Kama ni muhimu ule usiku, kula matunda. Kama huna matatizo ya kiafya usile itakusadia kupunguza uzito uliokithiri

sabuwanka

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
690
751
Wakuu salamu, nimendika sentensi hiyo hapo juu ambayo ni ushauri ulitolewa kwa mtu anayetaka kupunguza uzito, nimepitia thread moja humu mdau akieleza jinsi vyakula vya wali na ugali vinavyochangia kuongeza uzito hasa kwa wanaofanya kazi za maofisini, maana muda mwingi wanakuwa wamekaa na hata wakifanya mazoezi ya mwili bado hayana uhusiano wa moja kwa moja na kupungua uzito, pamoja na mazoezi ya mwili pia ushauri mwingine ni kupunguza/kuacha chakula Cha usiku kwa kuwa chakula tunachokula usiku hakina kazi kubwa na hivyo hutunzwa Kama mafuta katika sehemu za tumbo, mapaja , kiuno nk.

Kama umetumia mbinu nyingi umekwama kupunguza uzito...hii inaweza kukufaa ikiwa hauna kisukari!

Ikumbukwe kuwa janga la OBESITY ni janga la duniani, ndo maana makampuni yanayocheza na fursa yamekuja na madawa kwa ajili ya suluhisho...ingawa mchango wake sio mkubwa Kama unavyotangazwa

Uzito mkubwa na na kuwa na lehemu nyingi katika damu ni chanzo Cha magonjwa ya moyo, pamoja na kutokuwa na nguvu za kijinsia ......hii nayo imekuwa fursa ya kuja na kila lundo la dawa za nguvu za kiume bila kuangalia chanzo halisi Cha tatizo

Kwa yeyote mwenye mchango /uzoefu/maoni /mawazo kuhusu hii mada karibu
 
Bado hujakumbwa na jinamizi la uzito uliokithiri kulingana na BMI, endelea kuwa fiti kwa kufanya mazoezi ya mwili angalau mara 3 kwa wiki( mazoezi ya moyo/cardio/aerobics na ya nguvu ( strength/anaerobic)
 
Ingawa kwa siku za mwanzo utakuwa na mawenge wenge ya njaa...tumbo likizoea unaona kawaida
Hii ni nzuri, unalala ukiwa mwepesi, unapata usingizi mzuri sana, na unaamka asubuhi tumbo likiwa jepesi na mwili mwepesi.
 
Njia nzuri na nyepesi ambayo nafanya kaz haraka ni kuendesha baiskeli...asikwambie mtu ukiendesha baiskeli dakika 40 tu kwa siku matokeo utakayo yapata utakuja kunishukuru
 
Ingawa kwa siku za mwanzo utakuwa na mawenge wenge ya njaa...tumbo likizoea unaona kawaida
Nilishazoea kabisa. Naweza kunywa glass ya mtindi nikalala bila wasiwasi, asubuhi nikaamkia nusu lita ya maji ya uvuguvugu kisha mayai yangu matatu na mbogamboga. Wali, ugali nimeacha muda. Ni proteins, mbogamboga, na matunda yasiyo na sukari nyingi nakula kwa wingi.
 
Nilishazoea kabisa. Naweza kunywa glass ya mtindi nikalala bila wasiwasi, asubuhi nikaamkia nusu lita ya maji ya uvuguvugu kisha mayai yangu matatu na mbogamboga. Wali, ugali nimeacha muda. Ni proteins, mbogamboga, na matunda yasiyo na sukari nyingi nakula kwa wingi
Mabadiliko umeyaona? Na umefanya hivyo kwa muda gani?
 
Kula vyakula vya kujenga,kulinda na kuupa mwili nguvu yaani balance diet.

Kula milo mitatu kwa kihasi usile kama unahama na fanya mazoezi kila siku.

Mambo ya kutokula ni hatari siku ukija kupata ugonjwa utapukutika na kuwa kama namba moja.
 
Kula vyakula vya kujenga,kulinda na kuupa mwili nguvu yaani balance diet.

Kula milo mitatu kwa kihasi usile kama unahama na fanya mazoezi kila siku.

Mambo ya kutokula ni hatari siku ukija kupata ugonjwa utapukutika na kuwa kama namba moja.
Namba moja unamaanisha magufuli au unamaanisha nini ?
 
KWA nnavojua Mimi,
Ukitaka kupunguza uzito ulokithiri kwa haraka zaidi, Fanya yafuatayo:-

1. weka nyumba Bondi, Kisha Kakope pesa nyingi benki,
Afu pesa yote Kanunue shamba kando ya mto na uanze kulima tikiki na Ela itakayobaki uchimbe bwawa la ufugaji samaki.
Afu Mvua kubwa inyeshe, tikiki zote zioze , samaki wote wasombwe na maji waende mtoni.
Kisha benki waanze kufatilia Deni lao na hujui pa kupata pesa za kulipa.
Nna uhakika ndani ya mwezi, utapungua uzito.

2. Ingia kwenye mahusiano na MDANGAJI awe na gubu Sana. Afu umpende Sana kwa Moto wako wote.
Utapungua Sana uzito uto AMINI.
 
Back
Top Bottom