Kama PhD 17 zimetutia hasara Taifa je bado tunahitaji kutamba kwa kujiita Wasomi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,837
2,000
Kama PhD 17 za Benki Kuu ya Tanzania ( BOT ) zimeshindwa kusimamia Rasilimali na Uchumi wa nchi hii hadi kuliingiza Taifa katika hasara kubwa ya Matrilioni ya Shilingi je kuna haja ya Watu wengine waliobahatika kupita Vyuo Vikuu na kupata Degree, Masters na hizo hizo PhD zao kutamba, kujivunia na kujiita Wasomi?

Nitashukuru pia kama leo mtaweza kunipa maana halisi ya neno Msomi kwani Mimi binafsi kwa Mtazamo wangu tokea nchi ipate Uhuru hadi leo najaribu mno kutafuta tofauti ya Kimantiki kati ya Waliosoma na Wasiosoma lakini bado sijaiona na sana sana wote nawaona wako sawa tu.

Nawasilisha.
 

rubii

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
11,430
2,000
Mimi Binafsi simlaumu msomi yoyote kuwa mbinafsi kwa kuwaza maendeleo yake na familia yake na kutelekeza nchi
1.kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake.
2.Elimu ni ngumu sana, mtu unasota kwa uchungu mpaka unapata Cheo cha kipekee
Hata mimi nikipata hiyo nafasi Haki nitauza mpaka ikulu ile Ukoo wangu wote unehemeke
 

izzo

JF-Expert Member
May 31, 2015
2,817
2,000
Tanganyika hakuna wasomi bali kuna watu wanamiliki vyeti vya viwango tofauti vya elimu
 

NONIYANG'WAKA

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
1,207
2,000
nikujibu kwa mfano.

wewe ni mlinzi wa mikate.

kila saa2 asubuhi unaanza shifti yako hadi SAA 2 usiku.

inapofika SAA 3 asbh mwajiri wako hukuretea "chai kavu" na unatakiwa unywe umekaa mlangoni kuliko mikate!!

Siku ya kwanza, ya pili........ ya mia, je, utapiga chai kavu tu au utakuwa unasukumia na slesi?


amini na wambieni hata malaika akipewa wizara ya madini, maliasili, fedha, nk lazima uundiwe tume tu.

ova
 

dist111

JF-Expert Member
Nov 29, 2012
3,255
2,000
Sasa unataka tuwapeleke std 7???

Hapo ni ujanja tu plus lobbying kwa saana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom