Kama nia ni kupambana na ugaidi, kwanini watuhumiwa wa Uamsho wako nje kisha anashikiliwa Mbowe?

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,592
11,831
Jana Samia Suluhu ambaye nadhani ndie Rais wa Tanzania japo hakidhi vigezo vya kuwa Rais wa nchi yoyote ile alisema kuwa kwasasa dunia inakabiliwa na tatizo jipya la ugaidi. Yeye kwa maoni yake ugaidi ni tatizo jipya.

Kama kweli ameweka nia ya kupambana na magaidi ni kwanini watuhumiwa wa uamsho wameachiwa huru. walio hamasisha fujo hadharani na kusababisha mauji ya watu wasio na hatia, kujeruhi na upotevu wa mali za watu.

Kisha unamshikilia Mbowe ambaye kesi yake inatia ukakasi japo simtetei Mbowe sababu yeye sio malaika yawezekana kweli anahusika.

Uamsho aliwaachia kwasababu
1. Waislamu wenzake?
2. Wazanzibar wenzake?
3. Walionewa tu na kina JK?

Kwa walioyafanya hadharani mchana kweupe kisha wakachiwa huru kwanini sasa Mbowe awe gaidi?

Hawa wanaosema ni chuki za kisiasa na udini na Uzanzibar na Uzanzibar bara ndio ugaidi wa Mbowe wanaweza kuwa sahihi kutokana na vitendo vya Samia mwenyewe.

NB. Miaka ya hivi karibuni vikundi vya utishio wa kigaidi umekuja kwa kasi sana hapa nchini na hatujui hasa vinafadhiliwa nani ni uimara tu wa jeshi ndio umetuweka salama hadi sasa.
 
Kwani definition ya ugaidi ni nini? Au ndo umekaririshwa kuwa gaidi lazima awe shekhe na si mwanasisa!,, yani mpaka leo bado unateseka tu na wale masheikh!,, ujui ya kuwa wale walisota rumande zaidi ya miaka saba na ushahidi ulishwandwa kupatikana na ndio sababu wakaachiwa,, so hata na huyo mbowe nae serikali ikishindwa kuthibitisha ugaidi wake nae ataachiwa,, kinachokusumbua hapa ww ni itikadi yako ya kisisa na udini uliokujaa futsek!!
 
Pointi ya jamaa ni kuwa wale mashekhe matukio yalionekana waziwazi kama vile kuchoma majengo na kumwagia watu tindikali
Ila ya Mbowe hakuna lolote lililotokea na so far ushahidi uliotolewa hakuna unaoonyesha chochote kuhusu huo ugaidi
 
Kwa hiyo kama matukio yalionekana wazi wazi ya kuchoma makanisa we una ushahidi gani kama hao walitumwa na mashekhe kufanya uo uhalifu,, au ni kila tukio la kihalifu linalohusisha kanisa basi lazima wahusishwe mashekhe? Na si walipelekwa mahakamani na mbona hamkwenda kupeleka ushahidi, na mimi point yangu usiwahusishe mashekhe na kesi ya mbowe kwa kuwa mashekhe walishinda kesi,, na mbowe yake bado iko mahakamani
 
Ugaidi wa mbowe upo ktk kuhatarisha maslahi na hatima za madaraka yetu, ni Bora angelipua bunge likiwa tupu tungeweza msamehe kuliko huu ugaidi wa kuhamasisha watz wadai katiba mpya.
Mbaya zaidi anatumika Bastola yenye risasi 3 kukatia miti mikubwa ili gali zishindwe kupita.
 
Kwani definition ya ugaidi ni nini? Au ndo umekaririshwa kuwa gaidi lazima awe shekhe na si mwanasisa!,, yani mpaka leo bado unateseka tu na wale masheikh!,, ujui ya kuwa wale walisota rumande zaidi ya miaka saba na ushahidi ulishwandwa kupatikana na ndio sababu wakaachiwa,, so hata na huyo mbowe nae serikali ikishindwa kuthibitisha ugaidi wake nae ataachiwa,, kinachokusumbua hapa ww ni itikadi yako ya kisisa na udini uliokujaa futsek!!
Kabla hujaanza kusema nateswa na udini ungeuliza Kwanza mimi dini gani.

