Kama Raisi Magufuli na CCM hawataki mfumo wa vyama vingi nchini waseme wazi badala ya kufanya hujuma

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
8,520
2,000
Nasikia uchungu sana kwa nchi yangu Tanzania.

Imefikia mahali hata kama hujihusushi na mambo ya siasa, utaudhiwa na hujuma za wazi wazi zinazofanywa na serikali dhidi ya vyama vya upinzani nchini, nikiamini hujuma hizi zikiwa ni kwa shinikizo la CCM na hata kuchochewa na Raisi Magufuli mwenyewe.

Raisi Magufuli, kama alivyodai yeye mwenyewe, hawezi kukwepa kuwa raisi wa Watanzania wote, walio CCM, walio upinzani na hata wale wasio jihusisha na siasa. Kila mtu anajua kwamba kuna wakati Raisi Magufuli amefikia kutoa kauli zinaonyesha kwamba anaona mtu yeyote aliye kwenye chama cha upinzani kuwa adui.

Watanzania tunashuhudia kila siku hali ya "mpambano" ambao uko nje kabisa ya hali ya kawaida ya upinzani wa kisiasa, kati ya CCM na vyama vya upinzani. Kwa kuwa CCM ndio chama kilichoko madarakani, ni wazi kabisa mara nyingi "mpambano" huu huzaa hali ya kuonewa na kunyanyaswa kwa wale walio vyama vya upinzani. Hili hutokea ndani na nje ya Bunge, na hata katika nyanja za Majiji, Halmashauri na serikali za mitaa kwa ujumla. Na mbaya zaidi, vyombo vyetu vya usalama, pamoja na TISS na Polisi, wamekuwa wakiingizwa katika mpambano huu na kuharibu kabisa uhusiano wao na raia. Wakati fulani hata kumekuwa na jitihada za kujaribu kuwaingiza JWTZ.

Hali hii haipendezi kabisa kwa nchi yetu, na inatia aibu na kinyaa kuona watu wa uongozi wa juu hata ngazi ya raisi wakifanya kila wawezalo kuhujumu vyama vya upinzani.

Na tuseme wazi basi, kama Raisi Magufuli na CCM kwa ujumla wanaona kwamba kwa sasa hali ya vyama vingi vya siasa haifai kwa nchi yetu, basi waliweke hili wazi, ili tuamue na ikibidi kufanya referandum kuamua kuondoa mfumo wa vyama vingi na kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja au la.

Tupo wengi ambao ukweli ni kwamba tungependa kuona nguvu za viongozi shupavu na makini walioko CCM na vyama vya upinzani kama CHADEMA, CUF, ACT, NCCR nk zikiunganishwa ili kuendeleza nchi yetu. Sasa kama hili haliwezekani chini ya mfumo wa vyama vingi, basi ni bora tutafakari upya kama ni bora kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja na kuwa nguvu moja.
 
Masanyiwa Mabula

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
958
1,000
Kilicho nacho na mwanzo hakikosi kuwa na mwisho.
Ameshasahau uongozi ni dhamana. Akimuulize mwenzake wa Afrika magharibi anayekunywa kinywaji pendwa chenye jina la kiongozi wa Afrika mashariki yaan anamnywa raisi
 
Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
2,885
2,000
Tulikuwa hatujazoea kusikia Mstahiki MEYA anakamatwa, lakini tokea Wapinzani walipojipatia nafasi hizo, sasa tumeanza kushuhudia Mameya wakikamatwa hovyo, kudhalilishwa.

utashangaa wanaccm wanasisitiza heshima kwa "kiti" cha spika, "kiti" cha Rais, wanawataka wapinzani "waheshimu" nafasi hizo. hata Waziri wa Sheria, Kabudi, anapenda sasna kusisitiza hilo. na ni hoja nzuri tu. lakini kwanza hicho wanachoona kinakiukwa ni kule tu kuwakosoa.

hawataki kabisa viongozi wa CCM na serikali wakosolewe. lakini basi hata kama ni kuheshimu nafasi, mbona za wapinzani haziheshimiwi?
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
30,834
2,000
Tulikuwa hatujazoea kusikia Mstahiki MEYA anakamatwa, lakini tokea Wapinzani walipojipatia nafasi hizo, sasa tumeanza kushuhudia Mameya wakikamatwa hovyo, kudhalilishwa. utashangaa wanaccm wanasisitiza heshima kwa "kiti" cha spika, "kiti" cha Rais, wanawataka wapinzani "waheshimu" nafasi hizo. hata Waziri wa Sheria, Kabudi, anapenda sasna kusisitiza hilo. na ni hoja nzuri tu. lakini kwanza hicho wanachoona kinakiukwa ni kule tu kuwakosoa. hawataki kabisa viongozi wa CCM na serikali wakosolewe. lakini basi hata kama ni kuheshimu nafasi, mbona za wapinzani haziheshimiwi?
Mstahiko meya asiyejua taratibu na kuzifuata?
 
Kweli kabisa Mkuu. Na kinachokera hata zaidi ni kwamba wapo watu ndani ya CCM walipiga kura kuunga mkono kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa. Sasa waliunga mkono kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi ili kuja kuvihujumu vyama vya upinzani?

Kwa kuwa Tanzania iliridhia kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa, kiongozi mwenye hekima na busara ni yule atakaeulinda mfumo huo na hata kuuendeleza kwa manufaa ya Taifa, sio kutaka kudhoofisha na kuua upinzani nchini. Sasa Raisi Magufuli na watu wake wa CCM wapime wao wako wapi katika suala la vyama vingi vya siasa nchini; kama ni viongozi wenye hekima na busara au wenye kutenda kwa ubinafsi badala ya maslahi ya Tanzania. Imefika mahali lazima tuwaambie juu ya matendo yao yenye kutia aibu, sio dhidi ya CHADEMA au CUF, bali dhidi ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini kwa ujumla.

Magufuli hapaswi kusahau kuwa kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini ni suala la kikatiba, katiba aliyoapa kuilinda. Sitegemei alitamka yale maneno ya kiapo kama kasuku tu. Sasa katika mambo mengi tu, pamoja na hili la vyama vingi vya siasa, inatia shaka kama kiapo chake kilikuwa na maana yeyote kwa Watanzania.

Kama Raisi Magufuli na CCM wanaona mfumo huu haufai kwa hatua ya maendeleo nchi yetu ilipofikia, basi waseme wazi turekebishe, kwa ridhaa ya Watanzania wote, sio shinikizo la chama kimoja cha siasa kinachotaka kufanya mambo kwa ubinafsi na kuhodhi madaraka.
 
daud magigo

JF-Expert Member
Sep 5, 2014
981
500
Mimi hata mukiokoa MAKINIKIA,ulete BOMBADIER umkamate Sethi na Ruge halafu uninyime UHURU WA KUJIELEZA,yote uliyofanya ni UBATILI MTUPU.Nipe uhuru wa kujieleza kwani ni haki yaki yangu ya msingi kama binadamu na iko kwenye sheria pia.
 
Martin George

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,694
2,000
Nasikia uchungu sana kwa nchi yangu Tanzania.

Imefikia mahali hata kama hujihusushi na mambo ya siasa, utaudhiwa na hujuma za wazi wazi zinazofanywa na serikali dhidi ya vyama vya upinzani nchini, nikiamini hujuma hizi zikiwa ni kwa shinikizo la CCM na hata kuchochewa na Raisi Magufuli mwenyewe.

Raisi Magufuli, kama alivyodai yeye mwenyewe, hawezi kukwepa kuwa raisi wa Watanzania wote, walio CCM, walio upinzani na hata wale wasio jihusisha na siasa. Kila mtu anajua kwamba kuna wakati Raisi Magufuli amefikia kutoa kauli zinaonyesha kwamba anaona mtu yeyote aliye kwenye chama cha upinzani kuwa adui.

Watanzania tunashuhudia kila siku hali ya "mpambano" ambao uko nje kabisa ya hali ya kawaida ya upinzani wa kisiasa, kati ya CCM na vyama vya upinzani. Kwa kuwa CCM ndio chama kilichoko madarakani, ni wazi kabisa mara nyingi "mpambano" huu huzaa hali ya kuonewa na kunyanyaswa kwa wale walio vyama vya upinzani. Hili hutokea ndani na nje ya Bunge, na hata katika nyanja za Majiji, Halmashauri na serikali za mitaa kwa ujumla. Na mbaya zaidi, vyombo vyetu vya usalama, pamoja na TISS na Polisi, wamekuwa wakiingizwa katika mpambano huu na kuharibu kabisa uhusiano wao na raia. Wakati fulani hata kumekuwa na jitihada za kujaribu kuwaingiza JWTZ.

