figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,484
His Excellency Joko Widodo
Rais wa Indonesia Joko Widodo au Jokowi kama wengi wanavomuita, Baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Indonesia Mwaka 2014, katika hotuba yake ya kwanza aliwashukuru wale wote waliomfanyia kampeni hasa wanachama wa facebook, na kwa kutambua mchango wao, na kuwaomba waendelee kumshauri na kumuunga mkono. Vilevile aliwapa nafasi ya kumchagulia majina 34 ya Mawaziri kwa kupitia mtandao wa facebook. Yaani wapige kura za kimtandao wapate majina 34 ya Mawaziri ambayo wanapendekeza wawe katika Serikali yake.
Katika kampeni za Mwaka jana, Watu wengi wameshiriki Kampeni kwenye Mitandao ya kijamii hasa hapa JamiiForums, amabzo zimemuwezesha rais Pombe Magufuli kushinda Urais. Haikuishia hapo, Waanaendelea kumuunga mkono na kumshauri na kumpa ushirikiano wa kila namna. Ikiwemo kufichua majipu katika pembe zote za nchi na nje ya Nchi.
Ni nafasi kwa rais Magufuli kushukuru kwa kuungwa mkono mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na;
1. Kuhakikisha Vifurushi vya internet vinapungua bei. Hii ya MB 8 kwa mia tano ni kutufunga midomo sisi tunaotumia Mitandao, tushindwe kufichua maovu na kujua yanayoendelea hapa Nchini.
2. Aifanye Serikali yake kuwa karibu na rafiki wa Wananchi kwa kupitia mitandao ya kijamii hasa JamiiForums. Tayari anao Mawaziri ambao ni Wanachama wa JamiiForums, Mhe. Mwigulu Nchemba, Mhe. Nape Nnauye na Mhe. Dr. HKigwangalla. Hivyo anaweza kuwatumia wao kama demo kujibu maswali ya wananchi kupitia Mtandao ya JamiiForums.
Wizara zianzishe Accounts JamiiForums ili kuwafikia wananchi wa chini kabisa, ambapo watakua wanajibu maswali moja kwa moja kama anavyofanya Rais wa TFF Jamal malinzi. Hii itapunguza usumbufu wa Mtu kutoka Kigoma, Mtwara au Katavi kuja kuomba ufafanuzi Dar es Salaam. Na Serikali itapunguza matumizi na kurahisisha kazi.
3. Sheria ya Cybercrime na Sheria ya Takwimu zipitiwe upya na kurekebisha vifungu zisivyomsaidia mwananchi wa kawaida ili kumpa uhuru wa kutoa mawazo aliyonayo.
Wananchi wanatakiwa wawe na furaha katika nchi yao sio kuishi kama watumwa.
4.Nchi yetu bado ina safari ndefu, Hivyo wazawa kama hawa waanzirishi wa JamiiForums ndio inabidi wapewe kpaumbele. Ni maajabu eti unakuta Wizara ya Serikali au chombo cha inatumia Facebook pekee tena chombo cha nje wakati JamiiForums ipo kisa tu JamiiForums inafichua madudu yao. Uzalendo upo wapi? tuanzie hapa kuhiza kupenda vya nyumbani. JamiiForums itumike kama kioo cha Kujiangalia kama kweli Wananchi wanafurahia Utawala na wapi parekebishwe.
Hizi na zama za ukweli na Uwazi, Hatuwezi kuishi kama mwaka 47, sasa mambo yamebadilika na dunia ni kijiji. Tumeachwa sana na wenzetu, hivyo wakati wao wanatembea, sisi tukimbie ili tuweze kuwafikia.
Nawatakia kila la heri