Kama ningekuwa rais wa Tanzania

Asante kwa hayo yote, hakika yamekaa vyema. Je, unaweza kuniambia utamfanyaje utakayembaini ana vyeti vya kuazima?
 
Hoja muhimu kwa hili taifa letu lazima tuwe na equal distribution of resources mikoa yote kwa kuiendeleza Tanzania, kujenga miundo mbinu rafiki nchi mzima, serikali sasa kujenga miundo mbinu kwa ajili ya kilimo cha kisasa cha umwagiliaji na itoe ruzuku kwa wakulima, pia ili kilimo kiwe na manufaa kwa wakulima serikali ingewaondoa madalali wanaowadhulumu wa kulima, pia kujenga viwanda vidogo vidogo vya kusindika, na kuwapa wananchi ujanja wa kutoa na kuuza mazao nje bila kulanguliwa hii ingepunguza umaskini kwa sababu 80% ya Watanzania wanategemea kilimo.
Swala la ajira na viwanda, ni tatizo graduates wengi wanasomeshwa then wanabaki tu mitaani bila kuwa na cha kufanya, inabidi elimu yetu sasa itoke kwenye Ku karirishana na kuwa na GPA kubwa ijikite na kutoa graduate wenye kuwa na muono wa Ku solve matatizo ya jamii at the same time, kupitia hyo solving problems watu mie ujasiriamali kujikwamua, pia serikali ingetenga ka budget kuwawezesha hao wenye mawazo bunifu ya Ku solve matatizo.
 
Umofia.......,wale wasomaji fasihi simulizi au wale wa miaka yetu O-level 002/5watakuwa wanaijua salam hii na tayar wameitikia Kwenuuu!!

Nilikaa mida flani leo nikawa nawaza baadhi ya mambo nikaona sio vibaya kama nitabandika hapa.

Nilikuwa nikiwaza IKIWA IMETOKEA NIMEKUWA RAIS WA NCHI YETU PENDWA YA TANZANIA ningefanya nini....? Nikajikuta nawaza ka ifuatavyo hapa chini..

KATIKA KUKUZA UCHUMI/. MAENDELEO
Ningepanua wigo kwa mikoa yote kuweza kuwa na level za kiuchumi zinazoshabiiana.Kwa ile mikoa inayoonekana kama mikoa masikini ama iliyosahaulika kama Singida,Lindi,Rukwa,Kigoma ,Shinyanga n.k.ningepeleka mikoa hiyo baadhi ya ofisi muhimu za serikali kupunguza mrundikano wa office Jijini Dar.

Ningewatumia wawekezaji wa humu nchini au wa nje ya nchi kujenga vyuo vikuu katika mikoa hiyo ili ifikike kirahisi.Makao makuu ya baadhi ya mabenki na taasisi kubwa yangekuwa mikoani na sio Dar kama ilivyo sasa.

Mikoa yenye utajiri wa madini mfano Almasi,Dhahabu n.k wawekezaji katika makubaliano ya mkataba wangelazimika kujenga shule,vyuo na Mahospitali ili ku-busti maendeleo kwa haraka.

Ningejenga viwanja vya soka vya kimataifa mikoani.Hii ingesaidia kushawishi wafanya biashara kuwekeza.Madangulo bubu ningeyapa vibali na kuamrisha yaboreshwe na wahusika walipe kodi serikalini ikiwa ni pamoja na kuwapima HIV wale wanaoajiriwa.

KATIKA ELIMU
Ningeufumua mfumo mzima wa elimu yetu na kuupanga upya.Ningepunguza masomo katika level husika na kuacha yale ya muhimu.Kwa mfano hakuna umuhimu kwa mwanafunzi wa sayansi kufanya mtihani wa Taifa wa kiswahili ama histori.Mitihani ya kumaliza shule ingefanyika kikanda yaani mfano,kanda ya na kanda ya kati wangefanya mitihani tofauti.

Ningefuta kidato cha tano na sita ama ningepunguza miaka ya O-Level kuwa miwili.Ningepunguza miaka ya masomo ya Madarasa kutoka saba na kuwa minne ama mitano.

Wanafunzi ambao wangeferi sekondari ningeamuru waende vyuo vya ufundi(VETA).Ningetenga shule maalum katika fani mbalimbali mfano shule ya madaktari,mainjinia,Shule za walimu,shule za biashara.Hapa namaanisha kuanzia kidato cha 3 mwanafunzi anaanza kulelewa katika fani yake.

Walimu wenye shahada wangefundisha O-Level lakini pia Division 1,2 &3 ndizo zingekuwa sifa ya kuwa mwalimu.

Wanafunzi na Walimu wangekuwa na magari yao maalumu ya kuwafuta na kiwarudisha kwa wakati.Ningeboresha mishahara ya walimu na kufanya ualimu kuwa moja ya kazi zinazopendwa/Zinazokimbiliwa.

KATIKA KILIMO
Vijijini kungekuwa na mashamba na maghala maalumu kwa ajili ya kuhifadhi chakula cha kijiji.Tractor walau moja kwa kila kijiji,mtaalamu wa kilimo kila kijiji.

Maduka makubwa ya pembejeo yasingekuwa Dar kama ilivo sasa badala yake maduka hayo yangejengwa vijijini tena karibu na mashamba.Mazao ya shambani kama korosho,karafuu ,Pamba n.k yangenunuliwa kwanza na serikali kisha serikali ndo iyauze nje ya nchi.Barabara nzuri za lami ningejenga vijijini zaidi kuliko mijini.

KATIKA ADMINISTRATION
Ningefuta wadhifa wa Unaibu waziri,mawaziri vivuli,Wabunge wa kuteuliwa na Wakuu wa wilaya na mikoa badala yake wabaki wakurugenzi wa mikoa(sio wilaya).

Ningeleta huduma muhimu wilayani na vijijini zisiwe za kusubiri zitoke Dar.
Ningeshauri katiba ibadilishwe na kufuta baadhi ya nyazifa mfano Makamo wa Rais.

Hayo nii baadhi tu ya yale mengi

Je KAMA WEWE UNGEKUWA RAIS UNGEFANYA NINI?

..........Free Ideas..........
Sio mabaya mawazo yako
 
Hoja muhimu kwa hili taifa letu lazima tuwe na equal distribution of resources mikoa yote kwa kuiendeleza Tanzania, kujenga miundo mbinu rafiki nchi mzima, serikali sasa kujenga miundo mbinu kwa ajili ya kilimo cha kisasa cha umwagiliaji na itoe ruzuku kwa wakulima, pia ili kilimo kiwe na manufaa kwa wakulima serikali ingewaondoa madalali wanaowadhulumu wa kulima, pia kujenga viwanda vidogo vidogo vya kusindika, na kuwapa wananchi ujanja wa kutoa na kuuza mazao nje bila kulanguliwa hii ingepunguza umaskini kwa sababu 80% ya Watanzania wanategemea kilimo.
Swala la ajira na viwanda, ni tatizo graduates wengi wanasomeshwa then wanabaki tu mitaani bila kuwa na cha kufanya, inabidi elimu yetu sasa itoke kwenye Ku karirishana na kuwa na GPA kubwa ijikite na kutoa graduate wenye kuwa na muono wa Ku solve matatizo ya jamii at the same time, kupitia hyo solving problems watu mie ujasiriamali kujikwamua, pia serikali ingetenga ka budget kuwawezesha hao wenye mawazo bunifu ya Ku solve matatizo.
Perfect
 
Back
Top Bottom