Kama Otile na Marioo sio Matajiri hadi sasa basi Diamond Platumz ni Genius

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,124
11,113
Ukija kwenye Tasnia ya mziki wa Afrika Mashariki basi kati ya vijana ambao wanaimba ule mziki ambao ni wa viwango vya juu na hawatumii nguvu basi Marioo na Otile Brown wa Kenya hiyo sifa wanastahili majamaa wanaimba mziki mzuri sana ambao kwa kazi zao hii leo walitakiwa wawe matajiri wakubwa kama Burna Boy, Skiliza Dear Ex ya Marioo na nyimbo nyingine za Marioo, Skiliza Woman ya Otilie na Such kind of love na ile ya Chaguo langu la moyo majamaa wanaimba ule mziki wa viwango vya juu

Lakini ukija kwenye maendeleo ambayo wameyapata kutokana na kazi zao sijui kama hawa vijana mziki wao umewalipa ipasavyo kwa kweli na kama wanaimba mziki mkali kama huu na bado sio matajiri basi Diamond Platnumz apewe tuzo ya heshima kwa kweli maana amegeuza sanaa kuwa Utajiri , kijana ameweza kuifanya sanaaa kuwa utajiri na hilo ndio swala nalotaka wasanii wetu wafikie hapo

Vijana wetu wajitahidi kugeuza sanaa kuwaletea utajiri Hamna kitu kinachoniuma kama msanii kukaa kwenye gemu akitoa kazi kali alafu unamkuta kachoka kachakaa
 
Ukija kwenye Tasnia ya mziki wa Afrika Mashariki basi kati ya vijana ambao wanaimba ule mziki ambao ni wa viwango vya juu
Tatizo Mgt nzuri hamna humo! Mario utakuta anaji Manage mwenyewe tu, huwezi fanya kila kitu mwenyewe
 
Ukija kwenye Tasnia ya mziki wa Afrika Mashariki basi kati ya vijana ambao wanaimba ule mziki ambao ni wa viwango vya juu na hawatumii nguvu basi Marioo na Otile Brown wa Kenya hiyo sifa wanastahili majamaa wanaimba mziki mzuri sana ambao kwa kazi zao hii leo walitakiwa wawe matajiri wakubwa kama Burna Boy, Skiliza Dear Ex ya Marioo na nyimbo nyingine za Marioo, Skiliza Woman ya Otilie na Such kind of love na ile ya Chaguo langu la moyo majamaa wanaimba ule mziki wa viwango vya juu

Lakini ukija kwenye maendeleo ambayo wameyapata kutokana na kazi zao sijui kama hawa vijana mziki wao umewalipa ipasavyo kwa kweli na kama wanaimba mziki mkali kama huu na bado sio matajiri basi Diamond Platnumz apewe tuzo ya heshima kwa kweli maana amegeuza sanaa kuwa Utajiri , kijana ameweza kuifanya sanaaa kuwa utajiri na hilo ndio swala nalotaka wasanii wetu wafikie hapo

Vijana wetu wajitahidi kugeuza sanaa kuwaletea utajiri Hamna kitu kinachoniuma kama msanii kukaa kwenye gemu akitoa kazi kali alafu unamkuta kachoka kachakaa

Bora kufa
 
Ukija kwenye Tasnia ya mziki wa Afrika Mashariki basi kati ya vijana ambao wanaimba ule mziki ambao ni wa viwango vya juu na hawatumii nguvu basi Marioo na Otile Brown wa Kenya hiyo sifa wanastahili majamaa wanaimba mziki mzuri sana ambao
Mario amejiweka kwa Jimama Mimi Mars unategemea nini na kununua mikorogo unategemea nini ....
 
Si pashagi makabichiii🎶🎶 kachezee unapo chezagaa🎶
 
Huyo Diamond kaanza muziki zamani pia marioo hajafikisha hata kiaka nane kwenye game.

Otile kinachomkosti ni ukenya wake, wakenya ndio wanamuangusha angekuwa hongo angekuwa star mkubwa kuliko sasa.

Btw huyo Diamond si mzee wa chukua 40 mimi nichukue 60?

Diamond ametoka mwaka 2009 na wimbo wa nenda kamwambie. Haukuwa hit lakini mwaka 2010 akatoa mbagala ndio uliokuwa hitsong yake ya kwanza mpaka watu tukamjua.

Kwa spidi na hasira za kutoboa aliyokuwa nayo diamond mpaka kufikia mwaka 2013 mwishoni tayari alishafika levo ya kufanya wimbo na msanii mkubwa davido. Aliimba na davido remix ya number one mwaka 2013. Hapo davido alilipwa usd 5000 ndio akakubali kushiriki

Jiulize mario na otile brown tangu wametoka tumeanza kuwajua wameshafika levo za kuimba na msanii mkubwa hata number 1 tu wa africa kwa miaka hii. Mziki unataka kujitoa ndipo unatajirika
 
Ungeandika kwa nini ali kiba sio tajiri kihivyo ningekuelewa lakini sio marioo wala otile,watanzania tunapenda short cut sana,kwa hit song gani alizonazo marioo hadi awe tajiri kupita kwenye beat za amapiano au!!!! Muziki una njia zake tusipende kulazimisha wasanii wa kawaida size ya dogo janja waonekane wakubwa mwisho wa siku wakifeli wanaangukia kwenye madawa ya kulevya ili kupunguza stress kwa kuwa tumewakuza kupita uwezo wao.in short hao wasanii uliowataja bado sana.
 
Umeeleza vizuri ila hapo kwenye nenda kwa haukuwa hit unatudanganya.

Pia nenda kamwambie ndio ulifanya tukamjua Diamond acha uongo mzee.
Mbagala yenyewe ilikuwa ni mwendelezo wa hits tu sijui ulitumia kigezo kipi au labda sikio lako tu

Nikikumbuka nenda kamwambie ilivyojuil inapigwa sehemu kibao nashangaa..
 
Ungeandika kwa nini ali kiba sio tajiri kihivyo ningekuelewa lakini sio marioo wala otile,watanzania tunapenda short cut sana,kwa hit song gani alizonazo marioo hadi awe tajiri kupita kwenye beat za amapiano au!!!! Muziki una njia zake tusipende kulazimisha wasanii wa kawaida size ya dogo janja waonekane wakubwa mwisho wa siku wakifeli wanaangukia kwenye madawa ya kulevya ili kupunguza stress kwa kuwa tumewakuza kupita uwezo wao.in short hao wasanii uliowataja bado sana.
Wewe hauujui mziki tulia
 
Mkuu na mfumo wa music industry hapa kwetu inachangia kua hivo, hit 1 tu inatakiwa ikubadilishe maisha kabisa na mifano kibao tunaona kama yule jamaa alieimba amarulla akazunguka africa nzima kupiga show.. mbele ukipata hit 1 tu umeaga umaskini unless upuyange mwenyewe usimamiz wa fedha.
 
Back
Top Bottom