Kama Rais Kikwete ameheshimu Msiba wa Kanumba na Kuahirisha Safari kwa nini Kova alaumiwe kwa Saluti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama Rais Kikwete ameheshimu Msiba wa Kanumba na Kuahirisha Safari kwa nini Kova alaumiwe kwa Saluti

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Emil Mwangwa, Apr 27, 2012.

 1. Emil Mwangwa

  Emil Mwangwa Senior Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Serikali yote ya Kikwete iliacha shughuli na kukimbilia kenye msiba wa Kanumba kwa nini Kova alaumiwe kwa saluti????
  Waliohudhuria
  1. Raei Kikwete
  2.waziri Mkuu Pinda
  3.Makamu wa Rais Bilali
  4.Samweli Sita
  5.Membe kasema Kanumba ni sawa na balozi kaiwakilisha nchi kimataifa
  6.Mama Kikwete
  7.Ridhiwani Kikwete
  ....


  Ila cha kushangaza hapa familia yote ya Kikwete ilikuwepo lakini baba Mzazi wa Kanumba aligoma????
   

  Attached Files:

 2. Primitive

  Primitive JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  :mad2::mad2:confusing thread!
   
 3. 124 Ali

  124 Ali JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 5,705
  Likes Received: 2,388
  Trophy Points: 280
  Keli hapa ni jukwaa la hoja mchanganyiko lakini nahisi hoja yako wewe ni mvurugiko halisi wa fikra na ufahamu sijui nini huwa kinawasukuma kuanzisha thread zaaina hii na mkianzisha and take a step back what do you see in your own perceptive?
   
 4. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Du! Kwaheri! naona umekurupuka usingizini, la sivyo umekunywa viroba
   
 5. Tugutuke

  Tugutuke JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Mara Salute kwa Kova,mara Msiba wa Kanumba! Hueleweki ka sehemu za siri za kike. Unamaanisha nini?? Stupid man
   
 6. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmmh jombaa hujajipanga"; hebu kakojoe ulale ukiamka labda kichwa kitakua kimetulia uje umejipanga"
   
 7. t

  tata mugaka Member

  #7
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 47
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  mm navyofahamu kova hana makosa maiti yoyote inaheshima ya kipekee na inapigiwa salute nimeona sana huku kwetu tarime na nimeulizia kwa wastaafu askari
   
 8. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  weekend imeanza kunoga. tatizo ukikaa na mlevi nawe unalewa. mimi tayari. napita tu.
   
 9. M

  Michael Mwakyusa JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 307
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nijuavyo mimi mwili wa marehemu hupigiwa salute na askari hivyo sio ajabu alichofanya kamanda kova.
   
 10. Emil Mwangwa

  Emil Mwangwa Senior Member

  #10
  Apr 28, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  [h=2]Ridhiwani Kikwete anatajwa kumununukia gari Lulu[/h]
  Mbona sijamuona wakimtaja huyu jamaa?
  [​IMG]


  • [​IMG]

  [​IMG]
   
 11. Emil Mwangwa

  Emil Mwangwa Senior Member

  #11
  Apr 28, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  [h=2]Ridhiwani Kikwete anatajwa kumununukia gari Lulu[/h]
  Kanumba naye angekuwa hai tungemsuta kama ni Lulu tu aliyekuwa lulu ya kweli kwake au kuna zaidi aliokuwa nao baada ya kuigiza kuwa kweli.
  [​IMG]
   
