Kama nitakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kwanza mkuu unamuaibisha the great thinker, Albert Einstein.

Wasema demokrasia ni moja?Hivi nikuulize kwanza demokrasia ilianzia wapi?
 
Habari zenu wana JF. Moja kwa moja kwenye mada;

Kulingana na maono yangu kuhusiana na suala la maendeleo katika jamii ya watu wa Tanzania, naona asilimia kubwa ya watu wamesahau kitu ambacho waasisi wetu wa taifa walikua wamekiacha kama kifaa cha kuleta maendeleo. Mnamo mwaka 1967 kulikuwa na azimio la Arusha kuhusiana na siasa ya ujamaa na kujitegemea.

Siasa ya ujamaa na kujitegemea ililenga serikali kutumikia wananchi wake na watu katika jamii kusaidiana.Kila mtu kuweza kubuni fursa zitakazo tatua changamoto za kijamii.

Ni dhahiri kwamba waasisi wa taifa walikua na maono mazuri lakini walishindwa kubuni njia sahihi na nzuri za kuleta maendeleo.Hata sasa tunajua ya kuwa Mtanzania anaweza akatoa wazo zuri kwelikweli ambalo litatatua changamoto za kijamii, lakini hawawezeshwi kufikia ndoto zao.

Swali la msingi Watanzania wenzangu:Katika miaka 60 ya uhuru je Tanzania inafanya siasa ya ujamaa na kujitegemea au imebadilisha mlengo na kuingia katika siasa ya ubepari pasipo kuwa na azimio lolote lile?

Kama nitakua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania;

Nitakuwa moja ya viongozi wanaopinga siasa ya vyama vingi. Siasa ya vyama vingi ni siasa ya kibepari. Ili Tanzania iweze kuendelea ni lazima wote tuwe na malengo sawa na sawia.Nitavunja vyama vyote vya siasa(kuanzia kile nitakachokitumikia mpaka vile vya upinzani).Chama kipya cha taifa kitaundwa ambacho kitachukua viongozi na sio watawala.Yoyote yule aliye Mtanzania na mzalendo atajiunga pasipo kuangalia chama chake alichokitumikia hapo kabla.Nia ya kufanya hivyo ni kuwa na malengo sawa ya kimaendeleo hivyo kuhamasisha shauri na sio kupakaziana mabaya.

Mnamo mwaka 1944, Bretton Woods Institutions:IMF,WB ziliundwa nchini Marekani kwa lengo la kusaidia nchi za Ulaya kujijenga kiuchumi baada ya vita vya pili vya dunia.Lakini mnamo mwaka 1980 mlengo ulibadilika na kuhamia Afrika kwa kile walichokiita mpango wa kuondoa umasikini bara la Afrika.Ukoloni mambo-leo ukazaliwa na kuota mizizi katika ardhi ya bara la Afrika.

Zile SAP's ndizo chanzo kikuu cha ukoloni mambo-leo.Natumaini mnazijua SAP's pamoja na kanuni(principles) zake.

Leo hii watu wanaiita Marekani,mama wa demokrasia ilhali hiyo demokrasi yao imeleta mashoga(kwa misingi ya mtu kufanya chochote anachokitaka*Sisi Watanzania hatuna tamaduni hii na hatuwezi ikubali),imeshindwa kufuta ubaguzi wa rangi,maandamano ambayo jeshi la polisi limetumia nguvu ilhali watu wanasema ukweli,watu kuvamia bunge,masikini kukosa malazi(homeless) n.k.

Ukweli ni huu:wakati utafika Tanzania kuwa na demokrasia yake ambayo itaendana na mahitaji ya watu wake.Je panaweza kuwa na demokrasia ilhali chama cha siasa ni kimoja?Jibu langu ni ndiyo.Hili taifa kwa sasa halina enzi kuu(sovereignty) kwa sababu kuna viongozi ambao ni vibaraka wa nchi za kibepari na hutumia siasa ya vyama vingi kama chaka la kuficha maovu yao.

Siasa ya ujamaa na kujitegemea ndiyo siasa pekee itakayoleta elimu bure,matibabu bure,uwajibikaji,uzalendo,ubunifu,uwezeshaji,umoja,upendo,amani,maisha yenye kipato kizuri kwa kila Mtanzania.Ila kama tutaendelea kwa njia hii ya kutegemea uwekezaji kutoka nje(ubepari) mafarakano kati ya mkulima na mwekezaji,mfugaji na mwekezaji,mchimba madini na mwekezaji hajataisha na nchi haitokuja kuendelea.

