Kama Rais Samia amekiri vyama vya upinzani vina Katiba, kwanini Mutungi anawataka Chadema walete muhtasari wa kikao kilichowafukuza kina Mdee?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Nimeyasikikiza kwa makini Sana mahojiano maalum, aliyoyafanya mtangazaji mahiri, Salim Kikeke, wa shirika la habari la kimataifa la BBC, akimuhoji Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuhusu masuala mbalimbali yanayolihusu Taifa letu.

Mimi ningependa kuelezea kile alichokisema Rais wetu kuhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.

Katika mahojiano hayo Rais alifafanua kuwa vyama vya siasa vya upinzani nchini vina Katiba zao na haviingiliwi Katika maamuzi yao wanayoyafanya kwenye vikao vyao.

Sasa nimuulize Rais Samia, je yeye hajasikia kuhusu sakata la wale wabunge wa viti maalum 19 wa Chadema, wakiongozwa na Halima Mdee, ambalo Spika wa Bunge letu, Job Ndugai amegoma kufuata maamuzi ya vikao vya Chadema, vilivyowafuta uanachama wao hao wabunge wa Chadema?

Namwomba Rais Samia pia alitolee ufafanuzi hili suala la Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kuwataka Chadema wampelekee muhtasari wa kikao chao cha Kamati Kuu, kilichowafuta uanachama wao hao akina Mdee.

Hivi ni haki kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai kuendelea kuwakumbatia wabunge hao, ambao chama chao cha Chadema kilitangaza kuwavua uanachama wao?

Je, ni halali kwa Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi kuwataka Chadema wapeleke muhtasari wa kikao chao cha Kamati Kuu, kilichawavua uanachama wao, hao akina Halima Mdee?

Je, ni kwanini Spika Ndugai na mwenzie Msajili wa vyama, wanakuwa na "double standards" Katika maamuzi ya wabunge?

Kwanini CCM ilipomvua uanachama wake Sofia Simba, hatukuona Spika Ndugai, awagomee hao CCM kutokana na maamuzi yao na alitekeleza mara moja na kumvua ubunge wake?

Mbona hatukuona Msajili wa vyama amwombe muhtasari, Profesa Lipumba wa CUF, wakati akiwavua uanachama wao wale wabunge wa viti maalum?

Imenenwa Katika kitabu cha Mithali, 14:34 kuwa Haki huliinua Taifa na dhambi ni aibu ya watu wote.
 
AMEN
 
Back
Top Bottom