 12. Emil Mwangwa

  Emil Mwangwa Senior Member

  #12
  Apr 28, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  MSIBA wa msanii maarufu wa filamu nchini Steven Kanumba umezidi kuibua mambo, safari hii Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Suleiman Kova, amejikuta kwenye mjadala mzito, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
  Sambamba na hilo, kamati ya mazishi ya msanii huyo imesema kuwa imetumia sh milioni 70 kwa ajili ya gharama za kuuaga hadi kuuzika mwili wa Kanumba, huku mama mzazi wa msanii huyo, akiambulia sh milioni 4 za rambirambi.
  Tukirejea kwenye sakata la Kova, kamanda huyo ameingia kwenye mjadala wa kifo cha Kanumba kutokana na hatua yake ya kuamua kutoa salamu za mwisho kwa kupiga saluti mbele ya jeneza la Kanumba.
  Tukio hilo limeibua hisia mbalimbali miongoni mwa askari na wananchi kwa ujumla, huku kila mmoja akisema lake.
  Baadhi ya askari na wananchi waliohudhuria hafla ya kuagwa kwa msanii huyo, walionyesha kushangazwa na kuhoji hatua ya Kova, kupiga saluti wakati wa kumuaga marehemu Kanumba.
  Mmoja wa maofisa wa juu wa Jeshi la Polisi, ambaye hakupenda kutajwa jina lake, alibainisha kuwa Kova alichanganyikiwa kuipigia saluti maiti ya Kanumba kwani ni kinyume cha kanuni na taratibu za kijeshi.
  "Askari ukiwa umevaa sare katika misiba ya kijeshi ni sawa kuaga maiti kwa kutoa salamu ya kijeshi (saluti), lakini napo inazingatia na cheo husika kwa kweli kama siku hiyo Kova alikuwa amekusudia kumpigia saluti aliyekuwa mgeni rasmi, (Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Ghalib Bilal), ila katika kuaga mwili wa Kanumba, alikuwa amekosea," alibainisha ofisa huyo.
  Baadhi ya wanaomjadili Kova wanahoji uhalali wa afisa huyo wa juu ya Jeshi la Polisi kutumia saluti katika kutoa heshima wakati salamu za aina hiyo hutolewa kwa polisi waliozidi vyeo.
  Kwa upande wake, Kamanda Kova ametoa ufafanuzi wa saluti aliyoitoa wakati akitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa Kanumba.
  Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, Kova alisema anawashangaa askari wanaomshangaa kwani salamu hiyo ni ya kawaida tu katika nidhamu ya kijeshi.
  Alisema kwa majeshi yote nchini, saluti ni salamu au heshima na alifanya hivyo kwa Kanumba kuonyesha heshima na jinsi alivyothamini kazi na mchango wake kwa taifa.
  Alisema askari yeyote aliyevalia sale ya polisi kama anataka kusalimia au kutoa salamu kwenye shughuli kama ile ya Kumuaga Kanumba, lazima apige saluti.
  "Katika hali ya kawaida askari mdogo anapaswa kupiga saluti kwa askari mkubwa, lakini askari anaweza kupiga saluti kwenye tukio la kutoa heshima za mwisho kama nilivyofanya kwa mtu yeyote na sio lazima kwa askari kwa hiyo nilikuwa sahihi," alifafanua Kova.
  Kwa mujibu wa Kova ni kosa kwa askari kutompigia saluti mkubwa wake, lakini sio kosa kwa askari yeyote kutoa heshima kwa marehemu hata kama aliyefariki ni mtu wa kawaida kama Kanumba.
  Alisema siku ya kuuaga mwili wa Kanumba kulikuwa na watu mbalimbali na kila mtu alitoa heshima kuendana na utamaduni au imani yake, lakini kwake ilikuwa lazima apige saluti.
  Katika hatua nyingine, Kamati ya Mazishi ya Kanumba, imetoa ufafanuzi wa gharama za mazishi ya msanii huyo.
  Hata hivyo taarifa hiyo ya fedha ilikuwa na mkanganyiko mkubwa wa hesabu na hivyo kuacha maswali mengi yasiyo na majibu.
  Katika ufafanuzi huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Gabriel Mtitu, ‘The Game, alibainisha kuwa jumla ya fedha za makusanyo yote ya michango ya mazishi ilikuwa sh 53,252,000, huku matumizi yakiwa sh 52,102,000.
  Mtitu alisema katika fedha hizo, ahadi za fedha taslimu zilikuwa sh 15,500,000 huku ahadi za vifaa ni sh 18,400,000 na ahadi zilizolipwa ni sh 2,850,000.
  Mtitu alibainisha kuwa jumla ya matumizi yalikuwa ni sh 70,502,000 na salio ni sh 4,000.000 ambazo zimekabidhiwa kwa mama wa marehemu na zitaendelea kukabidhiwa kadiri ya marejesho na ahadi zitakavyokuwa.
  Lakini kwa hesabu za mwenyekiti huyo zinajichanganya kulingana na takwimu hizo, kwani matumizi ya sh milioni 70.5 alizozitoa ni tofauti na kiwango alichodai kimekusanywa na kilichotumika katika maombolezo hadi mazishi.
  Mtitu alisema lengo la kuunda kamati hiyo lilikuwa kuhakikisha shughuli za msiba zinafanyika bila tatizo ikiwa ni pamoja na kuomboleza na kumzika msanii huyo.
  "Kamati hii sio ya kidini wala ya wasanii ila ni ya watu mchanganyiko akiwemo mwanamitindo Happiness Magese, Ridhiwani Kikwete, Jacob Steven, ‘JB', mimi mwenyewe na wengineo; imekuwa ikisikika kama wanakamati wameufanya msiba huo kama sehemu ya biashara, kitu ambacho si cha kweli," alisema Mtitu.
  Aliongeza kuwa marehemu Kanumba aliacha mali zenye thamani ya sh milioni 700, ambapo kulingana na jina lake lilivyokuwa kubwa hapa nchini na nchi za jirani, inaonyesha kuwa amefariki akiwa bado maskini.
  "Kiukweli mali alizoziacha hazilingani na yeye; Kanumba alikuwa ni mtu ambaye mataifa mbalimbali yalimfahamu kutokana na kazi zake, lakini mali alizoziacha ni aibu tupu," alisema Mtitu.
  Mtitu pia alikiri kwamba ratiba ya mazishi haikupangwa vizuri na kuwaomba radhi Watanzania wote walioshindwa kuuaga mwili wa msanii huyo.
   
