pia si Kuyimwa Kura nao.

Siasa inaharibu utaratibu mzima wa Kiafya hasa mbele ya Janga hili baya na hatari la COVID-19. Asante sana Mdau kwa hili Bandiko lako kwani ni zuri, sahihi na uliyoyaanisha hapa yana ukweli mtupu. Hongera Umenena!
 
Unajua ukishakiri kua yesu ni bwana na mwokozi wa maisha yako unakua umetangaza vita na shetani, na shetani atajaribu kufanya kila njama za kukuporomosha hapo juu ulipo

Unajua kwamba shetani kapewa mamlaka ya kumjaribu binadamu na katika hili shetani kaamua kutumia huu ugonjwa kama jaribio ili kuwateka watu?

Unajua kukubali kusalia nyumbani kwa kuogopa maambukizi ambayo yamepangwa na shetani ni ishara kwamba shetani amekushinda nguvu na umekosa imani ya kupambana naye?

Unaelewa kwamba namna pekee ya kumshinda huyu shetani ilitakiwa yeyote yule ambaye amemkiri yesu kua bwana na mwokozi wa maisha yake ajitokeze katika wodi za wagonjwa wa corona kwa lengo la kuwafanyia sala ya toba kwa kuwashika vichwani?

Mnakumbuka kua ukiwa na yesu hakuna lishindikanalo maana amewaahidi kutengeneza njia mahala pasipo na njia?
 
Viongozi wa serikali ya ccm wanawaacha viongozi wa dini kuendelea na shughuli zao, ili baadae watakapochezea box la kura viongozi wa dini wasiweze kufungua mdomo. Hiyo ni rushwa ili uovu wao ufumbiwe macho na viongozi wa dini huko mbeleni.

Viongozi wa dini stukieni huo mtego, labda kama viongozi wa dini mmekubali kufumbia macho uovu utakaorndeshwa na watawala.
 
Ninachokijua tu ni kwamba ukiwa na Imani ya kweli kwa Mwenyezi Mungu / Allah hata ukisalia Sebuleni au Chumbani Kwako au Bustanini Kwake au hata Stoo basi Dua yako inakubaliwa na unabarikiwa vizuri tu. Huko kwenda Makanisani na Misikitini mara nyingine huwa ni Mbwembwe tu zilizochanganyika na Unafiki mwingi. Kama kuna Jambo ninaloilaumu Serikali yetu na sipendezwi nalo hata kidogo ni Kitendo cha Kuruhusu Ibada za Misikitini na Makanisani iendelee. Nina uhakika kama wasipoliangalia hili kwa marefu na mapana yake Waumini wengi wanaojazana huko / humo wataanza Kufa Siku si nyingi. Yaani Serikali inashindwa Kuzuia Ibada huko katika Nyumba za Ibada kwa sasa kwasababu inahofia Kuchukiwa na Kupoteza kama pia si Kuyimwa Kura nao. Siasa inaharibu utaratibu mzima wa Kiafya hasa mbele ya Janga hili baya na hatari la COVID-19. Asante sana Mdau kwa hili Bandiko lako kwani ni zuri, sahihi na uliyoyaanisha hapa yana ukweli mtupu. Hongera Umenena!
Viongozi wa dini hawawezi kupinga wao wanachojali ni sadaka tu, kuna msikiti wilayani Kondoa wamefunga hadi hii sekeseke iishe, viongozi wa huo msikiti wanajitambua, kwao afya za waumini wao ni Bora kuliko tamaa ya sadaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viongozi wa serikali ya ccm wanawaacha viongozi wa dini kuendelea na shughuli zao, ili baadae watakapochezea box la kura viongozi wa dini wasiweze kufungua mdomo. Hiyo ni rushwa ili uovu wao ufumbiwe macho na viongozi wa dini huko mbeleni. Viongozi wa dini stukieni huo mtego, labda kama viongozi wa dini mmekubali kufumbia macho uovu utakaorndeshwa na watawala.
Viongozi wa dini karibia wote ni CCM!
 
Tatizo ni akili za viongozi wetu wa serikali. Waliidharau covid wakidhani ni "kagonjwa kanakowahusu mabeberu" tu.

Viongozi wa dini si kwamba hawajui nini cha kufanya, bali wanadhani wakifanya tofauti na serikali inavyotaka ni kumpinga Magu na serikali yake.

Ndio maana hotuba za pasaka ziliishia kumpongeza Magu kwa maamuzi ya kuruhusu mikusanyiko ya ibada kana kwamba ametoa garantii corana haitaingia kwenye nyumba za ibada na waumini watapata nafuu ya maambukizi.
 
Saudi Arabia hawakuanzisha dini yoyote. Saudi Arabia ni nchi iliyoanzishwa juzi juzi tu 1932, na wale wale walioianzisha Israel.

Kama vitu huvijuwi ni heri ukafanya japo utafiti kwa kutumia Google tu kabla hujakurupuka na ku "offend' dini zisizo kuhusu.
 
Sisi sote tunajua Mungu ni muweza wa yote. Lakini yatupasa pia kutambua ni Mungu huyo huyo ametujalia neema ya kuwa na akili na ufahamu ili tufanye kazi.

Mungu kukuepusha kuna namna nyingi. Anaweza kukuponya ukiugua, anaweza kukufanya usiambukizwe, lakini ni kwa kutii maelekezo yake. Maelekezo yake tunayapokea vipi?

Tangu kale, Mungu alitumia malaika na manabii. Na zaidi manabii. Hata alipotaka kuuadhibu Ulimwengu, wale aliotaka wasiunganishwe katika angamizo aliwapelekea ujumbe. Hata ujumbe ulipopelekwa, wengi mioyo yao ilikuwa migumu.

Hawa wanaotuambia cha kufanya ili tusiangamie, waweza kuwa ndio manabii wa leo.
 
Back
Top Bottom