Kama nitapiga kura yangu ya Hapana katika rasimu hii ya Warioba , basi kwa kipengele hichi cha 50/20

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,357
2,000
Kama nitapiga kura yangu ya Hapana katika rasimu hii ya Warioba ,basi kipengele hichi cha Wabunge wa Tanganyika kuwa 50 na Zanzibar kua 20 ni mistake kwa Smz ,kwakua najua munakwenda kutunyoga Znz kwenye Bunge la Muungano kwakutumia veto ya wingi wenu Watanganyika.
Nimejaribu kupitia Rasimu nimeona hili la wabunge wa Jamuhuri ya Muungano watakuwa 50 kwa Tanganyika na 20 Zanzibar .
Hivi warioba na tume yake hapa kweli walitenda haki? mana ukiisoma Rasimu inazungumza wazi wazi ni shirikisho la nchi 2 mbili zilizoungana., inakuwaje nchi moja itowe 50 nyengine 20? Hii nikukusudia kwenda kutunyonga kwenye Bunge kwa kutumia wingi wetu?.
Mbona hawa Tanganyika wanataka kuendelea kutuburuza tena kwenye bunge? hivi Comoro na Ruwanda nchi ndogo lakini inawakilisha wabunge sawa sawa 9 tisa na nchi kubwa kwenye Muungano wa afrika Mashariki.
Inakuwaje Muungano huu wa shirikisho la nchi 2 Tanganyika na Zanzibar, Zanzibar tuhukumiwe kwa udogo wetu wakati ni swala la nchi mbili huru zenye hadhi sawa sawa katika shirikisho hili la Muungano?
Jee hapa Warioba kweli umetutendea haki Wazanzibar? Maswala ya serekali ya shirikicho(Shirika) ,yote yawe na uiano kwa vile kuna nchi mbili zenye hadhi zake sawa sawa na mambo yake.
Kuna hatari mbeleni hapa ,kwamaana kila itakapohitajika ipigwe kura, kwenye bunge la Muungano kuamua kitu,Wazanzibar tutashindwa kwa ajili ya uchache wa wabunge tulionao katika bunge la Muungano hii ni mtego tumetegwa kuburuzwa tena, mambo yanayo husu muungano yawe na usawa kwa vile ni mambo yanayohusu nchi mbili.na kitakacho jadiliwa Zaidi katika Bunge ni maslahi ya nchi mbili Zaidi.
Hii Warioba haikubaliki. Bunge nikwenda kutuzidi nguvu,Bunge ni chombo chenye maamuzi. 50% ya Wabunge itaipa uwezo wa Tanganyika kuweza kupitisha sheria yoyote inayohusu muungano bila Zanzibar kuwa na sauti ya kupinga
Ni ujuha kukubali uwiano wa namna hiyo.
Uamuzi wowote ambao Tanganyika watataka kuupitisha, utapita hata kama hao wawakilishi wote wa ZNZ wakiukataa hata kama utatumia kigezo cha simple majority.hii ni hatari kwa Zanzibar .
Tunaweza kukubali kama kuna mgao wa chakula cha msaada kwa waathirka wa njaa! Hapo nitakubaliana na wewe Watioba kutumia wingi wenu.lakini sio nchi mbili huru katika kutunga sheria, Warioba umeshemsha umeturudisha kule kule kwenye vita kwa kutupeleka kutunyoga kwa wingi wenu.
Kuna swala hili lisilo na mashiko wala ukweli kuhusu share cost za muungano sawa kwa sawa tushanjie Wazanzibar Katika Muungano,Hili halina ukweli wowote wakua Zanzibar tutashindwa au hatuwezi kama alivyo jisaliti na kujizalilisha Nahodha kwa kuto kutumia akili yake na kua mvivu wakufikiri .
Mara nyingi viongozi wetu wa Smz hujaribu kupotoa ukweli mpele ya Wazanzibar kuona kua Generation hii haijuwi kuchambua mambo na wao wana akili Zaidi kuliko raia wakawaida.
Tukija katika kuchangia ulinzi wizara uloitolea mfano kua inatumia pesa nyingi (ulinzi)Mh Shamsu Nahodha ufahamu kua Tanganyika ina eneo kubwa linalohitaji askari wengi na vifaa vingi vya kulinda mipaka na ulinzi mwingine wa ndani ya nchi ukilinganisha na Zanzibar? na Tanganyika ina watu wengi zaidi wanaohitaji gharama kubwa zaidi kiulinzi kuliko Zanzibar.Kwa mantiki hiyo, ukisema budget ya ulinzi igaiwe sawa kwa sawa,na Zanzibar hapo utakuwa unainyonya ZNZ.
