MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,975
Nilishangaa kidogo kusoma Press Release ya Ikulu ambayo ilitangaza majina ya Wakuu wa Mikoa ''wapya'' ambao WAMETEULIWA na Rais Samia. Kilichonishangaza ni lugha iliyotumika lakini ''kiuhalisia'' kilichofanyika ni UHAMISHO TU wa Wakuu wa Mikoa na kuziba nafasi za wale wamestaafu.
Rais Samia alichofanya ni kuhamisha hao Wakuu wa Mikoa kitu ambacho ni kizuri kiutendaji lakini pia ni kibaya kwa matumizi ya fedha na muda. Hawa Wakuu wa Mikoa itabidi walipwe pesa za Uhamisho lakini pia itawachukua muda kuyazoea mazingira kikazi ya sehemu waliyohamishwa.
Sasa kama ameweza kufanya hivi kwa Wakuu wote wa Mikoa, Kwa nini hakufanya hivyo kwa Waziri Mkuu na Mawaziri ili ionekane hii ni serikali yake ya Awamu ya Sita na sio Serikali ya Awamu ya tano yenye Rais wa Sita!
Rais Samia alitakiwa apendekeze Jina la Waziri Mkuu hata kama ni yule yule (Majaliwa) na likapigiwe kura bungeni kama Katiba inavyosema, halafu baadaye aunde baraza lake la Mawaziri hata kama ni wale wale halafu awaapishe kama atakavyofanya kwa Wakuu wa Mikoa.
Kwa sasa kila mara serikali inapofanya makosa, lawama wanatupiwa mawaziri ambao wanadaiwa niwa ''Rais Magufuli'' na wanafanya kazi kwa kutumia ''mentality'' ya Rais Magufuli kwa sababu hawakuteuliwa na Rais Samia. Kama angefanya kama alivyofanya kwa Wakuu wa Mikoa, hizi lawama zisingeendelea kuwepo!
Je, Rais Samia aliogopa nini kufanya kama alivyofanya kwa Wakuu wa Mikoa ''wapya''?