Kama Raisi Magufuli na CCM hawataki mfumo wa vyama vingi nchini waseme wazi badala ya kufanya hujuma

Mimi hata mukiokoa MAKINIKIA,ulete BOMBADIER umkamate Sethi na Ruge halafu uninyime UHURU WA KUJIELEZA,yote uliyofanya ni UBATILI MTUPU.Nipe uhuru wa kujieleza kwani ni haki yaki yangu ya msingi kama binadamu na iko kwenye sheria pia.
Umekatazwa wapi kujieleza mbona hapa unajieleza? Au unataka uruhusiwe kufunga SPK ikulu ujieleze?
 
Mbegu wanayoipanda karibu inaota wasifikiri kwamba Tanzania ipo mbinguni tunaomba mungu apishie mbali.Lakini hawatakwepa lawama.Labda wanatengeneza uraisi wa maisha.
Urais wa maisha atatoa nani kama sio wananchi? Je wananchi wamekubali kufanya hivyo?
 
Mtukufu anazuia watu wote isipokuwa wa yeye na wanachama wake kujieleza popote pale
Yeye anapita kila mahali na kutumia kila tukio (hata kumuapisha dc) kufanya kampeni miaka dahari kabla ya uchaguzi na kampeni kufunguliwa.Anamtuma 'mtu' wake Bulembo nchi nzima kufanya kampeni ikiwami maigizo ya kupokea kadi feki za vyama pinzani
Hataki vyama pinzani na viongozi wake wafanye lolote la kisiasa
Kama huu si udikteta ni nini ?
Hata iweje haiwezekeni kufanana na chama tawala au rais wake kwa asilimia 100
 
Kama unaamini kuna dalili zote za ccm kukataa Mfumo wa vyama vingi kwanini unangoja kutangaziwa?
Kama huo ndio mtindo wa kisasa basi hata huko Kibiti tusikalamike kutoambiwa sababu za kwa nini wanaua. Huo unakuwa ni ugaidi unaofanana basi. Mwaga mboga nimwage ugali.

Isitoshe, kuanza vyama vingi tulitangaziwa sivyo?
 
Na ukandamizaji unaoendelea unazidisha chuki sana.
Na italeta kitu tu huko mbele ya safari
 
Kosa la kutojua taratibu sio jinai ya kushikwa na polisi bali kuelemishwa taratibu zinasema nini. Vinginevyo pale bungeni taratibu zinakosewa kila leo ingikuwa sero zinajaa kila kipindi kama hiki cha bunge ila wanakumbushana taratibu na kanuni zinasemaje na kuendelea sio kumfungia sero!
Aelimishwe mara ngapi huku wana midomo michafu wakijidai wanapigania Uhuru? 48 hrs inawahusu hakuna namna mpk wanyooke.
 
Tunataka mapadri na mashehe watoe tamko kwa hili. Ni ujinga kama hilo la kuharibu bustani ya mtu na kumchafua kiongozi wa upinzani makusudi kama ni mwuza dawa wakati wanajua wazi ni uwongo mtupu. Very soon mambo yataenda mrama kwa upuuzi huu. Mimi mkuu wa wilaya hawezi kuniweka ndani sembuse Sumaye. Hivi Rais anapata raha gani kuona na kusikia haya? Fisiem nao wanaonaje na kupata usingizi usiku? Hovyo sana na ni ushamba kabisa kuanzia juu mpaka chini!
Hiyo ndio gharama za ukombozi nyie si mnataka kumtoa mkoloni mweusi lkn mnaogopa kukaa ndani?
 
Labda tusaidie tusio jua sheria; kuna kosa lolote la diwani/meya wa eneo husika kufanya ziara ya kukagua miradi ya maendelea kwenye eneo lake la utawala!?
Kwanini hakuwasiliana na mkuu wake ambaye ni mkurugenzi? Halafu sumaye alifuata nini?
 
Mkuu, madaraka ambayo unaweza kupewa kwa kujua tu kusoma na kuandika, au kujua tu jinsi ya kuimba ngonjera na kusifia chama chako cha siasa na kutoa vijembe kwa vyama vya upinzani, au kama wakati fulani Generali Ulimwengu alivyosema, kwa kuwa tu wewe ni mchumba au shemeji wa mkuu fulani, mimi hayo naona no uongozi wa ngazi ya chini. La sivyo nafasi hizi sisingetolewa kama sandakarawe amina, mwenye kupata apate, mwenye kukosa akose.

Mimi leo hii Raisi Magufuli akiniteua kuwa Mkuu wa Wilaya nitakataa. Ukuu wa wilaya umedhalilishwa sana kwa mtu mwenye usomi na hekima zake kuukubali. Hata ukuu wa mkoa, japo una nafuu kidogo, uko mkondo huo huo.
Unajua huwezi kupewa tulia sindano ikuingie.
 
