Kama ningekuwa kova ningewapanga polisi wa doria hivi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama ningekuwa kova ningewapanga polisi wa doria hivi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KAPECHA, Apr 24, 2009.

 1. K

  KAPECHA Member

  #1
  Apr 24, 2009
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  habari za uchovu wa kupigania shillingi wadanganyika wenzangu. hivi uozo huu utaisha lini wa mtu kusafiri kilo mita 100 kufuata huduma ya afya, maji ya visima , na umeme wa kibatari, ukiwauliza wanajibu enzi za mwalimu nilikuwa nakaa bunju lakini nasoma pugu na ili nibidi nitembee kwa miguu wakati wote.

  Sasa ni rudi kwa kamanda wa polisi wa jiji sugu la dar es laaam jinsi ya kuweza kuwapanga askari wake katika operation za ania mbali mbali . ndugu kuna askari wa doria ambao nitawapanga katika magroup yafuatayo
  1: askari wa miguu wenye bunduki ambao huwa watatu au wawili.
  2: askari kanzu wa miguu ambao huwa na bastola na huwa watatu au zaidi
  3: askari wa defender au TZ R ambao huwa watano mpaka nane kwa gari moja
  4: askari wa gari aina ya saloon zile gari zenye rangi mbili ambao kuwa wanne kwa gari moja
  5: askari maalumu kwa kazi maalumu ambao huwa na gari vile vile lakini hupaki vituoni kusubiri amri.

  Naanza kupanga kazi askari group namba moja ambao hawa wana takiwa wasimame kwenye makutano ya barabara zifuatazo.

  a: uhuru /msimbazi

  b: msimbazi/mogorogoro

  c:morogoro / united nation( fire)

  d: morogoro /bibi titi ( akiba)

  e:morogoro/kawawa( magomeni)

  f:morogoro / nyerere( ubungo)

  g: morogoro/shekilango( sinza)

  h; morogoro/ mabibo( big brother)
  i: mazese darajani
  j: mwembe chai
  k: mnazi mmoja
  l: nyerere/nkuruma
  m:nyerere na msimbazi
  n: round about BP
  o:nyerere/shauri moyo
  p:nyerere/kawawa/changombe
  q:tazara(nyerere/ mandela)
  r:vertinary
  s:nyerere na changombe
  t:nyerere/taifa
  u: nyerere na kilwa
  v: mtongani kwa azizi ally
  w: mtoni mtongani stend
  x: round about ya bp na kuelekea bandarini
  y:mwenge
  z: sayansi
  jamani nimeishiwa herufi nina maana sehemu zote zenye makutano ya barabara hawa polisi wawekwe kusubiri kupewa amri kwani huwa wanakuwa na simu za upepo.

  group la pili lipangwe kila njia yaani wawe wanatembea barabarabi tu kutoka point a kwenda b mfano

  a: kutoka tazara mpaka makutano ya changombe /nyerere ndio eneo lao au

  b: kutoka nyerere /changombe mpaka kwa kandoro na wengine wataanzia kutoka kwa kandoro mpaka mbuyuni pale kigogo na wengine kigogo mpaka magomeni na kuendelea.

  askari wa magroup mengine nao watajigawa hivyo hivyo.

  hivyo basi utakuta ruti moja ina askari wa aina tano hivyo mfano ukitokea wizi pale maeneo ya ddc klabu majambazi yanapola na kurusha risasi juu. wahusika wakipiga simu central polisi , central polisi itawapigia askari wake wa doria wanao zunguka eneo la tukio hivyo maaskari wote walio mnazi. bp fire, msimbazi round about. kigogo, kwa kandoro wanaweza kulifikia tukio likiwa bdo la moto kwa hesabu za haraka ni askari kama hamsini wanaweza kuliwahi tukio hilo.

  Kama mzee utaona njia hii ni too local basi tufanye kama wenzetu wa majuu na nina uwezo wa kukusaidia kudesign na kukufungia kamera nizazozunguka degree 360 na hazionekani na huweza kusense vitu kama mirio ya bunduki , movement za watu ambazo sio za kawaida ,

  Ngoja niishie hapa ili nikaiwahi familia yangu home mwenye macho na asikie

  ni mimi sungura mjanja

  IT IS BETTER TO TRY THAN TO FAIL TO TRY
   
Loading...