Kilichotokea Zanzibar nyakati za uamsho kilivuta macho na masikio ya wengi nchini na nje ya nchi mana kwa wiki kadhaa Zanzibar ilikuwa si sehemu salama.
Kama yalifanyika makosa ya kukamata hao unao waita mashekhe kwa chuki za kidini tu ama kuwaangushia jumba bovu basi ni vipi kuhusu huyu Mbowe haiwezekani ikawa ni chuki tu ya kisiasa?.
kama wale ambao matukio yao yalionekana dhahiri mchana kweupe wemeachwa huru huyu je ambaye hata harufu ya tukio lake la ugaidi hakuna?

Uamsho hawakukamatwa kwasababu ni mashekhe bali kwasababu ni watuhumiwa wa ugaidi.

Kama unadhani walikamatwa kwasababu ya ushekhe wao pamoja na matukio yote yale je vipi kuhusu Mbowe naye amekamatwa kwasababu ni chadema ?
mana hakuna hata tukio moja ambalo angalau laweza tumika kumhusisha na ugaidi.
 
Jana Samia Suluhu ambaye nadhani ndie Rais wa Tanzania japo hakidhi vigezo vya kuwa Rais wa nchi yoyote ile alisema kuwa kwasasa dunia inakabiliwa na tatizo jipya la ugaidi. Yeye kwa maoni yake ugaidi ni tatizo jipya.

Kama kweli ameweka nia ya kupambana na magaidi ni kwanini watuhumiwa wa uamsho wameachiwa huru. walio hamasisha fujo hadharani na kusababisha mauji ya watu wasio na hatia, kujeruhi na upotevu wa mali za watu.

Kisha unamshikilia Mbowe ambaye kesi yake inatia ukakasi japo simtetei Mbowe sababu yeye sio malaika yawezekana kweli anahusika.

Uamsho aliwaachia kwasababu
1. Waislamu wenzake?
2. Wazanzibar wenzake?
3. Walionewa tu na kina JK?

Kwa walioyafanya hadharani mchana kweupe kisha wakachiwa huru kwanini sasa Mbowe awe gaidi?

Hawa wanaosema ni chuki za kisiasa na udini na Uzanzibar na Uzanzibar bara ndio ugaidi wa Mbowe wanaweza kuwa sahihi kutokana na vitendo vya Samia mwenyewe.

NB. Miaka ya hivi karibuni vikundi vya utishio wa kigaidi umekuja kwa kasi sana hapa nchini na hatujui hasa vinafadhiliwa nani ni uimara tu wa jeshi ndio umetuweka salama hadi sasa.
Samahani mkuu kabla hujaandika haya yote ulishirikisha halmashauri yako ya kichwa au yamekutoka tu??? Nadhani ulikuwa na hoja nzuri tu ila jazba na mhemko vimevuruga kila kitu.
Kama ambavyo Masheikh wa uamsho hawakuwa magaidi ndivyo Mbowe asivyo gaidi.
Ila kama unataka kutuaminisha waislamu na masheikh ndio magaidi hapo nitakuelewa
 
Ndivyo ulivyo nielewa?
 
Mmoja wa mashekhe wa Uamsho ana uhusiano wa kidugu na jumong.

Huyu mchaga hajulikani hata na majirani wa jumong.

Kumbuka damu ni nzito kuliko maji.
 
Mashekh hawajawahi kupelekwa mahakamani zaidi ya kushikiliwa.
iyo kama matukio yalionekana wazi wazi ya kuchoma makanisa we una ushahidi gani kama hao walitumwa na mashekhe kufanya uo uhalifu,, au ni kila tukio la kihalifu linalohusisha kanisa basi lazima wahusishwe mashekhe? Na si walipelekwa mahakamani na mbona hamkwenda kupeleka ushahidi, na mimi point yangu usiwahusishe mashekhe na kesi ya mbowe kwa kuwa mashekhe walishinda kesi,, na mbowe yake bado iko mahakamani
 
Back
Top Bottom