Kwa nini nchi haitokuja kuendelea?Jibu:kwa sababu wawekezaji wa nje ni lazima wachukue asilimia kubwa katika magawio ilo kupata faida.Sasa kumbuka wakati wao wanachukua faida kujenga nchi zao vilevile sisi tunapata faida lakini yenye hasara,kwa nini?Jibu:Kwa sababu sisi hatuna wawekezaji wakubwa katika nchi za kigeni hususani Ulaya na Marekani hivyo hatuchukui faida kutoka kwao.Wakati sisi tunapiga hatua moja wale wanapiga hatua mia moja.Sasa tutawafikia lini?Au kwenye ndoto?Hii nchi inavyoendeshwa kuelekea maendeleo ni kana kwamba nchi nyingine zimelala!!

Kama nitakua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.....
wewe ungekuwa wa kwanza kuuliwa na kufutiliwa mbali kabisa, unataka uturudishe kwenye siasa za enzi za mao ze dong tsetsung za miaka ya 1940 na enzi za kina nyerere.

wenzako wanasonga mbele wewe unarudi nyuma. Hivi inamaana mpaka sasa hujajua tuu kitu kilichoondosha utawala wa magufuli na bashiru madarakani mapema? ni practice ya siasa hizo za mambo ya kijamaa, matokeo yake zikaishia kuleta chuki na ukabila ndani ya jamii.

pia ni unafki huo, hapo ni lazma tuu viongozi watajinufaisha na kusababisha wananchi wagundue ni unafki tuu, hatimae chuki.

ukimfosi mwananchi kufanya kitu ambacho wee mwenyewe badae utaonekana kwako hukitimizi na kujilimbikizia faida wewe tuu (ujamaa), utaonekana mnafki na msaliti mkubwa na kusababisha chuki.

Heri mtu ambaye yuko free asiyefungamana na upande wowote au mwenye kufuata ubepari, hata badae akija kuonekana anamiliki kitu kikubwa au anafaidika sana, haiwezi ikawa unafki wala kuleta chuki, maana hakufosi mtu wala watu waishi kwa ujamaa na tyari ilishagundulika ubepari ndo zake.
 
Mkuu sijapata majibu sahihi kwa sababu wapo wanaosema 'yes' na wapo wanaosema 'no'.Ninahitaji ushaidi kuhusu Sera zao ili tujue Kama ni za kijamaa au kibepari
 
Mimi nikiwa Rais wa JMT cha kwanza kabisa nitakachofanya ni kufungua ile website yetu pendwa ya "Swaumu" ambayo maza kaifunga mpaka tutumie VPN
 
wewe ungekuwa wa kwanza kuuliwa na kufutiliwa mbali kabisa, unataka uturudishe kwenye siasa za enzi za mao ze dong tsetsung za miaka ya 1940 na enzi za kina nyerere.

wenzako wanasonga mbele wewe unarudi nyuma. Hivi inamaana mpaka sasa hujajua tuu kitu kilichoondosha utawala wa magufuli na bashiru madarakani mapema? ni practice ya siasa hizo za mambo ya kijamaa, matokeo yake zikaishia kuleta chuki na ukabila ndani ya jamii.

pia ni unafki huo, hapo ni lazma tuu viongozi watajinufaisha na kusababisha wananchi wagundue ni unafki tuu, hatimae chuki.

ukimfosi mwananchi kufanya kitu ambacho wee mwenyewe badae utaonekana kwako hukitimizi na kujilimbikizia faida wewe tuu (ujamaa), utaonekana mnafki na msaliti mkubwa na kusababisha chuki.

Heri mtu ambaye yuko free asiyefungamana na upande wowote au mwenye kufuata ubepari, hata badae akija kuonekana anamiliki kitu kikubwa au anafaidika sana, haiwezi ikawa unafki wala kuleta chuki, maana hakufosi mtu wala watu waishi kwa ujamaa na tyari ilishagundulika ubepari ndo zake.
Mkuu rejea uzi wa awali.Kwa hiyo unataka kusema zao la wahuni, viroboto, kupe, chawa, walaji urefu wa kamba ni zao la ujamaa?
 
