Kama nitakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Habari zenu wana JF. Moja kwa moja kwenye mada;

Kulingana na maono yangu kuhusiana na suala la maendeleo katika jamii ya watu wa Tanzania, naona asilimia kubwa ya watu wamesahau kitu ambacho waasisi wetu wa taifa walikua wamekiacha kama kifaa cha kuleta maendeleo. Mnamo mwaka 1967 kulikuwa na azimio la Arusha kuhusiana na siasa ya ujamaa na kujitegemea.

Siasa ya ujamaa na kujitegemea ililenga serikali kutumikia wananchi wake na watu katika jamii kusaidiana.Kila mtu kuweza kubuni fursa zitakazo tatua changamoto za kijamii.

Ni dhahiri kwamba waasisi wa taifa walikua na maono mazuri lakini walishindwa kubuni njia sahihi na nzuri za kuleta maendeleo. Hata sasa tunajua ya kuwa Mtanzania anaweza akatoa wazo zuri kwelikweli ambalo litatatua changamoto za kijamii, lakini hawawezeshwi kufikia ndoto zao.

Swali la msingi Watanzania wenzangu: Katika miaka 60 ya uhuru je Tanzania inafanya siasa ya ujamaa na kujitegemea au imebadilisha mlengo na kuingia katika siasa ya ubepari pasipo kuwa na azimio lolote lile?

Kama nitakua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania;

Nitakuwa moja ya viongozi wanaopinga siasa ya vyama vingi. Siasa ya vyama vingi ni siasa ya kibepari. Ili Tanzania iweze kuendelea ni lazima wote tuwe na malengo sawa na sawia.Nitavunja vyama vyote vya siasa(kuanzia kile nitakachokitumikia mpaka vile vya upinzani). Chama kipya cha taifa kitaundwa ambacho kitachukua viongozi na sio watawala. Yoyote yule aliye Mtanzania na mzalendo atajiunga pasipo kuangalia chama chake alichokitumikia hapo kabla. Nia ya kufanya hivyo ni kuwa na malengo sawa ya kimaendeleo hivyo kuhamasisha shauri na sio kupakaziana mabaya.

Mnamo mwaka 1944, Bretton Woods Institutions:IMF,WB ziliundwa nchini Marekani kwa lengo la kusaidia nchi za Ulaya kujijenga kiuchumi baada ya vita vya pili vya dunia. Lakini mnamo mwaka 1980 mlengo ulibadilika na kuhamia Afrika kwa kile walichokiita mpango wa kuondoa umasikini bara la Afrika.Ukoloni mambo-leo ukazaliwa na kuota mizizi katika ardhi ya bara la Afrika.

Zile SAP's ndizo chanzo kikuu cha ukoloni mambo-leo.Natumaini mnazijua SAP's pamoja na kanuni(principles) zake.

Leo hii watu wanaiita Marekani, mama wa demokrasia ilhali hiyo demokrasi yao imeleta mashoga(kwa misingi ya mtu kufanya chochote anachokitaka*Sisi Watanzania hatuna tamaduni hii na hatuwezi ikubali), imeshindwa kufuta ubaguzi wa rangi, maandamano ambayo jeshi la polisi limetumia nguvu ilhali watu wanasema ukweli, watu kuvamia bunge, masikini kukosa malazi(homeless) n.k.


Ukweli ni huu:wakati utafika Tanzania kuwa na demokrasia yake ambayo itaendana na mahitaji ya watu wake.Je panaweza kuwa na demokrasia ilhali chama cha siasa ni kimoja?Jibu langu ni ndiyo.Hili taifa kwa sasa halina enzi kuu(sovereignty) kwa sababu kuna viongozi ambao ni vibaraka wa nchi za kibepari na hutumia siasa ya vyama vingi kama chaka la kuficha maovu yao.

Siasa ya ujamaa na kujitegemea ndiyo siasa pekee itakayoleta elimu bure,matibabu bure,uwajibikaji,uzalendo,ubunifu,uwezeshaji,umoja,upendo,amani,maisha yenye kipato kizuri kwa kila Mtanzania.Ila kama tutaendelea kwa njia hii ya kutegemea uwekezaji kutoka nje(ubepari) mafarakano kati ya mkulima na mwekezaji,mfugaji na mwekezaji,mchimba madini na mwekezaji hajataisha na nchi haitokuja kuendelea.

Kwa nini nchi haitokuja kuendelea?Jibu:kwa sababu wawekezaji wa nje ni lazima wachukue asilimia kubwa katika magawio ilo kupata faida.Sasa kumbuka wakati wao wanachukua faida kujenga nchi zao vilevile sisi tunapata faida lakini yenye hasara,kwa nini?Jibu:Kwa sababu sisi hatuna wawekezaji wakubwa katika nchi za kigeni hususani Ulaya na Marekani hivyo hatuchukui faida kutoka kwao.Wakati sisi tunapiga hatua moja wale wanapiga hatua mia moja.Sasa tutawafikia lini?Au kwenye ndoto?Hii nchi inavyoendeshwa kuelekea maendeleo ni kana kwamba nchi nyingine zimelala!!

Kama nitakua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.....
Hakuna kiongozi aliyepo madarakani anayekufikiria wewe na Mimi, kila mtu anawekeza kwa kizazi chake na walio nae karibu sana.Cha msingi kila ulipo pambana na usisahau kupiga kura uwatengenezee wenzio maisha.Hata wewe ukiingia jambo ambalo haliwezi kutokea ubinafsi na hulka nyingine zenye laana zitakuwa dhahiri.Afrika ni shida sana, hakuna atakayetokea mwenye fikra pevu kama Nyerere sio Steve au Yeriko.
 
Back
Top Bottom