 13. Emil Mwangwa

  Emil Mwangwa Senior Member

  #13
  Apr 28, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kwa nini asilaumiwe Kikwete analaumiwa Kova????
  [h=3]JK Aomboleza Msiba Wa Steven Kanumba[/h]
  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
  Nyumbani kwa marehemu, Sinza Vatican. Picha Zote: Ikulu
   
 14. Emil Mwangwa

  Emil Mwangwa Senior Member

  #14
  Apr 28, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  [h=3]JK Aomboleza Msiba Wa Steven Kanumba[/h]
  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
  Nyumbani kwa marehemu, Sinza Vatican. Picha Zote: Ikulu
   
 15. Emil Mwangwa

  Emil Mwangwa Senior Member

  #15
  Apr 28, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  [h=2]Jamani hii ya Kamanda Kova imekaaje?[/h]
  Naomba msaada kujua Kweli Salute ni nani anapigiwa kwani hapa naona anatoa salute wakati wa kumuaga Kanumba, I think this is not right, wanaojua please enlight me.[​IMG]
   
 16. GREATTHINKERMAN

  GREATTHINKERMAN Member

  #16
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kamanda Kova anajua alilopaswa kulitenda na aalilitenda bila kujali macho na maneno ya watu. Tatizo ni watu kuwa na uelewa mdogo juu ya salute. Kamanda mi nakupa salute kwa ulichokifanya.
  Saluuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuute. safi sana
   
 17. Pipiro

  Pipiro JF-Expert Member

  #17
  Apr 28, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 307
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Duuh mimi nilifikiri tatizo ni la kwangu kuwa uwezo wangu wa kuelewa una mushkeli kumbe la hasha.. Nimeshindwa kabisa kumuelewa jamaa ana maana gani au alikusudia nini hasa kwenye uzi wake huu.. Ila baada ya kufungua attachment najilazimisha kutaka kumuelewa hoja yake kuwa Afande Kova hakutakiwa ampigie jamaa saluti... Aah inanichanganya
   
 18. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #18
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kila maiti hupigiwa saluti?mbona kova alikubali kukosea?mimi nachojua askari atampigia askari mwenzake,na sikufuatilia msiba huu ila nina uhakika kuna askari wengine wadogo wengi tu hawajampigia saluti.kova alipitiwa
   
 19. Salathiel m.

  Salathiel m. JF-Expert Member

  #19
  Apr 28, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  ChecheeeeeeeeeeeeeeeeeeeEeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 20. Mjuni Lwambo

  Mjuni Lwambo JF-Expert Member

  #20
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 5,464
  Likes Received: 683
  Trophy Points: 280
  kova was right to salute the late kanumba
   
Loading...