Kama sababu ni hii basi ‘’Kolomije boy’’ hawezi kutumbuliwa!

Hii stori imetungwa kwa maslahi maalumu yenye faida kisiasa. Hongera sana mwandishi kuna kitu umekilenga na umefanikiwa kwa kiasi fulani.
 
Nimenistuka na kushangaa sana baada ya kuambiwa sababu ya mahusiano ya karibu kati ya ‘’buldoza’’ na ''mwana mpendwa'' wa kisiasa. Madudu aliyoyafanya na anayoendelea kuyafanya‘’mwana mpendwa’’ huku akiendelea kuwa ‘’governor’’ wa ‘’Bandari salama’’ yamenifanya nidhani kuna mantiki katika maelezo niliyoyasikia.

Nimeambiwa hata bifu kati la watendaji wakuu ''vikongwe'' wa chama halijaanza jana bali lilianza wakati ya kampeni za kuingia kwenye ‘’nyumba nyeupe’’ mwaka 2015.

Nimeambiwa ile helikopta iliyoishia angani na kumuondoa duniani ambaye kwa habari za ndani ndiye alikuwa chaguo la ‘’buldoza’’ awe Kiongozi wa Shughuli za Serikali ndani na nje ya Bunge ilikuwa ndio chanzo cha bifu kwa sababu ilipangwa ‘’buldoza’’ aitumie katika kampeni.

Nimeambiwa bifu hili lilichagizwa na ukweli kuwa chaguo la kwanza la ‘’mzee wa meno ya tembo’’ kwenye nafasi ya ugombea ‘’nyumba nyeupe’’ alikuwa ni ‘’maembe’’.

Nimeambiwa ‘’ mwezi wa kwanza marope’’ na ‘’Mzee wa meno ya tembo’’ walijua helikopta ni ‘’bomu’’ ambalo lingeweza kumpasukia ‘’buldoza’’.

Nimeambiwa ‘’mwana mpendwa’’ alikuwa pia kwenye timu ya ‘’Maembe’’ kabla ‘’buldoza’’ hajateuliwa kuwa mgombea wa ‘’nyumba nyeupe’’ kwa tiketi ya ‘’Chukua Chako Mapema’’ lakini baadaye akaanza kujipendekeza kwa ‘’buldoza’’ baada ya ‘’buldoza’’ kuteuliwa kuwa mgombea kwa tiketi ya ‘’Chukua Chako Mapema’’.

Nimeambiwa baada ya ‘’mwana mpendwa’’ kunusa nusa tetesi hizo kutoka kwenye ''timu maembe'' alimtahadharisha haraka ‘’buldoza’’ ili aweze kuaminika zaidi kwa sababu ‘’buldoza’’ alimjua kuwa ni ‘’timu maembe’’.

Nimeambiwa ‘’mwana mpendwa’’ ni mnafiki na opportunist mzuri sana kiasi kwamba kundi kubwa la wana umoja wa vijana wa ‘’chukua chako mapema’’ hawampendi kwa sababu amewageuka wengi na kuwaumiza kisiasa.

Nimeambiwa ‘’buldoza’’ baada ya kupata kionyo akaachana na ratiba ya kampeni za anga kwa kisingizio kuwa yeye ana ‘’flying phobia’’ kutokana na alimanusra ya ajali iliyohusisha pia makamu wa ‘’nyumba nyeupe’’, Mkuu wa ‘’bandari salama’’na mkuu wa ‘’wavaa magwanda ya khaki bandari salama’’ kwenye ajali ya helikopta wakati wakiangalia athari za mafuriko ‘’bandari salama’’ mwaka 2014.

Nimeambiwa dhumuni kuu la kukodisha moja ya ‘’bomu’’ lilikuwa ni kurudi tena kwenye vikao vya chama ili kupata mgombea mwingine baada ya ‘’bomu’’ kumpasukia‘’buldoza’’ angani.

Nimeambiwa ‘’Mzee wa meno ya tembo’’ alijua kama wangerudi tena kwenye vikao vya chama basi aliyekuwa mbunge wa ‘’millet’’ angechaguliwa kuwa mgombea wa ‘’nyumba nyeupe’’ huku ‘’mwezi wa kwanza marope’’ akiteuliwa kuwa kiongozi wa shughuli za serikali bungeni na nje ya bunge

Nimeambiwa ‘’Mwezi wa kwanza marope’’ yeye alijua wakirudi kwenye vikao vya chama atachaguliwa yeye kuwa mgombea ‘’nyumba nyeupe’’ badala ya aliyekuwa mbunge wa ‘’millet’’.

