Kama ningekuwa na simu…………………

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,395
Inaelezwa kwamba wanawake wa mjini ambao hawana simu, wanapoanzisha uhusiano na mwanaume ambaye ana simu, kauli ya, ‘kama ningekuwa na simu ingekuwa vizuri sana,’ hujitokeza.

Kuna idadi kubwa ya wanaume ambao wamewanunulia mahawara simu za mkononi, lakini wamekuwa wakilalamika kwamba, simu hizo zimekuwa zikitumika kuwapigia wanaume wengine.

Hii ni kwa sababu baada ya kupata simu, mwanamke hupunguza mawasiliano na hawara kwa sababu, huenda anakuwa amepata alichokuwa anatafuta. Kwa kuwa kuna yule anayempenda kwa dhati, ndiye ambaye atakuwa anawasiliana naye zaidi na wakati mwingine hata kumpa simu hiyo.

 
ni aina mojawapo ya kuhongwa .... kawaida mawasiliano ya simu kati ya mwanamke na mwanaume huwa hayadumu sana kwani kikishapatikana kilicholengwa basi mawasiliano yanalegalega
 
hivi kuna wanaosema sina simu mpaka sasa...coz hadi mtoto wa primary ana simu
 
Back
Top Bottom