Kama ni tuzo ya PhD ya heshima katika miaka 50 ya uhuru nani anastahili kupewa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama ni tuzo ya PhD ya heshima katika miaka 50 ya uhuru nani anastahili kupewa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nderingosha, Oct 7, 2011.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,525
  Likes Received: 1,312
  Trophy Points: 280
  Wana JF nimesikitishwa na taarifa(fununu)kuwa eti mijamaa pale UDSM wamepanga kumtunuku JK tuzo ya PhD ya heshina katika miaka 50 ya uhuru!!
  Kama ni honorary PhD wako candidates wengi TZ.......na si JK. Huyu bwana sijui anawafanya nini watanzania mpaka wanampapatikia namna hii jamani.Sipati picha nchi hii iko kwenye matatizo chungu mzima tangu huyu bwana amechukua nchi alafu kila kukicha kuna mijamaa wanajipanga kumpa tuzo huyu mswahili,haiingii akilini yaani...huyu bwana hata kwenye list ya potential candidates hafai kuonekana si tu kufikiriwa.Najua siasa zimeingia sana kwenye vyuo vyetu siku hizi na mijamaa wengi maprofessor yameingia kwenye ushabiki wa kisiasa siku hizi....hili ni janga tena kubwa sana kwa taifa.Kuona mi professor badala ya kufanya research wameingia kushabikia siasa za maji taka na sasa wanataka kumpa tuzo mjinga ili tu kulipa fadhila au kupandishwa vyeo(Mukandara type)......badala ya kufanya research za kumkomboa mtanzania mijamaa wanafanya siasa za chooni, kama kuna mmoja anaboa sana na comments zake (somebody Bana!!) zinazomfagilia kila leo JK na siasa za maji taka za chama chake cha CCM.Mi si mshabiki wa chama lakini i get pissed off napoona mpaka mi professor inatoa so biased comments on status quo ya Tz politics. Ndio sababu misomi yenye hadi PhD siku hizi inakimbilia kwenye siasa za maji taka ili wapate ubunge....wamesahau hata waliyosomea vyuoni......na mbaya zaidi misomi hii hii yenye ajira serikalini ndio kwa kushirikiana na siasa za maji taka za chama tawala wamelifikisha taifa hapa lilipo kwa kujali tu vitambi vyao na 10% za mikataba feki.I wish tz tungekuwa na mtu kama president Sata wa Zambia ambaye ameamua kukamua uchuro wote mwanzo mwisho baada tu ya kuapishwa. Katika kusherekea miaka 50 ya uhuru wa nchi hii watu wachache sana wanaweza kuwa kwenye list (lakini si JK please!)...miongoni mwao ni kama wafuatao...(proposed)...
  • Baba wa Taifa-Julius.K.Nyerere
  • Hayati Edward M.Sokoine
  • Dr.Salim Salim
  • Jaji Joseph Sinde Warioba
  • Dr.Asha Rose Migiro
  • Mzee Kawawa Rashid
  Hawa at least wametukuka (na wote wanaweza kupewa tuzo)........sioni zaidi TZ.....you can comment!!! viongozi waliopita kina Mkapa au Mwinyi au Dr.Shein wangeweza kuwemo lakini wachafu tayari (mfano Dr.Shein ni msafi lakini alikuwa kwenye awamu ya Mkapa ambako hakuweza kubadili mambo), mzee Karume hayumo kwasababu tunasherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania (na si Zanzibar)......Mama Prof.Tibaijuka angekuwemo lakini sasa anatumikia dola dhalimu hivyo tumpe mda kama ataweza kuleta tija..., mama Getrude Mongela angekuwemo lakini nae aliharibu kule Addis Ababa kabla hajatimuliwa. Hawa jamaa niliowataja ni wasafi kwa kweli na wazalendo wa kweli na si wanafiki kama kina JK....wanaojifanya hawajui eti dowans ni kina nani??kuna wengine wengi katika technocracy wanaofaa lakini nimeweka politicians kwani wao ndio wanaongoza sekta zote katika nchi.....if you have stupid and corrupt politicians you can consequently have corrupt technocrats.
   
 2. k

  kinyongarangi Member

  #2
  Oct 7, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  EDWARD LOWASA kwa kuanzisha shule nyingi za kata
   
 3. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Mama Maria Nyerere kwa kutofanya biashara akiwa ikulu
   
 4. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2011
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Apewe Dr. Willibrod Slaa aliyethubutu kuwataja mafisadi hadharani pale uwanja wa Mwembe Yanga.
   
