Kama Raisi Magufuli na CCM hawataki mfumo wa vyama vingi nchini waseme wazi badala ya kufanya hujuma

Mimi ni mwana CCM ninayejitambua na ninayeitakia mema nchi yangu.I understand your concern brother na nadhani viongozi wetu wajuu chamani watalielewa hili na kulifanyia kazi. Kwa bahati nzuri Rais wetu analielewa hili vizuri sana.Wenye shida mimi naona ni hawa viongozi wetu wana Chama wa ngazi za chini.Ila point taken brother. Hii confrontational behavior haitatusaidia sana kwenye maendeleo yetu,ni lazima ikomeshwe.
Sasa kama kweli haya 'madudu' yanayofanywa na watendaji wa Rais, hayana blessings za Mkulu ni kwa nini hawatumbui?

Hakuna asiyejua kuwa Rais wetu ni mwepesi sana wa kuwatumbua watendaji wake hata kwa 'vijikosa' vidogo sana.

Sasa swali la msingi ni kwa nini mathalani ameendelea kumkumbatia RC wa Dar, pamoja na madudu yote aliyofanya, pamoja na kufoji vyeti na kuvamia Clouds media na askari wenye silaha?

Hakuna sababu ya kuguess guess, ukweli ni kuwa pamoja na Magu kupenda kujinadi kuwa yeye ni Rais wa wote kwa maana ya wanaccm na wale wa upinzani, lakini practically anafanya vice versa, kwa kuwa anaonyesha wazi kuwa anawachukia sana viongozi wa vyama makini vya upinzani na kuwaona kama 'wahaini' ndani ya nchi yetu!

Refer tamko lake majuzi alipomsifu Spika Ndugai jinai anavyowatimua wabunge wa upinzani na kumhakikishia kuwa akishawatimua huko Bungeni na yeye huku uraiani atawashughulikia ipasavyo!

Ni ukweli usiopingika kuwa huu ufa anaoutengeneza Magu kwa kuligawa Taifa hili kwa misingi ya itikadi za siasa na ukanda, utakuja kuleta madhara makubwa sana siku za usoni.
 
Wasiwasi wangu ni kwamba awamu hii itazaa Kibiti nyingi sana
Mkuu nilikutana na wachaga mkoa flani wanalalamika kuwa awamu hii wanaonewa sana hasa baada ya mbowe kuharibiwa shamba lake, wamechukia sana
 
Sasa kama kweli haya 'madudu' yanayofanywa na watendaji wa Rais, hayana blessings za Mkulu ni kwa nini hawatumbui?

Hakuna asiyejua kuwa Rais wetu ni mwepesi sana wa kuwatumbua watendaji wake hata kwa 'vijikosa' vidogo sana.

Sasa swali la msingi ni kwa nini mathalani ameendelea kumkumbatia RC wa Dar, pamoja na madudu yote aliyofanya, pamoja na kufoji vyeti na kuvamia Clouds media na askari wenye silaha?

Hakuna sababu ya kuguess guess, ukweli ni kuwa pamoja na Magu kupenda kujinadi kuwa yeye ni Rais wa wote kwa maana ya wanaccm na wale wa upinzani, lakini practically anafanya vice versa, kwa kuwa anaonyesha wazi kuwa anawachukia sana viongozi wa vyama makini vya upinzani na kuwaona kama 'wahaini' ndani ya nchi yetu!

Refer tamko lake majuzi alipomsifu Spika Ndugai jinai anavyowatimua wabunge wa upinzani na kumhakikishia kuwa akishawatimua huko Bungeni na yeye huku uraiani atawashughulikia ipasavyo!

Ni ukweli usiopingika kuwa huu ufa anaoutengeneza Magu kwa kuligawa Taifa hili kwa misingi ya itikadi za siasa na ukanda, utakuja kuleta madhara makubwa sana siku za usoni.
Rais ni binadamu kama mimi na wewe mkuu,at times he becomes infuriated. Tukubali kwamba wakati mwingine wapinzani wanaudhi sana,they become unnecessarily difficult!
 
Kwanini hakuwasiliana na mkuu wake ambaye ni mkurugenzi? Halafu sumaye alifuata nini?