Hali hii haipendezi kabisa kwa nchi yetu, na inatia aibu na kinyaa kuona watu wa uongozi wa juu hata ngazi ya raisi wakifanya kila wawezalo kuhujumu vyama vya upinzani.

Na tuseme wazi basi, kama Raisi Magufuli na CCM kwa ujumla wanaona kwamba kwa sasa hali ya vyama vingi vya siasa haifai kwa nchi yetu, basi waliweke hili wazi, ili tuamue na ikibidi kufanya referandum kuamua kuondoa mfumo wa vyama vingi na kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja au la.

Tupo wengi ambao ukweli ni kwamba tungependa kuona nguvu za viongozi shupavu na makini walioko CCM na vyama vya upinzani kama CHADEMA, CUF, ACT, NCCR nk zikiunganishwa ili kuendeleza nchi yetu. Sasa kama hili haliwezekani chini ya mfumo wa vyama vingi, basi ni bora tutafakari upya kama ni bora kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja na kuwa nguvu moja.
Mkuu kaisome vizuri sheria ya vyama vya siasa utaelewa kuwa CCM ni chama kikuu cha siasa, na kwahiyo upinzani ni jina tu lakini hivi ni surpotive parties na hata ukiangalia itikadi zao hazitofautiani kabisa na CCM!
 
Menyainganyi

JF-Expert Member
Mar 12, 2013
1,172
2,000
Synthesizer,

Pole kwa maumivu unayopata . . Huu upumbavu huu unaofanywa na CCM kwa kushirikiana na DOLA . . , unaendelea kuzalisha chuki mbaya sana ktk Taifa hili . .

Ni kama nchi inatawaliwa na wakoloni hivi, watu wazima wanaswaga tuu kama ng'ombe . . , viongozi waliochaguliwa na watanzania wananyimwa haki yao ya Kikatiba ya kuongoza watu wao kwa uhuru . .

Tazama makatazo ya kufanya mikutano ya kisiasa yanavyowabana vyama vya upinzani tuu, lakini maandamano ya kumuunga mkono Mwenyekiti wa ccm RUHKSA . . Tazama wakuu wa Wilaya na Mikoa walivyo MIUNGU WATU . . , wao wanaweza kumtia ndani yeyote kwa amri hata ya kilevi tuu . . Tunakwenda wapi Watanzaniaaa . . ?!

Matendo haya ya ukiukwaji wa haki za utawala bora, haki za binadamu, ni DHARAU KUBWA sana inayoonyeshwa na CCM kwa wapiga kura wa Tanzania . .

Hii ni namna ya ccm kupeleka ujumbe kwa watanzania kuwa, MKITUCHAGUA au MSIPOTUCHAGUA bado tutawatawala kimabavu tunavyotaka . . , hakuna wa kutuwajibisha . .

Tujiulize watanzania, hawa wakuu wa Wilaya na Mikoa, Wakurugenzi wa Majiji , ni viongozi tuliowachagua sisi . . ???!
Kama sio, jee kwa nini wao ndio wenye NGUVU kuliko viongozi wetu (wabunge,madiwani, ma Meya) tuliowachagua sisi kwa KURA zetuuu . . ?!

Kwa nini Baraza la madiwani linazidiwa nguvu na MTU mmoja, Mkuu wa Wilaya/Mkoa, ambaye hakuchaguliwa na wananchi . . ??!
Kwa nini Mkuu wa Wilaya/Mkoa awe na mamlaka ya kuwatia ndani Wabunge wetu, madiwani wetu, ma Meya wetu hata bila sababu ya maana . . ??!

Hii inaudhi sana, ni UDHALILISHAJI wa wazi kabisa wa wananchi waliosimama juani masaa 8 na zaidi kuwachagua viongozi wawapendao . . !

