Kama ningekuwa Ruge ningempigia magoti Lady Jaydee na kumuomba msamaha

Jospina

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,421
1,387
Katika kipindi cha Sun Downer cha Magic FM, mtangazaji huyo amesema kwamba shangwe zilizolipuka mara baada ya Jaydee kutajwa kuwa miongoni mwa wanaowania tuzo ya msanii bora wa kike katika tuzo za KTMA, ni ishara ya mwanadada huyo kukubalika katika jamii.

Mtangazaji huyo amesema kwamba Jaydee ni mwanamke mwenye uthubutu katika harakati za kuyasaka maisha na kwamba yeyote mwenye nia ya kukwamisha jitihada zake aibu na iwe juu yake.

Ameongeza kuwa kukubalika kwa mwanadada huyu pia kulidhihirika pale watazamaji katika tukio hilo walipomshinikiza Meneja wa msanii huyo (Gadna) kutaja kiingilio na tarehe ya maadhimisho ya miaka 13 ya Jaydee katika uga wa muziki.

Hivyo, Sebo anaona ni vyema Ruge akajishusha na kumaliza tofauti zake dhidi ya Jaydee

 
kwakweli ruge hana sababu ya kuzidi kupoteza muda mwingi na mali zake kutafuta watu wa kupambana na jide, angekubali walao mara fulani kwamba safari hii amekutana na kisiki.
 
Back
Top Bottom