Kama Paul Makonda angekuwa RC Dar matukio ya ajabu yasingetokea, maana alidhibiti uhalifu. Wauza shisha walipotea kama barafu iliyoyeyuka

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Msingi wa jeshi la polisi imara ni operation ili kudhibidi uhalifu. Ndio maana Makonda kama mkuu wa masuala ya usalama aliamini kwenye operation.

Makonda alimsimamia vyema Igp Sirro wakati huo ni kamanda wa kanda maalumu kuhakikisha uhalifu wa kila aina unatoweka Dar.

Vibaka, wahuni, majambazi walipotea kabisa Dar.

Jeshi la polii lilikuwa na utayari wakati wote na hata yeye kama mkuu wa mkoa alihakikisha linapata vifaa kama magari.

Kwa mantiki hii kama Dar ingekuwa na Rc kama makonda matukio ya ajabuajabu yasingetokea.
 
Makonda hafai mshauri aanze kulima au afanye kazi zingine kimya kimya maana naamini hata akifanya biashara watu wengi hawatapenda kumuunga mkono..Ni mfano mbaya sana kwa nchi kwa yale aliyotendea watu.... Hata Gwajima alimfuta kabisa katika ulimwengu wa siasa...alitesa watu sana akajiona yeye ni yeye sasa atulie ashukuru hajakamatwa si alikua anaingia clouds na maslaha au hujui???
 
Yaani unamsema huyu makonda akiwa RC tuliweza kusikia matukio kama

1.watu kutekwa kama Moo, Roma ben sanane

2.kituo cha clouds kuvamiwa

3.kifo cha akwilinaa pale kinondoni

4.kituo cha stakishari maaskari wetu kuteswa na kuwawa

5.panya road

Na matukio mengi infact makonda ktk swala la security alishafeliii
 
Kama hivi
44b971b6aeed88d064edb45ed70c7ebc.jpg
 
Hamna kitu . Aliliweza Je kwa kupoteza watu ?! Au wasiojulikana na Noah zao nyeusi ?!. Sukuma gang bwana !!.

Ashukuru ana mahusiano mazuri na boss vinginevyo alitakiwa awe kama Sabaya .
Mambo mengine ni hadithi za kusadikika tu. Huna ushahidi wa dhahiri.

Habari za sukuma gang zinatoka wapi?
 
Back
Top Bottom