Haya mambo hayakubaliki na wala hayavumiliki kwa MTU mzima yeyote mwenye akili yake timamu . . !
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
8,520
2,000
Mkuu kaisome vizuri sheria ya vyama vya siasa utaelewa kuwa CCM ni chama kikuu cha siasa, na kwahiyo upinzani ni jina tu lakini hivi ni surpotive parties na hata ukiangalia itikadi zao hazitofautiani kabisa na CCM!
Hapana Mkuu, sheria ya vyama vya siasa inatambua kuwepo chama tawala, lakini sio CCM kama chama kikuu cha siasa.
 
kahupwe

JF-Expert Member
Sep 9, 2016
290
250
Mbegu wanayoipanda karibu inaota wasifikiri kwamba Tanzania ipo mbinguni tunaomba mungu apishie mbali.Lakini hawatakwepa lawama.Labda wanatengeneza uraisi wa maisha.
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
8,520
2,000
Synthesizer,

Pole kwa maumivu unayopata . . Huu upumbavu huu unaofanywa na CCM kwa kushirikiana na DOLA . . , unaendelea kuzalisha chuki mbaya sana ktk Taifa hili . .

Ni kama nchi inatawaliwa na wakoloni hivi, watu wazima wanaswaga tuu kama ng'ombe . . , viongozi waliochaguliwa na watanzania wananyimwa haki yao ya Kikatiba ya kuongoza watu wao kwa uhuru . .

Tazama makatazo ya kufanya mikutano ya kisiasa yanavyowabana vyama vya upinzani tuu, lakini maandamano ya kumuunga mkono Mwenyekiti wa ccm RUHKSA . . Tazama wakuu wa Wilaya na Mikoa walivyo MIUNGU WATU . . , wao wanaweza kumtia ndani yeyote kwa amri hata ya kilevi tuu . . Tunakwenda wapi Watanzaniaaa . . ?!

Matendo haya ya ukiukwaji wa haki za utawala bora, haki za binadamu, ni DHARAU KUBWA sana inayoonyeshwa na CCM kwa wapiga kura wa Tanzania . .

Hii ni namna ya ccm kupeleka ujumbe kwa watanzania kuwa, MKITUCHAGUA au MSIPOTUCHAGUA bado tutawatawala kimabavu tunavyotaka . . , hakuna wa kutuwajibisha . .

Tujiulize watanzania, hawa wakuu wa Wilaya na Mikoa, Wakurugenzi wa Majiji , ni viongozi tuliowachagua sisi . . ???!
Kama sio, jee kwa nini wao ndio wenye NGUVU kuliko viongozi wetu (wabunge,madiwani, ma Meya) tuliowachagua sisi kwa KURA zetuuu . . ?!

Kwa nini Baraza la madiwani linazidiwa nguvu na MTU mmoja, Mkuu wa Wilaya/Mkoa, ambaye hakuchaguliwa na wananchi . . ??!
Kwa nini Mkuu wa Wilaya/Mkoa awe na mamlaka ya kuwatia ndani Wabunge wetu, madiwani wetu, ma Meya wetu hata bila sababu ya maana . . ??!

Hii inaudhi sana, ni UDHALILISHAJI wa wazi kabisa wa wananchi waliosimama juani masaa 8 na zaidi kuwachagua viongozi wawapendao . . !

Haya mambo hayakubaliki na wala hayavumiliki kwa MTU mzima yeyote mwenye akili yake timamu . . !
Mkuu umenielewa vema. Sasa mjumuisho wa yote uliyosema ndio ninachouliza hapa - je, tunahitaji kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa ikiwa uwepo wake unaleta hizo hali ambazo hazipendezi na hazina manufaa kwa umoja wetu wa kitaifa?

Nakumbuka kwamba suala la kuanzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa lilipopigiwa kura, ni 20% ndio walikubali, na 80% walikataa. Ilikuwa ni ushauri wa Nyerere kwamba tuingie mfumo wa vyama vingi japo wengi wamekataa.

Sasa ifikie mahali tukubal kwamba inawezekana kabisa tulilazimisha kuwa na mfumo wa vyama vingi wakati Watanzania wengi hawautaki. Ndio maana nikasema huenda ni vema kufanya referandum nyingine, na safari hii tuheshimu matakwa ya walio wengi.

