Wasalaam Wana Jamii,
Nimefuatilia mijadala mingi kwenye hii forum na kuona watu wengi wakilaumu juu ya Uteuzi wa Mhe. Mnyeti kuwa RC - Manyara kwasababu eti anatuhumiwa (haijathibitika) kutoa rushwa kwa madiwani wa CDM ili wakihame chao na hivyo hakustahili kuteuliwa.Dhana hii imejengwa juu ya ushahidi uliowasilishwa TAKUKURU na Mhe. Nassari.
Baada ya kutafakari kwa kina, nimeona kimsingi walichofanya kina nassari dhidi ya mnyeti ni siasa na lengo lilikua ni kurudisha imani ya wananchi kwa chama chao ionekane madiwani hawakuhama kwa hiari yao au kwasababu walizotoa bali ni kwa kununuliwa/tamaa ya fedha. Well, hata kama ilifanyika hivyo nijuavyo mimi siasa ni maslahi (cheo, fedha n.k) hakuna mwanasiasa (hasa walio kwenye uongozi au wenye ushawishi mkubwa katika jamii) ambae ameshawahi kuhama chama chake kwenda kingine bila kufuata maslahi niliyoyataja na kabla ya kuhama ni lazima mazungumzo yafanyike kwenye chama anachohamia ili kujihakikishia kwamba maslahi yake yanazingatiwa.
Kuthibitisha haya, nitolee mfano kwa kujikumbusha wakati Bw.Lowassa anahamia CDM kutoka CCM. Kabla ya kuhama, yalifanyika mazungumzo ambayo mengine yalikua ya siri na mengine yalifanyika wazi ingawa hayakua public (yale yaliyofanyika bahari beach) lengo la mazungumzo yale pamoja na mambo mengine ilikua ni kumhakikishia Bw. Lowassa kwamba atakapohamia CDM basi atapewa nafasi ya kuwa mgombea urais na ikawa hivyo, japokua CDM ilikua tayari imeshakamilisha mchakato wa kumchagua mgombea urais wake na ilikua imebakia kuafikiana na UKAWA na kisha kumtangaza (rejea maelezo ya Dk.Slaa wakati anang'atuka CDM na ujio wa Lowassa).
Sasa tunapozungumzia rushwa kwa tafsiri isiyo rasmi ni kitu chochote mtu anachotoa kwa lengo la kupata kitu fulani kwa njia isiyo halali. Sasa swali la kujiuliza hapa ni ipi 'njia isiyo halali' hususan kwenye siasa. Je, kumpa ahadi mwanasiasa kwa kuzingatia maslahi yake ya kisiasa (fedha, cheo n.k) ili ahamie kwenye chama chako ni njia isiyo halali? kama tunakubaliana kwamba njia hii siyo halali basi tukubaliane pia kwamba hata Lowassa alihamia CDM kwa njia isiyo halali kwasababu alihama kwa lengo la kupata cheo/ nafasi ya kugombea u Rais aliyoahidiwa (vinginevyo asingehama). halikadhalika, kama tunaamini kwamba DC Mnyeti (sasa RC) kitendo chake cha kufanya mazungumzo na madiwani waliohama CDM na kutoa ahadi ili wahame chama chao ni kosa ambalo linahusiana na rushwa basi hata Kamati Kuu ya CDM, Mhe.Mbowe na washirika wao waliofanikisha lowassa kuhama CCM basi inabidi na wao washitakiwe kwa kosa hilo hilo la rushwa ya kumshawishi Lowassa ahamie kwenye chama chao ili apewe nafasi ya kugombea rais. Otherwise, kama tunasema njia iliyotumika kumshawishi Lowassa kuhamia CDM ilikua halali basi tuseme pia njia iliyotumika kuwashawishi madiwani ni halali.
Hivyo, Mhe. Mnyeti hakufanya kosa lolote na wala hatupaswi kuwashurutisha TAKUKURU kuchukua hatua dhidi yake kwa sababu ile haikua RUSHWA bali ni USHAWISHI uliozingatia maslahi ya kisiasa. Na kwa maana hiyo Mhe.Rais hakukosea kumteua kada mtiifu aliefanya kazi yake kwa uadilifu na werevu Mhe. Alexander Mnyeti kuwa RC mpya - Mkoa Manyara.
Naomba kuwasilisha.