Kama Rais ndio anatoa vibali kutibiwa nje ya nchi, ndani ya miezi 6 zimetumika bil 17.1 - wametibiwa kina nani?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
CAG anatuambia kwamba gharama za matibabu ya nje ya nchi katika kipindi cha MIEZI SITA TU (30th june 2017 –Desemba 2017 ) zimeongezeka kutoka shilingi (Bilioni 28.6 mpaka shilingi Bilioni 45.7) Ndugu Rais ulisema kuwa katika kipindi cha UTAWALA wako matibabu nje ya nchi yatamalizwa kabisa/yatapunguzwa. Hata Mhe. Lissu mmegoma kumlipia MATIBABU mpaka SASA! CAG anatuonyesha kwamba umevunja rekodi kwa MATUMIZI!!

Sote tunajua hakuna anayetoka nje ya nchi ,kwa pesa ya serikali bila KIBALI CHA IKULU..’ndio maana tulimdharau na kumpuuza waziri wako aliposema…eti wanafanya ‘uhakiki’ kwa sababu wanahisi kuna watu walidanganya wanaenda kutibiwa moyo,lakini anakwenda kupandikizwa mimba sababu ya uzazi”

Je, kuna watu wanakwenda nje kutibiwa kimyakimya bila taarifa zao kuwekwa wazi? Kama wakati wa Kikwete Sh. Bilioni 2 kwa miezi 6 zilionekana nyingi, kwanini mwaka jana imetumika Bilioni 17.1 na serikali ya Magufuli ipo kimya?

Kama Bunge letu lingekuwa limeifanyia kazi ripoti ya CAG kwa kuibana Serikali ieleze ni kwanini gharama za matibabu nje ya nchi zimeongezeka maradufu, wakati idadi ya wanaoenda kutibiwa nje imepungua? Ni akina nani hao wanaotibiwa kimyakimya kwa mabilioni ya kodi zetu?

Haiwezekani Sh. Bilioni 2 kwa miezi 6 wakati wa Kikwete ionekane yalikuwa matumizi mabaya ya pesa, halafu Sh. Bilioni 17.1 kwa miezi 6 kipindi cha Magufuli ionekane ni kawaida tu!

Soma pia

Kibali kimetolewa cha mtoto kwenda nje kupandikiziwa mimba ya mjukuu wa taifa. Sasa kwa mujibu wa mbunge msukuma mayai yalifanana ikabidi wanunue yai la hisp kumpandikizia mmoja kati ya wawili hao. Sasa hilo yai la kununua halitaleta mjukuu wa kichina/ghana/rwanda au kwingineko?
Tusisahau pesa ya walipakodi ishaidhinishwa na ishatumika tayari.
 
Yaani ukishangaa ya firauni walahi utaona ya Musa,nami nimejiuliza kina nani wanaotibiwa nje wakati alikataza, ama yule mtoto wake aloenda kupandikiziwa mimba na huyu spika wetu ndo wamemaliza mabilioni yetu???Arghhh nchi inatia hasira hii haki ya nani
 
CAG anatuambia kwamba gharama za matibabu ya nje ya nchi katika kipindi cha MIEZI SITA TU (30th june 2017 –Desemba 2017 ) zimeongezeka kutoka shilingi (Bilioni 28.6 mpaka shilingi Bilioni 45.7) Ndugu Rais ulisema kuwa katika kipindi cha UTAWALA wako matibabu nje ya nchi yatamalizwa kabisa/yatapunguzwa. Hata Mhe.Lissummegoma kumlipia MATIBABU mpaka SASA! CAG anatuonyesha kwamba umevunja rekodi kwa MATUMIZI!!

Sote tunajua hakuna anayetoka nje ya nchi ,kwa pesa ya serikali bila KIBALI CHA IKULU..’ndio maana tulimdharau na kumpuuza waziri wako aliposema…eti wanafanya ‘uhakiki’ kwa sababu wanahisi kuna watu walidanganya wanaenda kutibiwa moyo,lakini anakwenda kupandikizwa mimba sababu ya uzazi”

Mbatia, Lowasa, Sumaye, Zito Kabwe, Spika wetu, Msigwa, ...
 
kuna ukweli kwamba kuna walioenda kupandikiza mimba japo walisema wanaenda kupima malaria
 
Temeni mate chini, msikejeli kuumwa kwa wenzenu mnakosea. Siku ukipatwa na shida wakat mfukon iko buku 5 kule Daktar anakwambia Mgonjwa anatakiwa aende Apollo gharama mil 43 ndio utajua kwanin gharama zimefika hizo. Tuache ujuaji ktk kila kitu mwisho wa siku tunaumia wanyonge.
 
CAG anatuambia kwamba gharama za matibabu ya nje ya nchi katika kipindi cha MIEZI SITA TU (30th june 2017 –Desemba 2017 ) zimeongezeka kutoka shilingi (Bilioni 28.6 mpaka shilingi Bilioni 45.7) Ndugu Rais ulisema kuwa katika kipindi cha UTAWALA wako matibabu nje ya nchi yatamalizwa kabisa/yatapunguzwa. Hata Mhe.Lissummegoma kumlipia MATIBABU mpaka SASA! CAG anatuonyesha kwamba umevunja rekodi kwa MATUMIZI!!

Sote tunajua hakuna anayetoka nje ya nchi ,kwa pesa ya serikali bila KIBALI CHA IKULU..’ndio maana tulimdharau na kumpuuza waziri wako aliposema…eti wanafanya ‘uhakiki’ kwa sababu wanahisi kuna watu walidanganya wanaenda kutibiwa moyo,lakini anakwenda kupandikizwa mimba sababu ya uzazi”
Jaribuni wanachadema kuwa na kuali za staha.Ndiyo maana wengi mtapatwa na majanga kwa kauli zenu ambazo zimekosa uungwana
 
Temeni mate chini, msikejeli kuumwa kwa wenzenu mnakosea. Siku ukipatwa na shida wakat mfukon iko buku 5 kule Daktar anakwambia Mgonjwa anatakiwa aende Apollo gharama mil 43 ndio utajua kwanin gharama zimefika hizo. Tuache ujuaji ktk kila kitu mwisho wa siku tunaumia wanyonge.
Hujaelewa hoja iliyopo mezani.
Soma tena ukiwa na sober mind.
Kama safari za kwenda kutibiwa nje zimedhibitiwa na kupungua, iweje matumizi yawe makubwa kuliko ilivyokuwa kipindi watu wanaenda kutibiwa nje kiholelaholela?
 
Back
Top Bottom