Enzi za chama kimoja hakukuwa na viongozi wa vyama vya upinzani lakini sio kwamba upinzani haukuwepo. Wakati wa uchaguzi watu walielekezwa kuchagua kati ya picha ya Nyerere na kivuli lakini bado kuna watu walichagua kivuli bila ya kuongozwa na kiongozi yeyote wa upinzani.
Kwangu mimi kununua au kuhonga kiongozi aje upande wako ni stage ya mwisho ya chama kinachoelekea kupoteza dira au chama kinachoelekea kufa, kwamba chama kimeishiwa sera na mbinu za kuwafanya wananchi kujiunga nacho zaidi ya kutumia nguvu ya pesa na kuwahonga vyeo.
Nionavyo mimi njia sahihi ya kuuwa vyama vya upinzani ni kutimiza ahadi ambazo chama au mgombea alizitoa, kuwaletea wananchi maendeleo chanya kiasi kwamba viongozi au wananchi wenyewe wakose sababu ya kubaki upinzani.
Kununua kiongozi wa upinzani, hakuondoi shida ya maji watu wataendelea kudai maji, kununua viongozi wa upinzani hakufanyi elimu iwe bora, hakuongezi ajira wala hakuongezi mlo kwenye familia, kununua viongozi hakujengi viwanda wala hakuboreshi maisha ya Mtanzania.
Upinzani siyo viongozi, kiongozi wa upinzani ni shida unazopata, mateso unayopata, haki unayonyimwa kulingana na unavyostahili kupata, upinzani ni chakula chako unachopata, ni elimu yako uliyopata, kiongozi wa upinzani ni miundombinu yako, ni afya yako uliyonayo, ni upatikanaji wa maji, ni uhuru wa kujieleza ulionao, siku hivyo vitu vikikosekana akili yako yenyewe itakuongoza kumkataa aliyeko madarakani hautasubiri kuambiwa na kiongozi wa upinzani.
Kwahiyo kitendo cha kununua au kuhonga viongozi ili waje upande mmoja hakutafanya watu wakupende au wakipende chama chako, hata kama CCM itafanikiwa kuwanunua viongozi wote wa vyama vya upinzani, najua hakitaweza kuwanunua watanzania wote million 50, bado kitakuja kupambana na wananchi wenyewe na mbaya zaidi wananchi walioachwa watakuwa hawana kiongozi wa kuwaelekeza wafanye nini.