Nikiwa Rais

Google Diggers

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
940
1,123
Moja ya mambo nitakayoangalia kwa umakini mkubwa ni mitandao hii yaani inaweza ukakutoa kwenye reli kabisa.

Many social media edicted monsters speak nonsense, allogancy, stupid, fallacy and impossibly views.

Wakati mwingine nasoma mambo heading tu inanitosha kutosoma thread. What's is wrong with you empty headed mnajaza thread tu humu.

Mzee marehem magu alikuwa anapaniki Kwa sabb tu ya haya mamitandao.

Siku Moja alipaniki jukwaan akimwabia mama mmoja, baada ya kumuuliza Jina akijib yeye sijui ni mrema akasema wewe tena mchaga, kuhusu toilet ukanyee kwenu
 
Ningekuwa mzalendo kumzidi Jembe.

Watoto wangu wote wangesoma shule ya serikali ya "kata" kuanzia msingi mpaka chuo kikuu.

Watumishi wote wa umma kuanzia Makamu wangu na wengine wote ingekuwa lazima kusomesha watoto wao katika shule za Serikali.

Yes!!. Mimi ndio ningekuwa mhimili uliojichimbia chini zaidi, then bila shaka ningekuwa mwenyekiti wa chama.

Ningetoa maelekezo kwa wabunge pia, ningewaambia wasomeshe watoto wao shule za kata ili wanisaidie kutambua changamoto za elimu katika majimbo yao "kwa ukaribu zaidi".

Ningewataka wabunge waibane Serikali yangu kuhalikisha huduma zote za kitaaluma na miundombinu vinapatikana kwa kiwango cha juu.

Mbunge ambae angekaidi wakati mimi ni mwenyekiti angepoteza uanachama na mnajua ukipoteza uanachama nini kinafuata kama wewe ni mbunge kulingana na Katiba.

Hayo yote ningeweza kuyafanya kirahisi sana kwa nguvu ambayo ningeipata kupitia Katiba yangu hii sababu hakuna ambae angenibishia na wangenipigia meza pale mjengoni mbaka viganja vingekuwa vyekundu.

Sheria ingepita nakuanzia hapo shule za kata zingekuwa kama za wamisionari.

Usiseme isingewezekana, ingekua amri.
Halafu mngeita mpango wangu huo jina lolote kama udikteta nk.

Maendeleo yasingekuwa na chama.
 
Wabunge na wakuu wote wa serikali chama na taasisi zake..mishahara yao ijulikane na ikatwe kodi.

Pia teuzi zote lazima kuwe na usaili.

#MaendeleoHayanaChama
 
Yes, hapo ndio angalau kungekuwa na usawa wanao uhubiri kilasiku.
 
Nasema kama ningekuwa Rais, kipaumbele changu namba moja ingekuwa kilimo, katika utawala ningehakikisha hakuna kijana asiye na angalau hekari 2 za kilimo. Nisingejenga daraja la Salendar badala yake ningeagiza matrekta kwa wingi niyagawe kwenye vijiji vya kimkakati.

Ningehakikisha kila kijiji kinakuwa angalau na trekta tano ambazo watazitumia kwa ujamaa, kulima mapori yote yasiyo ya hifadhi na yamekaa tu ningetangaza mtu yeyote anaetaka kulima apewe bure, kwa ajili ya kilimo tu.

Viongozi wote wa serikali kuu kila mmoja angejinunulia gari lake kutoka na mshahara anaopata. Hata hawa mawaziri, serikali yangu ingewapatia magari ya bei nafuu, pesa yote ningeipeleka kuhudumia kilimo.

Kwa mfano kuwatafutia mbegu bora na mbolea ya mkopo kwa kila mkulima, wavuvi wangepewa zana bure na boti ndogondogo zitakazo wasaidia kuendesha uvuvi bila misukosuko mikubwa.

Ningejenga viwanda vikubwa vya kuchakata minofu ya samaki na kusafirisha samaki nje ya nchi. Ningekuwa Rais maeneo yote ya bonde la Ruvu ningehakikisha nafungua mashamba makubwa ya miwa pamoja na kubuni maeneo mengine mapya yanayostawisha miwa kama Tanga, Kagera, na Mbeya ili sukari iwe kutosha muda wote. Vijana wengi wangepata ajira na wangelima bila shida.

Ningekuwa Rais reli ya standard gaurge ningeijenga mwisho Dodoma, pesa nyingine yote ningejenga mahospitali makubwa kila wilaya, ningekuwa Rais cheo cha Mkuu wa Wilaya ningekiondoa abaki Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi na RAS.

Ningekuwa Rais ningepunguza misafara kwenye ziara za viongozi badala ya gari kumi na kubaki na mbili tu Ili kupunguza gharama ya mafuta, ningekuwa Rais nisingetoa ajira zinazojirudia kwa watu wale wale na jamii ile ile au koo zile zile.

Ningekuwa Rais ningeondoa nafasi ya Makamu wa Rais ningebaki na Waziri Mkuu tu. Kama ningekuwa Rais wahitimu wote wa JKT wangejiunga na jeshi kwa hiari.

Mwisho ningekuwa Rais ningepunguza mishahara ya wabunge na kuelekeza pesa hizo kwenye huduma ya jamii, ningekuwa Rais wajumbe wa nyumba kumi wangepewa mshahara hata laki moja kwa mwezi na halmashauri zao.
 
Yale yale ya Magu yeye maono yake ilikuwa kuua upinzani na kutukana mabeberu tu.
Na bado hatujifunzi tu.
Uongozi si sehemu ya kujikweza au kutafuta sifa na utukufu kwa kushinikiza mabadiliko ya dharura kwenye maisha ya wananchi!

Maendeleo ni mchakato wa kitaalamu! Unapaswa kuwa jumuishi na wenye hatua bayana ili kuwezesha uperembuaji!

Je, malengo mkakati ya taifa (Vision 2025) yanasemaje...?
Je, ilani ya uchaguzi inahakisi Vision 2025?

Je, kiongozi anajua hivyo?
Je, wananchi wanajua hivyo?

Maendeleo yanayokuja nje ya Vision 2025 yanaleta contradictions safarini.
In short kiongozi mzuri ni yule wa kutekeleza malengo mikakati ya taifa!
 
Kama ningekuwa rais kipaumbele changu namba moja ingekuwa upatikanaji wa nishati kwa kiasi kikubwa majumbani na viwandani na kwa bei nafuu. Ili kitu chochote kifanye kazi kinahitaji nishati.

Afya na Elimu
Kilimo ndo vipaumbele ambavyo vingefatia japo ni muhimu sana na penyewe.
 
Back
Top Bottom