Mkuu unashangaa Sumaye alifuata nini, mbona hushangai Polepole jana huko Pwani alipewa nafasi ya kumpokea mwanachama wa ACT aliyehama na kuhamia ccm? Yeye kule pwani alifuata nini, ilikuwa ni ziara ya kichama? Halafu rais eti anatuona watanzania wote ni watoto anakaribisha kama kuna mwanachama wa cdm, cuf, nccr nk kumpokoea mwanachama wa ccm au chama kingine kuhamia chama chake. Mkuu naona unatetea jinsi unavyopenda, lakini nikueleze ukweli kwa sasa mkuu wetu wa nchi ukiachia mambo mazuri machache anayoyafanya lakini penda usipende ndiye anayapandikiza kwa kasi ya ajabu siasa za chuki ndani ya nchi hii. Huwezi elewa hili kulingana na upande uliosimamia kwa sasa.

Ila mimi sijali sana kwani nimejifunza kitu kwamba kutesa ni kwa zamu. Leo hii ungeweza kuamini kwamba Sumaye, Lowassa watalimia meno? Mkapa na JK ni kama kadi ya njano wameaanza kuiona. Huko mbeleni anaweza kuingia rais mwingine mwenye chuki zake za binafsi na hiki unachokiona leo ni sahihi akakifanya kibaya zaidi ya hiki na akakivika nguo nzuri ya uzalendo. Usishangae huyu rais unayedhani leo anafanya sawa akawa wakwaza kukutana na chuki hizo. Tunza hii post iko siku utayakumbuka maneno yangu.
 
Upinzani umekuwa too soft. The best way si kufa kikondoo. WaTz waandaliwe kisaikolojia kujitetea na kutetea viongozi wao pale haki inapovunjwa waziwazi.
Ule uonevu wa kule HAI kwenye bustani ya yule Mangi wa Cdm ni huruma. Yule jamaa hakupaswa kutoka salama hata kama angesindikizwa na vifaru. Upole wetu hautatuacha salama.
Naona sasa hivi kuna vikundi vya watu wanajifanya kuomba kiranja mkuu aongezewe muda. Hii janja ndo aliitumia best yake wa ile nchi ndogo hapo western ili aendelee kula mema ya jengo jeupe.
UKUTA umendoka na matumaini yote
Jamani tusiwe tunapotosha ukweli. Hivi ndivyo vurugu zinavyoanza nchini.

Kuhusu shamba la mheshimiwa Mbowe, alikwisha elezwa kuwa asiendelee na ule umwagiliaji naye akakubali na kuahidi atasitisha shughuli zake ifikapo Mei 23, 2017. Wakaguzi walipokwenda baada ya hii tarehe wakakuta ndio kwanza ameanza kupanda mazao mengine upya.

Sasa kwa hili wewe ungefanyaje kama serikali baada ya mtu kukaidi.

Kupandikiza mbegu za chuki ili serikali ionekane wabaya haitawasaidia CDM. Watafute tu mbinu mbadala za kuwakoga wananchi kama ilivyokuwa kabla ya uchaguzi wa 2015.
 
Mimi hata mukiokoa MAKINIKIA,ulete BOMBADIER umkamate Sethi na Ruge halafu uninyime UHURU WA KUJIELEZA,yote uliyofanya ni UBATILI MTUPU.Nipe uhuru wa kujieleza kwani ni haki yaki yangu ya msingi kama binadamu na iko kwenye sheria pia.
kweli mkuu. Walibya walipewa karibu kila kitu na Gaddaffi lakini bado walimng'oa sababu tu ya uhuru wao kuminywa!
 
What goes around comes around. Angalia kibiti. Soon nchi nzima itakuwa hivyo kwa ajili ya ccm kujenga chuki. Angalieni sana msilaaniwe kwa kuleta vita nchi hii.
Hapa unataka kutueleza kuwa haya mauaji ya mkoa wa Pwani yanafanywa na vyama vya upinzani (CDM, CUF, n.k.)?
 
kweli mkuu. Walibya walipewa karibu kila kitu na Gaddaffi lakini bado walimng'oa sababu tu ya uhuru wao kuminywa!
Huu nao ni upotofu wa ukweli. Qaddafi hakutolewa na Walibya bali alitolewa na multinationals waliotaka mafuta ya Libya. Angalia Walibya wenyewe wanavyoteseka sasa. Wanajuta kilichotokea.
 
Huu nao ni upotofu wa ukweli. Qaddafi hakutolewa na Walibya bali alitolewa na multinationals waliotaka mafuta ya Libya. Angalia Walibya wenyewe wanavyoteseka sasa. Wanajuta kilichotokea.

