Kama ningekuwa Rais...

Alaik

Member
Jul 30, 2012
61
119
Wakuu habari za jioni! Poleni na mihangaiko ya siku,

Niende moja kwa moja kwenye mada! Kuna vitu nafikiri ningevifanya kama Rais, naomba nieleweke pia kuwa Rais ninayemzungumzia sio mtu ni Taasisi. Kwenye hii Taasisi mtu ni sehemu ya muhimili na sio yeye ndio kila kitu.

Mambo yafuatayo ningeyafanya kama kiongozi na sio mtawala;

1: Kuimarisha au kutengeneza Taasisi za Umma.
Hapa nazungumzia mifumo huru ya kiutendaji na kimaamuzi itakayoweza kukiendesha yenyewe, yenye maono na malengo yake yanayojitosheleza. Hii ni pamoja na kupunguza madaraka yangu ya Rais kwa viongozi wa Taasisi hizi ili kuleta uwajibikaji na Uhuru wa maamuzi.

Hili limesahaulika sana ndio maana kuna maneno kama " maagizo kutoka juu". Hii inatuonyesha kuwa Taasisi hakuna au zipo lakini haziko huru kabisa zinapokea maagizo bila kuhoji au kupima hasara na faida kwa Taifa.

Vyombo kama usalama, Jeshi, Polisi na Tume ya Uchaguzi ni muhimu sana viwe huru visiingiliwe kiutendaji au kimaamuzi. Tunataka bluu iitwe bluu na sio njano.

2: Kurekebisha Katiba.

Pasipo kuangalia maslahi yangu au chama changu bali kuangalia maslahi ya Taifa naamini Katiba ikiwekwa imara itasaidia vizazi vijavyo katika kufaidi maslahi mapana ya Taifa hili.

Wengine hawaoni umuhimu wake kwakuwa hawataki kufikiri zaidi ya miaka 20/50/100 ijayo. Huwezi kuona umuhimu wake kama hicho chenye kasoro ndicho kinakulisha na kukuweka mjini utakionaje kinakasoro? Tunahitaji viongozi watakaoona thamani ya maendeleo ya Taifa na sio vyama vyao.

Tukiweka mfumo mzuri utakaodumu kwa miaka zaidi ya 50, utaozungumza juu ya sifa, ukomo, adhabu/ uwajibikaji wa viongozi kwenye Taasisi za Umma! Mfumo utakaotoa fursa za ushindani badala ya kusubiri teuzi ili kumpendezesha aliyekuteua.

Katiba na sheria zitazoeleza kwa uwazi uendeshaji na manufaa ya rasilimali za Taifa. Katiba itakayopunguza madaraka ya Rais na kuongeza nguvu ya Bunge na Mahakama viwe vyombo huru kimaamuzi na kiuendeshaji.

3: Kukubali kuwajibika au kumuwajibisha mteule wangu.

Hii nadhani imeeleweka vizuri sana! Kiongozi lazima ukubali kuwajibika pale unaposhindwa kutimiza wajibu wako. Pia kama Rais unayonguvu na mamlaka ya kumuwajibisha yeyoto uliyemteua kama atakiuka taratibu au maadili ya kazi yake tunataka kuona viongozi wanokubali kukosea na kushaurika.

Inakusaidia nini kununua watu au kura ili uwe kiongozi? Labda kama unataka kuwa mtawala na sio kiongozi! Uongozi nikutatua changamoto au matatizo ya watu, jamii na Taifa kwa ujumla.

4: Uongozi Shirikishi na Uwazi

Rais unaogopa nini kukusolewa au kushauriwa hadharani? Uwazi na ushirikishwaji wa vyama vya upinzani na wadau wa maendeleo ndio mfumo unaoleta uwazi na uwajibikaji.

Kama ni kwa manufaa ya Taifa ni shida gani unapata kusimamia uwazi na ukweli pamoja na uhuru wa vyombo vya habari?.

Nisiwachoshe ningali ninayomengi ya kusema. Wacha niweke kalamu chini nitaendelea wakati mwingine.
 
Hapo namba 2 sikubaliani nawe.Hatuhitaji marekebisho ya Katiba.Tunataka KATIBA MPYA.Tena itokane na Wenyenchi (wananchi) na SIO wanasiasa.
 
5. Kuwalazimisha chadema wakarabati makao yao makuu. Haiwezekani chama kinachukua ruzuku ya mamilioni halafu hata kupaka rangi tu jengo lao wanasua sua miaka nenda rudi. Huu ni ufujaji wa ruzuku.
 
Mfumo uliopo sasa hivi ni tosha kabisa,hakuna haja yoyote ya marekebisho ya aina yoyote ile.
Kama kila mwananchi kwa Imani yake atafanya ibada kwa dhati kwa alivyo amrisha Mwenyezimungu tutakwenda vizuri.
Tutakapokufa tutajuwa nini tulitakiwa tufanye kwenye uhai wa duniani na tutakuwa tumechelewa saana.
 
Back
Top Bottom