Mkuu sijapata majibu sahihi kwa sababu wapo wanaosema 'yes' na wapo wanaosema 'no'.Ninahitaji ushaidi kuhusu Sera zao ili tujue Kama ni za kijamaa au kibepari
 
Mkuu nasikitika kwa kutopata ushaidi wa sera.
 
Mkuu nasikitika kwa kutopata ushaidi wa sera.
Katiba ya JMT 1977
SEHEMU YA PILI
MALENGO MUHIMU NA MISINGI YA MWELEKEO WA SHUGHULI ZA SERIKALI
9.(k) kwamba nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.
 
Katiba ya JMT 1977
SEHEMU YA PILI
MALENGO MUHIMU NA MISINGI YA MWELEKEO WA SHUGHULI ZA SERIKALI
9.(k) kwamba nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.
Sijakataa kama katiba inasema.Je katiba inafuatwa?Hivi kabisa mnadhani hii nchi inaendeshwa kijamaa?
 
Umsamehe bure alikuwa hajazaliwa huyo enzi za ujamaa na kujitegemea.
Mkuu rejea uzi wa awali.Nimesema waasisi walikua na maono mazuri ila walishindwa kubuni njia sahihi za kuleta maendeleo.Ndio maana nchi ilivyomshinda Mwl.J.K.Nyerere akaamua kung'atuka (kujiuzulu) kutokana na shinikizo kutoka Bretton Woods Institutions akamuachia Mwinyi.Ukweli ni huu:Toka awamu ya Mwinyi hii nchi inaongozwa kibepari japokua katiba inasema ujamaa (kama uelewi ubepari rejea kamusi ili usikurupuke) sasa nieleze huo ubepari umesaidia nini Tanzania ilhali hali halisi ya nchi unaijua.
 
Habari zenu wana JF. Moja kwa moja kwenye mada;

Kulingana na maono yangu kuhusiana na suala la maendeleo katika jamii ya watu wa Tanzania, naona asilimia kubwa ya watu wamesahau kitu ambacho waasisi wetu wa taifa walikua wamekiacha kama kifaa cha kuleta maendeleo. Mnamo mwaka 1967 kulikuwa na azimio la Arusha kuhusiana na siasa ya ujamaa na kujitegemea.

Siasa ya ujamaa na kujitegemea ililenga serikali kutumikia wananchi wake na watu katika jamii kusaidiana.Kila mtu kuweza kubuni fursa zitakazo tatua changamoto za kijamii.

Ni dhahiri kwamba waasisi wa taifa walikua na maono mazuri lakini walishindwa kubuni njia sahihi na nzuri za kuleta maendeleo. Hata sasa tunajua ya kuwa Mtanzania anaweza akatoa wazo zuri kwelikweli ambalo litatatua changamoto za kijamii, lakini hawawezeshwi kufikia ndoto zao.

Swali la msingi Watanzania wenzangu: Katika miaka 60 ya uhuru je Tanzania inafanya siasa ya ujamaa na kujitegemea au imebadilisha mlengo na kuingia katika siasa ya ubepari pasipo kuwa na azimio lolote lile?

Kama nitakua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania;

Nitakuwa moja ya viongozi wanaopinga siasa ya vyama vingi. Siasa ya vyama vingi ni siasa ya kibepari. Ili Tanzania iweze kuendelea ni lazima wote tuwe na malengo sawa na sawia.Nitavunja vyama vyote vya siasa(kuanzia kile nitakachokitumikia mpaka vile vya upinzani). Chama kipya cha taifa kitaundwa ambacho kitachukua viongozi na sio watawala. Yoyote yule aliye Mtanzania na mzalendo atajiunga pasipo kuangalia chama chake alichokitumikia hapo kabla. Nia ya kufanya hivyo ni kuwa na malengo sawa ya kimaendeleo hivyo kuhamasisha shauri na sio kupakaziana mabaya.

Mnamo mwaka 1944, Bretton Woods Institutions:IMF,WB ziliundwa nchini Marekani kwa lengo la kusaidia nchi za Ulaya kujijenga kiuchumi baada ya vita vya pili vya dunia. Lakini mnamo mwaka 1980 mlengo ulibadilika na kuhamia Afrika kwa kile walichokiita mpango wa kuondoa umasikini bara la Afrika.Ukoloni mambo-leo ukazaliwa na kuota mizizi katika ardhi ya bara la Afrika.