Na kama itadhihirika kwamba wengi hawautaki basi tuufute. Ila ikiwa wengi watautaka basi tutakuwa na sababu nzuri za kuwakemea watu kama Raisi Magufuli na wengi katika CCM kwamba lazima waheshimu mfumo ambao umekubalika na watu wengi kitaifa.
 
Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
9,621
2,000
Sijasoma content ya thread yako mbali na heading. Kama kweli ni hujuma jambo hilo ni kuvunja katiba ya tanzania ya mwaka 1977 toleo la 14 ambalo linasisitiza na kuweka bayana suala la demokrasia ya vyama vingi.

Kuna baadhi ya wabunge pia wana dhana potufu kuwa demokrasia ya vyama vingi ni mwanya wa ukoloni mamboleo.
 
kivava

JF-Expert Member
Apr 2, 2013
5,787
2,000
Mtukufu anazuia watu wote isipokuwa wa yeye na wanachama wake kujieleza popote pale
Yeye anapita kila mahali na kutumia kila tukio (hata kumuapisha dc) kufanya kampeni miaka dahari kabla ya uchaguzi na kampeni kufunguliwa.Anamtuma 'mtu' wake Bulembo nchi nzima kufanya kampeni ikiwami maigizo ya kupokea kadi feki za vyama pinzani
Hataki vyama pinzani na viongozi wake wafanye lolote la kisiasa
Kama huu si udikteta ni nini ?
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
8,520
2,000
Mbegu wanayoipanda karibu inaota wasifikiri kwamba Tanzania ipo mbinguni tunaomba mungu apishie mbali.Lakini hawatakwepa lawama.Labda wanatengeneza uraisi wa maisha.
Mbegu wanayopanda ni kuwatia hasira sehemu ya wananchi wa Tanzania siku hadi siku. Suala ni kwamba hii hasira inaweza kufikia critical mass wakati fulani hata tukaanza kushuhudia matukio ya kulipiza kisasi kama kuuwawa kwa viongozi wa CCM, hujuma za kigaidi dhidi ya CCM na hata kuuwawa kwa Polisi? CCM wasidhani hili haliwezekani hapa Tanzania. Mtu mwenye hasira anaweza kufanya lolote.

Mfano ni hili suala la ziara za Meya kwa Kindondoni na Sumaye sijui, kukagua miradi, kwenye eneo ambalo CHADEMA wanaliongoza. Je, kweli lilihitaji kuweka viongozi hawa wa ngazi ya juu ndani ili kurekebishana? Ni wazi hapa nia ya CHADEMA ilikuwa nzuri, lakini kama kulikuwa na makosa, kweli yalistahili watu kuwekwa ndani na kina Sumaye kutangaziwa wakamatwe na Polisi popote walipo kama vile ni wahalifu? Mara ngapi CCM wamefanya mambo kwa nia nzuri lakini kwa kukiuka utaratibu na wala hatuoni kama ni jambo kubwa la kuwaweka ndani?

Mara ngapi hata Raisi Magufuli amefanya jambo kwa nia njema lakini akakiuka utaratibu na hata kuvunja katiba lakini watu tukaona ni jambo la kurekebishana tu?

Sasa hizi taratibu na kuwekwa ndani, ni kwa ajili ya viongozi wa vyama vya upinzani tu? Kwa nini tunashindwa kuvumiliana kwa mambo madogo madogo kama haya?

Na kama huyu mkuu wa wilaya alikuwa na nia nzuri kwa nini asiwakumbushe mapema badala ya kutafuta nafasi za kuvizia ili kuwadhalilisha viongozi wa upinzani na kuwaweka ndani kwa sababu ndogo za kutofuata utaratibu uliopo, mambo ambayo kila kukicha CCM pia wanakosea?

Na ujasiri huu wa watu wadogo kama wakuu wa wilaya kutangaza kumtia ndani Waziri Mkuu mstaafu Sumaye wanaupata wapi kama sio toka kwa Raisi Magufuli? Niambie Mkuu wa wilaya gani atakuwa na ujasiri wa kutoa amri waziri mkuu mstaafu Pinda ambaye bado yuko CCM atiwe ndani kwa "kukiuka utaratibu". Ndio maana nikasema hata huyu Raisi Magufuli katika haya mambo ya kuleta chuki nchini na kuhujumu upinzani ni mhusika mkuu.
 
mwita_zakayo

Member
Jun 17, 2017
18
45
Si kweli kwamba viongozi WA upinzani hawatendewi haki suala ni kwamba haimanishi kwamba kuwa mpinzani usifate utaratibu hapana serikali haiwezi kusita kumchukulia mtu hatua kwamba yeye ni mpinzani kama amekosea sheria lazima ichukue mkondo wake lakini pia nashangaa kwa yule anayesema Mheshimiwa Rais hataki vyama vya upinzani .

suala ni kwamba wapinzani hamuna common agenda maana yote mliokuwa mnayapigia kelele yametekelezwa sasa mnatapatapa kwanza kwa mpinzani mwenye akili timamu sasa ndo mda mwafaka WA kumpongeza Mheshimiwa Rais maana ni mtu anayeleta maendeleo bila kujali itikadi za vyama hiyo haitoshi Anafanya uteuzi anateua ambao sio wanaccm.

wapinzani mnataka awafanyie nini kama mmeishiwa hoja fungal vyama vyenu wenyewe msisingizie mtu yeyote na mambo yataenda kama kawaida kwanza MNA destructive politics mnachelewesha maendeleo na hakuna kilichaharibika mbona kipindi cha mfumo WA chama kimoja CCM iliongoza na mambo yalienda CCM Oyeeeeeee Magufuli JUU HAPA KAZI TU
 
PMM

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
778
250
Mstahiko meya asiyejua taratibu na kuzifuata?
Kosa la kutojua taratibu sio jinai ya kushikwa na polisi bali kuelemishwa taratibu zinasema nini. Vinginevyo pale bungeni taratibu zinakosewa kila leo ingikuwa sero zinajaa kila kipindi kama hiki cha bunge ila wanakumbushana taratibu na kanuni zinasemaje na kuendelea sio kumfungia sero!
 
areafiftyone

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
7,387
2,000
Nasikia uchungu sana kwa nchi yangu Tanzania.

Imefikia mahali hata kama hujihusushi na mambo ya siasa, utaudhiwa na hujuma za wazi wazi zinazofanywa na serikali dhidi ya vyama vya upinzani nchini, nikiamini hujuma hizi zikiwa ni kwa shinikizo la CCM na hata kuchochewa na Raisi Magufuli mwenyewe.

Raisi Magufuli, kama alivyodai yeye mwenyewe, hawezi kukwepa kuwa raisi wa Watanzania wote, walio CCM, walio upinzani na hata wale wasio jihusisha na siasa. Kila mtu anajua kwamba kuna wakati Raisi Magufuli amefikia kutoa kauli zinaonyesha kwamba anaona mtu yeyote aliye kwenye chama cha upinzani kuwa adui.

Watanzania tunashuhudia kila siku hali ya "mpambano" ambao uko nje kabisa ya hali ya kawaida ya upinzani wa kisiasa, kati ya CCM na vyama vya upinzani. Kwa kuwa CCM ndio chama kilichoko madarakani, ni wazi kabisa mara nyingi "mpambano" huu huzaa hali ya kuonewa na kunyanyaswa kwa wale walio vyama vya upinzani. Hili hutokea ndani na nje ya Bunge, na hata katika nyanja za Majiji, Halmashauri na serikali za mitaa kwa ujumla. Na mbaya zaidi, vyombo vyetu vya usalama, pamoja na TISS na Polisi, wamekuwa wakiingizwa katika mpambano huu na kuharibu kabisa uhusiano wao na raia. Wakati fulani hata kumekuwa na jitihada za kujaribu kuwaingiza JWTZ.

Hali hii haipendezi kabisa kwa nchi yetu, na inatia aibu na kinyaa kuona watu wa uongozi wa juu hata ngazi ya raisi wakifanya kila wawezalo kuhujumu vyama vya upinzani.

Na tuseme wazi basi, kama Raisi Magufuli na CCM kwa ujumla wanaona kwamba kwa sasa hali ya vyama vingi vya siasa haifai kwa nchi yetu, basi waliweke hili wazi, ili tuamue na ikibidi kufanya referandum kuamua kuondoa mfumo wa vyama vingi na kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja au la.