Harama za kuchangia Zanzibar katika shirikisho la Muungano
Harama za kuchangia Zanzibar katika shirikisho la Muungano halitokua swala gumu kwa Zanzibar kushindwa kuchangia pindipo ,tutakua na mamlaka kamili , lakini ikiwa mambo yote ya nje yamemilikiwa na Serekali ya Muungano,Bank kuu,Sarafu,na mengineo?
Nikweli Zanzibar tunaweza kushindwa kuchangia Muungano, na kwa mimi nitatafsiri ni kukomolewa kwa makusudi ili tushindwe kuchangia, na Mfano huu itakua ni sawa na Mzee Mandela alipogombania uraisi wa south Africa .
Wazungu wa South Africa ,walizihamisha pesa zote katika ma-bank ya south africa ili Mzee Mandela akingia katika madaraka ashindwe kuongoza nchi kwa kuikuta nchi iko haina saving bank .
Hii ilikuwa ni kukomolewa Mzee Madela na Matajiri wa kizungu kwa mbinu za kumuangusha ,na kuonekana kashindwa kuongoza na kuwatatulia hali zao wananchi.
Sasa na formula hii hii ndio wanayotaka Tanganyika kuitumia kwa kutukomoa Wazanzibar.
Tukija swala jengine aliotushemshia Warioba ni Hadhi ya Raisi wa Muungano ambaye kwa uiano huu siku zote atakua anatoka Tanganyika kwa wingi wao.
Raisi wa Muungano katika ibara inayosema kutokezea hali ya hatari anao uwezo bila ya kushauriana na Bunge la Muungano , anao uwezo wa kuwasiliana na mkuu wa Jeshi na usalama wa Taifa kutangaza vita bila kulishauri Bunge.
Huu ni Mpengo mwengine tumetegwa Wazanzibar kuweza kusalimu amri na kusalimisha amri vikosi vyetu.
Hapa hakutajwa Raisi wa Muungano kuwasiliana kwanza na Raisi wa Zanzibar au Tanganyika? Imetajwa kuwasiliana na wakuu wa jeshi au usalama?
Sasa jalia Raisi wa Muungano kamua kuivamia Zanzibar kijeshi itakuaje na huku ana kizuizi chochote kinacho mpiga ikiwa washauri wake ni wakuu wa Jeshi na usalama?.
Hili ni kosa na linaweza mbeleni kutuharimu sana na tukajuta kwa vile Jeshi lote hivi sasa mpaka la polisi ni mali ya Muungano, jee tumeliangaliaje Wazanzibar hili katika rasimu mpya kujikinga?.
Swala jengine ni nguvu na hadhi ya Zanzibar hivi sasa kuelekea Katiba mpya iko wapi? Ikiwa Baraza la wawakilishi litabadilisha kitu chochote kisicho kubalika na katiba ya Muungano,kitu hicho hakitokua na nguvu automatic .
Mfano haya marekebisho ya katiba ya Zanzibar kipengele namba 10 zanzibar kuwa na vikosi vyake vya ulinzi vya Smz ambalo ni jeshi la polisi la Zanzibar , hivi sasa unambiwa Kuanzia Jeshi na Polisi lote ni moja na ni la Muungano.
Kati ya mambo ambayo naomba Mungu asaidie ni huu muungano kuvunjika!
Labda kama kuna umuhimu wake basi umebaki siri ya viongozi.. lakini kwa mimi Mzanzibar naona ni kilimacho tu tunavyo fanyiwa na viongozi !
Nasema hivi kwa nini? Ukilinganisha Rasimu ya Warioba na Ubabe wa Mick Tyson haina tafauti yoyote ile kilichotumika hapa ni nguvu tu za ku force mambo kwa utashi wa viongozi wa Tanganyika, kutumia nguvu silazima utumie vyombo vya dola laa.
Hii aloitumia Warioba ni nguvu ya madaraka sio rudhaa ya wananchi wenyewe ,
Ungwana hapa ilikuwa kabla ya katiba mpya kufanywa , ilikuwa ibuliwe mwanzo Tanganyika ikae na Zanzibar ili kujadiliana lipi liwe la Muungano na lipi kila mtu abakie nalo mwenyewe?.
Sasa hii iliotumiwa ni force kupwa zidi ya raia wa Zanzibar , na niku high jack maoni ya Wananchi wa Zanzibar na Baraza lau la Uwakilishi, Sote tumechuhudia Warioba alivyo eleza kibabe mimi naita kibabe kwa ukweli huu.
Warioba kapuuza maoni ya Wananchi wa Zanzibar na Baraza letu la wawakilishi, kakiri mwenyewe kusema wananchi wa Zanzibar 60% walitaka Serekali ya Mkataba na Baraza la Wawakilishi walitaka Serekali 3 lakini zenye Mamlaka kamili.
Sasa kwa maneno haya nikua warioba hakuheshimu mamuzi ya Wananchi wa Zanzibar wala Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, ndio maana nikasema Warioba kafanya mapinduzi Baridi zidi ya Zanzibar.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom