Kama Plato aliishi miaka 3000 kabla ya yesu na maandiko yake yapo hadi leo kwanini tusiamini uwepo wa Yesu kama Mungu?

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,417
30,927
Wana jukwaa pendwa naomba niulize swali kama habari za Plato na Aristotle ni za kweli na ziko documented kwann tutilie shaka kuwepo kwa yesu kristo wakati plato aliishi miaka elfu kabla ya yesu karibuni
 
Mapokeo ya kihistoria yanathibitisha existence ya Plato. Kwanza kazi zake bado zipo na zimekuwa na influence kubwa katika jamii since ancient time.

Modern day civilization ime stem from Greek civilization ambao tunajua kuwa wagiriki ndio watu wakwanza kuanzisha civilization ya binadamu kuishi kwa utashi ikiwa ni pamoja na kutunga sheria, kuanzisha mifumo ya elimu na mambo mengi yanayofanyika leo hii duniani.

Wanafalsafa kama Plato na wenzie ndio waliotengeneza hii misingi tunayoiona leo hii na inayoweza kuthibitika kisanyansi.

Lakini kwa suala ya Yesu hizo ni nadharia zilizoanzishwa na baadhi ya watu ambao mpaka leo haijajulikana nia yao ilikua nini lakini hudhaniwa kuwa nia yao ilikuwa ni indoctrination ili kuweza kuwa control wanadamu kwa kuwaogopesha kwa mambo yakutisha yasiyo na proof yoyote.
 
Kwani kuna ambae anabisha Yesu hakuwahi kuwepo?

Kinachobishiwa matamko yake kama vile Plato anavyobishiwa pia.
 
Mapokeo ya kihistoria yanathibitisha existence ya Plato. Kwanza kazi zake bado zipo na zimekuwa na influence kubwa katika jamii since ancient time.

Modern day civilization ime stem from Greek civilization ambao tunajua kuwa wagiriki ndio watu wakwanza kuanzisha civilization ya binadamu kuishi kwa utashi ikiwa ni pamoja na kutunga sheria, kuanzisha mifumo ya elimu na mambo mengi yanayofanyika leo hii duniani.

Wanafalsafa kama Plato na wenzie ndio waliotengeneza hii misingi tunayoiona leo hii na inayoweza kuthibitika kisanyansi.

Lakini kwa suala ya Yesu hizo ni nadharia zilizoanzishwa na baadhi ya watu ambao mpaka leo haijajulikana nia yao ilikua nini lakini hudhaniwa kuwa nia yao ilikuwa ni indoctrination ili kuweza kuwa control wanadamu kwa kuwaogopesha kwa mambo yakutisha yasiyo na proof yoyote.
Hapa umefel mkuu
 
Yesu alikuwepo.
Kuhusu Yesu kuwa mungu, hiyo ni imani kwa sababu hata Kim Il Sung kuna watu wanaamini ni mungu.
Hiyo ni juu yao kuamini au kutoamini.
 
!!!!!!! SHANGAZO!!!!!!!!
umesema miaka 3000 kabla ya Yesu? inamaana miaka tunayo ambiwa yesu alihudumu hapa duniani (30+) huwenda pilato alimhukumu yesu huku yeye (pilato) akiwa na miaka 3030+??

au ni zile kanuni za kuhesabu miaka kurudi nyuma ndio zimetumiia hapa?
Mkuu pilato na Plato ni watu wawili tofauti
 
!!!!!!! SHANGAZO!!!!!!!!
umesema miaka 3000 kabla ya Yesu? inamaana miaka tunayo ambiwa yesu alihudumu hapa duniani (30+) huwenda pilato alimhukumu yesu huku yeye (pilato) akiwa na miaka 3030+??

au ni zile kanuni za kuhesabu miaka kurudi nyuma ndio zimetumiia hapa?
Ndugu ama Mimi sijamuelewa mtoa Uzi au sijakuelewa wewe, huyo kasema Plato yaani yule Mwanafalsafa nguli na MTU wa kale sana, ila wewe naona umemsema Pilato....
 
Tunaamini Yesu alikuwepo pia kuna vitabu vilivyokwepo kabla yake ambavyo tunaviita agano la kale ambavyo tunavitumia pia.
 
Mapokeo ya kihistoria yanathibitisha existence ya Plato. Kwanza kazi zake bado zipo na zimekuwa na influence kubwa katika jamii since ancient time.

Modern day civilization ime stem from Greek civilization ambao tunajua kuwa wagiriki ndio watu wakwanza kuanzisha civilization ya binadamu kuishi kwa utashi ikiwa ni pamoja na kutunga sheria, kuanzisha mifumo ya elimu na mambo mengi yanayofanyika leo hii duniani.

Wanafalsafa kama Plato na wenzie ndio waliotengeneza hii misingi tunayoiona leo hii na inayoweza kuthibitika kisanyansi.

Lakini kwa suala ya Yesu hizo ni nadharia zilizoanzishwa na baadhi ya watu ambao mpaka leo haijajulikana nia yao ilikua nini lakini hudhaniwa kuwa nia yao ilikuwa ni indoctrination ili kuweza kuwa control wanadamu kwa kuwaogopesha kwa mambo yakutisha yasiyo na proof yoyote.
Eti nini?
Za Yesu ni nadharia?
 
Mungu hayupo.

At least nyie huwa mnajalibu ingawa bado.

Hata science inakiri pasipo na kitu kuna kitu,yaani vacum inasimama yenyewe ni sign ya kutokuwepo kitu.

Sasa Mungu hayupo,ila kuna............
 
Mkuu kuwepo kwa Yesu kama binadamu halipingwi. Kuna maoni tofauti juu ya Uungu wa Yesu. Hili ndo lina mitazamo tofauti. Hakuna anayepinga kwamba Plato na Aristotle walikuwepo ila sijasikia wakihusishwa na Uungu. Pande hizi mbili hazilinganishwi kwani hazifanani namna zinavyozungumzwa
 
Back
Top Bottom