Tupo wengi ambao ukweli ni kwamba tungependa kuona nguvu za viongozi shupavu na makini walioko CCM na vyama vya upinzani kama CHADEMA, CUF, ACT, NCCR nk zikiunganishwa ili kuendeleza nchi yetu. Sasa kama hili haliwezekani chini ya mfumo wa vyama vingi, basi ni bora tutafakari upya kama ni bora kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja na kuwa nguvu moja.
Mimi ni mwana CCM ninayejitambua na ninayeitakia mema nchi yangu.I understand your concern brother na nadhani viongozi wetu wajuu chamani watalielewa hili na kulifanyia kazi. Kwa bahati nzuri Rais wetu analielewa hili vizuri sana.Wenye shida mimi naona ni hawa viongozi wetu wana Chama wa ngazi za chini.Ila point taken brother. Hii confrontational behavior haitatusaidia sana kwenye maendeleo yetu,ni lazima ikomeshwe.
 
majeshi 1981

JF-Expert Member
Dec 7, 2013
2,093
1,500
Mimi ni mwana CCM ninayejitambua na ninayeitakia mema nchi yangu.I understand your concern brother na nadhani viongozi wetu wajuu chamani watalielewa hili na kulifanyia kazi. Kwa bahati nzuri Rais wetu analielewa hili vizuri sana.Wenye shida mimi naona ni hawa viongozi wetu wana Chama wa ngazi za chini.Ila point taken brother. Hii confrontational behavior haitatusaidia sana kwenye maendeleo yetu,ni lazima ikomeshwe.
Sidhani kama upo sahihi kumweka mkuu wa wilaya katika ngazi ya viogozi wa ngazi za chini
 
Bashite og

Senior Member
Mar 15, 2017
176
225
mta
Synthesizer,

Pole kwa maumivu unayopata . . Huu upumbavu huu unaofanywa na CCM kwa kushirikiana na DOLA . . , unaendelea kuzalisha chuki mbaya sana ktk Taifa hili . .

Ni kama nchi inatawaliwa na wakoloni hivi, watu wazima wanaswaga tuu kama ng'ombe . . , viongozi waliochaguliwa na watanzania wananyimwa haki yao ya Kikatiba ya kuongoza watu wao kwa uhuru . .

Tazama makatazo ya kufanya mikutano ya kisiasa yanavyowabana vyama vya upinzani tuu, lakini maandamano ya kumuunga mkono Mwenyekiti wa ccm RUHKSA . . Tazama wakuu wa Wilaya na Mikoa walivyo MIUNGU WATU . . , wao wanaweza kumtia ndani yeyote kwa amri hata ya kilevi tuu . . Tunakwenda wapi Watanzaniaaa . . ?!

Matendo haya ya ukiukwaji wa haki za utawala bora, haki za binadamu, ni DHARAU KUBWA sana inayoonyeshwa na CCM kwa wapiga kura wa Tanzania . .

Hii ni namna ya ccm kupeleka ujumbe kwa watanzania kuwa, MKITUCHAGUA au MSIPOTUCHAGUA bado tutawatawala kimabavu tunavyotaka . . , hakuna wa kutuwajibisha . .

Tujiulize watanzania, hawa wakuu wa Wilaya na Mikoa, Wakurugenzi wa Majiji , ni viongozi tuliowachagua sisi . . ???!
Kama sio, jee kwa nini wao ndio wenye NGUVU kuliko viongozi wetu (wabunge,madiwani, ma Meya) tuliowachagua sisi kwa KURA zetuuu . . ?!

Kwa nini Baraza la madiwani linazidiwa nguvu na MTU mmoja, Mkuu wa Wilaya/Mkoa, ambaye hakuchaguliwa na wananchi . . ??!
Kwa nini Mkuu wa Wilaya/Mkoa awe na mamlaka ya kuwatia ndani Wabunge wetu, madiwani wetu, ma Meya wetu hata bila sababu ya maana . . ??!

Hii inaudhi sana, ni UDHALILISHAJI wa wazi kabisa wa wananchi waliosimama juani masaa 8 na zaidi kuwachagua viongozi wawapendao . . !

Haya mambo hayakubaliki na wala hayavumiliki kwa MTU mzima yeyote mwenye akili yake timamu . . !
mtajijua ccm mbele kwa mbele
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom