Kama ni viwanda tuwekeze zaidi kwenye chuma na makaa

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,298
12,600
Kama viwanda vyetu havitaji chuma chetu na makaa yetu tumekosea Sana.

Hatuwezi kujivunia kuwa na viwanda vingi vya kutengeneza pampas na kuucha mhimili mkubwa wa viwanda duniani wa chuma na makaa ya mawe.

Tuchimbe chuma tukiyeyushe na kupata mazao yake Kwa viwanda vyetu na ziada kuuza nje. Sisi ni makosa kufikia kujenga viwanda kabla ya kufikiria kilimo kikubwa cha kulisha watu wetu na Africa, dunia. Ni makosa makubwa kuwapa wananchi wasiokiww na mitaji na ujuzi ardhi ya mashamba ya Mkonge, Nafco, mpira, cocoa badala ya kuwapa wawekezaji wakubwa kama jkt, magereza, na matajiri wanaoweza kuyatumia Kwa uzalishaji mkubwa wenye tija.

Liganga na mchuchuma ndicho kingekuwa kituvu cha mapinduzi ya kilimo Tanzania Kwa kuzaliza bidhaa kama matrector ya kilimo, malori ya kusafirisha mazao hayo. Afrika ina njaa na dunia pia, kilimo ndiyo bidhaa yetu ambayo masoko yake yako njenje kuliko pampas, tiles, sabuni, na bidhaa nyingi za viwanda.

Haya shime tuelekeze bajeti zetu liganga, mchuchuma na songwe kama tunataka ahueni.
 
Back
Top Bottom