Zile SAP's ndizo chanzo kikuu cha ukoloni mambo-leo.Natumaini mnazijua SAP's pamoja na kanuni(principles) zake.

Leo hii watu wanaiita Marekani, mama wa demokrasia ilhali hiyo demokrasi yao imeleta mashoga(kwa misingi ya mtu kufanya chochote anachokitaka*Sisi Watanzania hatuna tamaduni hii na hatuwezi ikubali), imeshindwa kufuta ubaguzi wa rangi, maandamano ambayo jeshi la polisi limetumia nguvu ilhali watu wanasema ukweli, watu kuvamia bunge, masikini kukosa malazi(homeless) n.k.

Ukweli ni huu:wakati utafika Tanzania kuwa na demokrasia yake ambayo itaendana na mahitaji ya watu wake.Je panaweza kuwa na demokrasia ilhali chama cha siasa ni kimoja?Jibu langu ni ndiyo.Hili taifa kwa sasa halina enzi kuu(sovereignty) kwa sababu kuna viongozi ambao ni vibaraka wa nchi za kibepari na hutumia siasa ya vyama vingi kama chaka la kuficha maovu yao.

Siasa ya ujamaa na kujitegemea ndiyo siasa pekee itakayoleta elimu bure,matibabu bure,uwajibikaji,uzalendo,ubunifu,uwezeshaji,umoja,upendo,amani,maisha yenye kipato kizuri kwa kila Mtanzania.Ila kama tutaendelea kwa njia hii ya kutegemea uwekezaji kutoka nje(ubepari) mafarakano kati ya mkulima na mwekezaji,mfugaji na mwekezaji,mchimba madini na mwekezaji hajataisha na nchi haitokuja kuendelea.

Kwa nini nchi haitokuja kuendelea?Jibu:kwa sababu wawekezaji wa nje ni lazima wachukue asilimia kubwa katika magawio ilo kupata faida.Sasa kumbuka wakati wao wanachukua faida kujenga nchi zao vilevile sisi tunapata faida lakini yenye hasara,kwa nini?Jibu:Kwa sababu sisi hatuna wawekezaji wakubwa katika nchi za kigeni hususani Ulaya na Marekani hivyo hatuchukui faida kutoka kwao.Wakati sisi tunapiga hatua moja wale wanapiga hatua mia moja.Sasa tutawafikia lini?Au kwenye ndoto?Hii nchi inavyoendeshwa kuelekea maendeleo ni kana kwamba nchi nyingine zimelala!!

Kama nitakua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.....
Huna akili kamwe you can't to be president..... mfumo wa ujama ni mfumo duna.
Ili ufanye maendeleo unatakiwa ufungue mipaka na kuruhusu ushindani wa biashara wenzetu wazungu hii waliliona mapema sana
 
Naomba ushaidi? Kuna Uzi pia hapa JF una haya maudhui. Sijawahi elewa kwa nini masikio yenu yapo sensitive kumsikiliza Mmarekani. Kwanza naomba ushaidi alafu niambie China inaongozwa na chama gani, je kuna vyama vingapi, na sera zao ni zipi? Sasa tuone hizo sera ni za kijamaa au kibepari. Vilevile toa ushaidi kwamba sera za urusi ni za kibepari.

Vilevile nitajie rank ya North Korea kiuchumi duniani? Nanitolee ushaidi wa picha unaoonyesha umasikini wa nchi hiyo.Kama umetanguliza sikio kabla ya jicho basi hakuna unachojua maana utaishia kusema: mara kuna mtu alitoroka akahojiwa UN...., mara wanawake wananyanyaswa, maneno kibao pasipo ushaidi wa picha ni ubatili
Mzee mbona unataka kutulazimisha kuamini vitu Ambazo siyo.....
Yaani ikiambiwa useme Russia, china ni nchi za kijamaa. Utataja Duh!!! Aibu kubwa sana...
 
Huna akili kamwe you can't to be president..... mfumo wa ujama ni mfumo duna.
Ili ufanye maendeleo unatakiwa ufungue mipaka na kuruhusu ushindani wa biashara wenzetu wazungu hii waliliona mapema sana
Labda nikuulize,Hivi Tanzania inaongozwa kijamaa au kibepari?
 
Back
Top Bottom