Nimeambiwa baada ya ‘’buldoza’’ kuamua kuachana na kampeni za helikopta, ‘’mwezi wa kwanza marope’’ alitumia tena mwanya mwingine na kumshawishi aliyekuwa rafiki wa karibu wa ‘’mwami wa Kigoma’’ Bungeni kuitumia helikopta hiyo katika kampeni zake wakati hata jimbo lake katika mkoa wa ‘’midzombe’’ halikuwa na upinzani mkubwa.

Nimeambiwa nia ya ‘’Mwezi wa kwanza marope’’ kumshawishi kutumia helikopta ilikuwa ni kuitaka kazi ya Kiongozi wa Shughuli za Serikali ndani na nje ya Bunge apewe yeye baada ya ‘’bomu’’ kumlipukia rafiki wa karibu wa ‘’mwami wa kigoma’’ bungeni kwa sababu alinusa kuwa ndiye chaguo la ‘’buldoza’’ kwenye nafasi hiyo baada ya ''filikumidzombe'' kutoa siri kwa ''mwami wa kigoma'' ambaye naye akamweleza siri hiyo rafikiye ''mwezi wa kwanza marope''.

Nimeambia mnuso wa ‘’mwana mpendwa’’ ulikuwa ‘’vindicated’’ baada ya ‘’bomu’’ hilo kulipuka angani na kuua wasafiri wote waliokuwemo ndani yake. ‘’Vindication’’ hii ndio ilizaa ‘’MWANA MPENDWA’’.

Nimeambia kuwa mbunge wa sasa wa ‘’millet’’ alikuwa pia ni kipenzi cha ‘’buldoza’’ lakini sakata la ‘’mawingu media’’ lilimfanya ‘’buldoza’’ akosane na mbunge huyo baada ya ‘’mwana mpendwa’’ kufanikiwa kumfitini kwa ‘’buldoza’’ kuwa anashirikiana na wapinzani wake kuweka shinikizo ili aonekani ‘’mwana mpendwa’’ hafai na amtumbue kwa manufaa ya wapinzani.

Nimeambiwa ‘’buldoza’’ baada ya kuwauliza waliokodi moja ya ‘’bomu’’ kutoka General Aviation Services Ltd walisema hawakujua lilikuwa ni ‘’bomu’’. Tukio hili lilisababisha mpaka CEO wa General Aviation Service Ltd akaachia ngazi mwaka 2016.

Nimeambiwa kwa vile ‘’buldoza’’ ni mzuri kwenye visasi kama utamchokoza, basi tukio hilo lilimfanya awachukie wale wote walihusika kwa namna moja au nyingine na ukodishaji wa moja ya ‘’bomu’’.

Nimeambiwa baada ya ‘’buldoza’’ kutangaza jina la ‘’saada’’ kuwa ndiye kiongozi wa shughuli za serikali bungeni na nje ya bunge, ‘’mwezi wa kwanza marope’’ alianza kumkejeli ‘’buldoza’’ huku akitumia ujumbe wa picha na katuni kwa sababu aliamini yeye ndiye angeteuliwa kwenye nafasi hiyo baada ya ''filikumidzombe'' kuiacha dunia.

Nimeambiwa ‘’buldoza’’ alimuacha ‘’Mwezi wa kwanza marope’’ nje ya kabineti la kwanza lakini ‘’mzee wa tabasamu’’ akamuomba ‘’buldoza’’ asimuache nje. ‘’buldoza’’ kwa shingo upande akaamua kumpa wizara isiyokuwa na maslahi ya kisiasa na mguso wa karibu kwa wananchi wa chini.

Kwangu mimi tuhuma hizi ni nzito ambazo zinahitaji kuwashirikisha wanaJF ili tujue ukweli wake.

Je, hizi tuhuma niza kweli au ni kile waingereza husema, ‘’conspiracy theory’’.

Nimalizie mada yangu kwa maneno ya wahenga yanayosema, ‘’Mjumbe hauwawi’’. Waingereza husema, ‘’don’t shoot the messanger’’!
Huu ni umbeya tu wala hauna ukweli wowote
 
February alikitaka sana cheo fulani kikubwa, masikini ya Mungu akasahau kuwa riziki halali ya mtu anayeigawa ni yule tunayempigia magoti ijumaa na jumapili.

Somo zuri sana kwa wanasiasa vijana wanaoibuka miaka hii ya sasa.
Mkuu;
Wanasiasa huwa hawana somo lolote kwa sababu siasa hazina fomyula na sheria!
 