 5. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  wampe Dr. Slaa, ndiye kiongozi aliyetukuka
   
 6. c

  chuwaalbert JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 3,049
  Likes Received: 1,436
  Trophy Points: 280
  Habari nilizonazo ni kuwa Bana hakusoma FORM SIX. Alifeli Form Four. Amefika University kwa KUUNGA. Alipitia mlango wa Diploma ya Adult Education!
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  apewe dr WILBROAD SLAA kwa kutufumbua macho watanzania wengi kuhusu ufisadi unaofanywa na KIKWETE NA WENZIE
   
 8. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Nipeni mimi na mke wangu, tutawazalia watoto ambao sio wezi!
   
 9. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  na pia kwa kutuibia watanzania
   
 10. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  walewale km mtoto wa mkulima kujidai kulialia kumbe anazuga wa2
   
 11. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  na pia kwa kutuibia watanzania
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  UGAWAJI OVYO PhD NCHINI KAMA VITUMBUA MWANANYAMALA HUENDA UKAKUMBANA NA COURT INJUNCTION HIVI KARIBUNI NA KUFEDHEHESHA ZAIDI WAHUSIKA WAKE

  Hakuna haja kaburi kupewa tuzo kama Chuo Cha Kata Dodoma kilivyofanya kwa Simba wa Vita Kawawa kuzawadiwa PhD pamoja na Kikwete.

  Kama ni LAZIMA SAAAAAAAAAAAAAAAAAANA kwamba UDSM nayo isibaki nyum katika hii fesheni mpya ya kugawa PhD bila kuipigania, sawa na VITUMBUA KULE MWANANYAMALA, basi tuzo hilo la PhD lastahili kumuendea mtu mmoja tu Tanzania hii.

  Na mtu huyo ni Mama Maria Kambarage Nyerere kwa mchango wake kumshauri vema Baba wa Taifa mpaka wakaweza kujenga misingi imara ya amani, utengamano, heshma kwa utu bila kudhalilishwa na ufisadi kama hivi leo, na KUFANIKIWA KUONDOAHARUFU ZA UKABILA, UDINI NA TABAKA ambazo hivi sasa tumekazania kuzirejesha kwa Ari kubwa zaidi, Nguvu kubwa zaidi na Kasi ya Kikwete hivi leo.

  Hadi hapo, endapo
  Prof Palamagamba Kabudi, Mkandara na yule mwingine sijui Bansen Burner - watakapojiruhusu japo kidooogo tu ili Uprofesa wao kweli usimame na Ukada wao kwa CCM tunayoizika hivi karibuni ulale basi watakubaliana na Wa-Tanzania wenye chuo chetu kwamba Kikwete hastahili hata cheti hapo kwa mujibu wa ufisadi na udini ulivyoachiwa ovyo nchini.

  Tunawajua sana mnaoshinikiza jambo hili kutokea na msije mkalalamika migomo na maandamano itakaposhika kasi juu ya hili.

  Laa sivyo, sitoshangaa sana kusoma humu kwamba Kikwete kuvuliwa PhD zote mahakamani alizoshinikiza kuzipata kupitia mlango wa nyuma. Nasema court injunction inanukia kwa zoezi hili na mpaka hapo ndipo sifa za mkabidhiwa na mtoa PhD vitumbua vitakapojulikana hatima yake katika vyombo vya nyumbani na vya kimataifa.
   
 13. d

  dotto JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Researcher: Foleni za magari dar > uchumi kukua; Mimba shuleni > Kiherehere; Kwa nini Tz ni maskini > hata mimi sijui; Kula > nawe uliwe; n.k. Kwa haya machache anasitahili PHD na sio PhD.
   
 14. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Sijaona, bado nchi iko kwenye hali mbaya sana.
   
 15. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Laiti ingewezekana ingestahili itolewe kwa watanzania masikini (kwa ujumla wao) kutokana na utulivu wao hata pale haki yao inapopokwa wazi wazi!
   
 16. p

  plawala JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuzo nyingi za JK toka vyuo vya ndani ni yeye mwenyewe anazipendekeza apewe kupitia kwa wapambe wake
  Na hawa wakuu wa vyuo wanakuwa hawana namna zaidi ya kupeleka kwa masenetors wao kwa ajili ya kujadiliwa
  Ikishafikia hatua hiyo inakuwa vigumu kukataliwa kwa sababu utaratibu unaotumika ni kupigwa kura,na kampeni zinapigwa kama kawa
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  QUOTE=dotto;2610212]Researcher: Foleni za magari dar > uchumi kukua; Mimba shuleni > Kiherehere; Kwa nini Tz ni maskini > hata mimi sijui; Kula > nawe uliwe; n.k. Kwa haya machache anasitahili PHD na sio PhD.[/QUOTE]
  Umesahau kwa nini hawa maiti wa mv spice islander wasipimwe DNA..hahaaaa jk mwanakwet.kaz
   
Loading...