Mkuu kwani hao multinationals hawawezi kuja hapa? Wewe unasema multinationals lakini mauaji yalifanywa na mikono ya vijana wa Libya. Kwani hii nchi yetu hakuna raslimali ambazo hao multinationals wanazitaka?

Mimi naamini kilichomtoa Gaddafi kirahisi pia ni aina yake ya uongozi wa kujiona ni mzalendo kuliko wengine, hivyo aliona wengine hawastahili kuongoza nchi hiyo bali yeye tu. Tabia hiyo pia iko hapa nchini, kuna chama kinaona chenyewe ndio chenye haki ya kuongoza nchi hii kwa namna yoyote, na sasa imefikia hatua kuna uonevu wa wazi kwa wapinzani wa ukweli. Ni vyema tukatendeana haki kwa upendo bila kujali tofauti zetu za kisiasa kwani huu ufa unaojengwa kwa nguvu awamu hii unaweza kuchangia hao multinationals kutumia huo ufa kufanya yao. Nikuhakiishie jambo hilo ni rahisi sana kufanywa na wazungu kwani nchi zetu za kiafrika ni nyepesi kama pamba pindi wazungu wakiamau. Namna pekee ni kushikamana kama taifa na sio kuonyeshana umwamba wa kisiasa kisa uko madarakani.
 
Aelimishwe mara ngapi huku wana midomo michafu wakijidai wanapigania Uhuru? 48 hrs inawahusu hakuna namna mpk wanyooke.

Bahati mbaya hawatanyoka kama unavyodhani, ila watakuwa "hard core" na ni hatari sana amini nakwambia. Mwanadamu si punda tuna utashi na hata punda akiamua pamoja na kumbebesha mzigo na kumpiga hulala chini na ndio mwisho wa safari.
 
kwa kauli tata zilizotolewa na kiongozi wa bunge kwamba majimbo ya upinzani yqsipelekewe miradi ya maendeleo kwa kweli hakuna haja ya kuwa bunge kamwe. hatuwezi kuwa na mhimili wa bunge unaochochea ubaguzi kwa taifa letu kamwe.
 
Chuki na hujuma matokeo yake ndio hayo tunaona Kibiti. Sasa hawa wapiga raia na walemavu na wafunga wapinzani wameshindwa kudhibiti sehenu ndogo sana ya Kibiti - hii chuki ikiendelea ikazaa Kibiti nyingi zaidi watafanya nini?

Wanapasa kujiuliza sana. Kwa nini huko Kibiti ni watu wa CCM na Polisi tu wanauwawa? Soon or later kutakuwa na copy cats against serikali ya CCM, CCM wenyewe na polisi, sehemu nyingine zaidi ya Kibiti. It is just a matter of time wakiendelea hivi.

They must learn the hard way. Shauri yao. No sympathy there.

Hawataki kujifunza shauri yao.
 
Kwanini hakuwasiliana na mkuu wake ambaye ni mkurugenzi? Halafu sumaye alifuata nini?
Ninavyoelewa Meya ni mkubwa kuliko Mkurugeni. Kwa hiyo ni kama kusema Raisi anapaswa kupata kibali cha Waziri Mkuu.
 
Unajua huwezi kupewa tulia sindano ikuingie.


Aah wapi MKuu. Mie binafsi kuniambia niwe Mkuu wa Wilaya ni ku-insult my intelligence, kuniweka level moja na wale wachumba na mashemeji waliopewa ukuu wa wilaya. Unajua kuna wakati nchi hii watu wenye pesa walikuwa wanahonga vi- Corolla kwa wanawake. Ikafikia wakati wenye mamlaka nchi hii wakagundua wao wanachoweza kutoa ni ukuu wa wilaya!

Katika mambo ambayo nilimsifia sana Magufuli ni kuondoa wakuu wa wilaya wote walioteuliwa kwa misingi ya uchumba na ushemeji, wengine wakitokea UVCCM, na wengine walioteuliwa-teuliwa tu bila sababu za kueleweka. Hata hivyo bado wapo wakuu wa wilaya wengi, wateule wa Raisi Magufuli huyo huyo, kama huyu anaeamrisha Sumaye akamatwe kwa kufanya ziara ya miradi, ambao wanafanya nione ukuu wa wilaya si kitu naweza kukikubali asilani!
 
Back
Top Bottom