Theory hii inaweza kuwa na ukweli ndani yake. Kuna mambo yalitendeka baada ya Bulldoza kingia Magogoni siku za kwanza ambayo yamenifanya nifungue macho. BTW kwanini ''mzee wa tabasamu'' alikuwa na wasiwasi sana na akawa anarudi Magogoni mara mbili mbili kama amesahau kitu?
Reply yako imenisidia kuelewa "mzee wa tabasamu" ni nani. Lol! Hizi codes inabidi kuzichukulia dararasa kabisa!!
 
Makonda hakuanzia hapo alipo leo,Kapitia kwa watu maarufu wengi,akina Mzee Six,kaja kwa mtoto wa JK.
Kamzaba makofi Jaji/Waziri Mkuu mstaafu/Bwana Katiba mpya makofi na matusi hadharani,vyombo vya ulinzi na usalama viligwaya.Watu walilaani kitendo cha kumzaba makofi Mzee Warioba lakini,kwa jeuri tena kwa makeke Raisi JK akampa UDC Kinondoni.
Millet na Marope hawakujua nguvu ya Makonda.
Makonda atazidi kudunda hadi 2025 tupende tusipende labda yeye aamue kuachia ngazi.
Makonda is very ambitious man,sitashangaa nikisikia ni Waziri wa Mambo ya ndani,au Waziri Mkuu,hata kiongozi no.1 wa nchi.
Umesema Millet na Marope hawakujua nguvu ya Makonda!

Nguvu yake ni ipi? Nieleweshe?
 
Magazeti ya bongo yangeandika hilo tukio la kukamatwa kwa hao wauaji wa deo,labda kama wamefungwa kwa kesi ya ujangili
Habari za jioni wakuu!

Nimeambiwa ajali ya ndege haikusababishwa na bomu lililolipuka ndani ya ndege wala Fili hakupambana na mabaunsa waliotumwa kummaliza ndani ya ndege.

Nimeambiwa ajali ya ndege ilisababishwa na majangili wenye silaha waliokuwa wanawinda ndani ya pori la akiba la selous

Nimeambiwa ndege ilikuwa inapaa kuelekea mahali walipo majangili. Majangili walihisi ndani ya ndege kuna askari wanataka kuwakamata majangili hao.

Nimeambiwa jangili mwenye silaha aliilipua ndege kwa lengo la kujihami ili wasikamatwe. Watu wote waliokuwa ndani ya ndege walipoteza maisha.

Nimeambiwa jangili aliyetungua ndege alikuwa anasimulia mkasa huo akiwa amelewa kwenye vilabu vya pombe kijijini.

Nimeambiwa habari zilienea kwa kasi zikawafikia watu wa vyombo vya ulinzi na usalama kwenye maeneo anayoishi.

Nimeambiwa mtu aliyetungua ndege akiwa amelewa, alikuwa anaropoka na kuwataja watu aliokuwa nao porini siku hiyo.

Nimeambiwa watu wa vyombo vya ulinzi na usalama walikuja kumkamata mtu aliyetungua ndege na watu wote aliokuwa nao aliwataja nao wakakamatwa kwa nyakati tofauti tofauti.

Nimeambiwa wahusika wote wapo jela wanatumikia kifungo cha maisha.

Je, habari hizi ni za kweli? Kama kuna mtu mwenye taarifa kamili naomba atujuze ili tupate ukweli!

Mjumbe hauwawi!!!!!!!!

Mshua.
 
Labda anamcha mungu wa burigi
Siyo uchawi kabisa, Rais Dr Magufuli ni mcha Mungu saaaana, ila kumbuka binadamu mbaya akishindwa kukuloga/kuchafua sifa yako, atakupachika sifa ‘ jamaa mchawi, jamaa mshirikina’ kwa sababu tu ya kushindwa kukufanyia mabaya. Kwa hiyo kama mnashindwa kufanyia mabaya Mhe Makonda au Rais wa nchi ni kwa sababu ya nia zenu mbaya!! I believe you have understood me!! Hence leave Makonda alone. Struggle for your survival and genuine and legal means of getting your daily bread!!! Period.
 
Kwa hulka yetu watanzania tunavyopenda umbea, hii stori ni tamu sana! Si rahisi kuruka hata neno moja hata kama "Saada" hujamfahamu itabidi utafute mtu yeyote umfix hapo ili uendelee na uhondo wa masimulizi... Anyway Fili ali-R.I.P kwa tamaa ya Marope, tamaa ambayo hadi sasa inatuhakikishia kuwa yupo katika maumivu makali na chuki kuu kuliko ya shetani baada ya kubaki na ubunge akiwa na madeni chungu nzima.
 
Back
Top Bottom