Jamani mbona inajulikana wazi kwamba kiongozi anayo ruhusa ya kufanya madudu ila alimradi tu aimbe nyimbo za CCM. mbona Meya Masaburi alifanya madudu makubwa mno ya kuumiza nchi, lakini hakuna aliyemgusa. leo Mameya wa upinzani wanachapa kazi na kuleta tija, wanaandamwa. Lakini jibu liko wazi pia. NI WIVU TU. CCM HAWATAKI KABISA KUSIKIA UPINZANI WANALETA MABADILIKO YA KWELI KWA WANANCHI. NDIO MAANA SERIKALI YA CCM INAZIDI KUWEKA MIKAKATI YA KUZIPUNGUZIA MAPATA HALMASHAURI NA MANISPAA HASA ZA MAJIJI MAKUBWA AMBAZO NYINGI ZIPO CHINI YA UPINZANI. CCM WANAOGOPA WANANCHI WATAONA WAPINZANI NI BORA ZAIDI. NI WIVU TU TENA WA KIKE
Kwahiyo anamuiga masaburi?
 
Chuki na hujuma matokeo yake ndio hayo tunaona Kibiti. Sasa hawa wapiga raia na walemavu na wafunga wapinzani wameshindwa kudhibiti sehenu ndogo sana ya Kibiti - hii chuki ikiendelea ikazaa Kibiti nyingi zaidi watafanya nini?

Wanapasa kujiuliza sana. Kwa nini huko Kibiti ni watu wa CCM na Polisi tu wanauwawa? Soon or later kutakuwa na copy cats against serikali ya CCM, CCM wenyewe na polisi, sehemu nyingine zaidi ya Kibiti. It is just a matter of time wakiendelea hivi.

They must learn the hard way. Shauri yao. No sympathy there.
Kibiti itakomeshwa tu just wait n watch
 
What goes around comes around. Angalia kibiti. Soon nchi nzima itakuwa hivyo kwa ajili ya ccm kujenga chuki. Angalieni sana msilaaniwe kwa kuleta vita nchi hii.
 
At ze end of the dey bila hawa wapinzani tutaburuzwa kama mbwa nawaambia skuzote awapendwi ili ccm ipate nafasi yakuiba kwa Uhuru na magu anapambania hilo
 
Tunataka mapadri na mashehe watoe tamko kwa hili. Ni ujinga kama hilo la kuharibu bustani ya mtu na kumchafua kiongozi wa upinzani makusudi kama ni mwuza dawa wakati wanajua wazi ni uwongo mtupu. Very soon mambo yataenda mrama kwa upuuzi huu. Mimi mkuu wa wilaya hawezi kuniweka ndani sembuse Sumaye. Hivi Rais anapata raha gani kuona na kusikia haya? Fisiem nao wanaonaje na kupata usingizi usiku? Hovyo sana na ni ushamba kabisa kuanzia juu mpaka chini!

Mkuu usitegemee lolote toka kwa viongozi wa dini kuhusu huo uonevu wa wazi toka kwa ccm kwa mgongo wa urais. Hao viongozi wa dini utawaona siku wapinzani watakapoamua kuchora mstari wa uonevu ndio utawasikia wanaambiwa wakaonye kuhusu watu wanaotaka kuharibu amani ya nchi yetu.

Huyo Sumaye unayemtaja hapa ndio huyo wakati akiwa ccm na madarakani alikuwa anaona upinzani ni ushetani. Tetea unavyoweza lakini usimtumie Sumaye kama sehemu ya upinzani kuonewa kwani yeye ndio aliyepanda hii mbegu ya wapinzani kuonewa.

Kwa taarifa yako ccm wanapata raha sana kwani kabla ya cdm kubadilisha gia angani kwa tamaa za Mbowe, kwa kumchukua Lowassa na kumpa nafasi kubwa kabisa ya kugombea urais, ccm ilipata wakati mgumu sana dhidi ya wapinzani.

Kama sio tume isiyo huru ya uchaguzi na mizengwe ya siasa za kiafrika leo hii ccm ingekuwa kama KANU ya Kenya.

Kwa hiyo kwakuwa CCM imepita kwenye tundu la sindano na kupata rais asiye na uwezo wa siasa za ushindani wala hoja za ushawishi, namna pekee ni kuficha udhaifu huo kwa kuwanyanyasa wapinzani na hata ikibidi kuua kabisa kwani uwezo wa kushindana na upinzani kwa hoja haupo.

Jaribu kupata picha unamuweka Magufuli na Zitto kwenye mdahalo huru kama hutabaki kinywa wazi. Nakuunga mkono kwamba kwa sasa ccm inaendesha siasa za kishamba sana na wala kwa hilo hakuna ubishi.
 
Back
Top Bottom