Kama ni MAJIPU Serikali za CCM zote zlizopita ni MIJIPU

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,745
Yupo atakaeweza kulipinga hili ? Na alipinge tuone ! haya yanayotokea sasa ya kutimuana ndani ya wiki na kila mmoja amekuwa shupavu kumpa aliyemkuta siku tatu au saba afanye hili au alifanyie kazi agizo fulani kulitimiza, huo ni uonevu .

Nilimsikia Rais Magufuli akisema amewateua na yeye pia ni mhusika kwa kuwaondolea uteuzi huo au kuwafukuza kazi.

Mheshimiwa baada ya kuingia madarakani tu alikuiingia kwa pupa na vishindo akiwa na ameshikilia bango la hapa kazi tu na baada ya wiki na punde akakoleza msemo wa kupasua majipu ,hapa tuliona wengi wakipoteza nafasi zao za kazi kiholela.

Katika serikali ya Mheshimiwa Magufuli zipo sura nyingi ambazo zilikuwemo katika serikali zilizopita akiwemo yeye mwenyewe na wapo waliowachwa nje wakineemeka na kile walichokichuma .

Hawa wanaoitwa MARAISI wastaafu ni lini watachunguzwa na wao waonekane ni wasafi ?? Mawaziri waliopita na waliostaafu nao ni lini kisu cha upasuaji kitawagusa au ndio Serikali ya Magufuli itatumia ule msemo wa mitaani ..ndio imetoka hio...!

Hasara iliyopata Taifa ambayo mheshimiwa Magufuli amekuwa akiitonya kila apatapo data haikuzuka pale tu Magufuli alipoanza kuiongoza nchi kama Raisi ni mambo yaliokuwa yamefanywa na awamu zilizopita kwa maana uoza alioukuta si wa awamu yake ni uoza uliokuwa na mizizi na mashina.ukichunguza yanamuhusisha baba mwana mtoto mjukuu.

Kuna WaTz wanatumika au wanaendelea kutumika kwa kuwa na mali zisizokuwa zao wao ni wawakilishi tu ila walioko nyuma ni wale wa awamu zilizopita ndio wamiliki halali ,kama litapita azimio la Arusha basi wengi wataumbuka maana mali wanazomiliki ni za kupinduki.

Je ni majipu ya aina gani anayoyatumbua Mheshimiwa Magufuli ? Serikali zilizopita zikiyalea majipu kwa faida yao na ndio tukaona viremwe wanamiliki kubwa na mirija yao inaendelea.

Mirija inahitaji kukatwa kwani serikali za CCM zilizopita zinatisha kwa mirija na zimejijengea himaya inayohitaji Mheshimiwa Magufuli avunje urafiki kwa wanachama wenzake ,awe ni kiongozi aliejitolea kwa hali na uhai katika kuipigania Tz ya wanyonge aweze kkuondoa matabaka ,watz watazidi kuwa na imani kuwa kweli wamepata kiongozi anejali si maisha na hali za Watz walala hoi wanyonge tu bali anaejali hali ya Taifa zima la Tanzania watu na mali zake.

Mikataba feki ya kurubuniwa,makampuni ya vigogo ambayo si ya kawaida kwa ukubwa na umiliki na hata kutoeleweka nani ni mmiliki.

Kama Magufuli anahitaji kutoka au kuiondoa Tz hapa ilipo mbali ya kusaka inapovuja kodi basi hawa Maraisi waliopita wote bila ya kujali ukaribu nae ni lazima awaundie kikosi kazi kiwachunguze kutoka nywele za utosi hadi kutumia darubini kuangaza nywele na vimelea vilivyo kwenye nyayo.
 
Kama Magufuli anahitaji kutoka au kuiondoa Tz hapa ilipo mbali ya kusaka inapovuja kodi basi hawa Maraisi waliopita wote bila ya kujali ukaribu nae ni lazima awaundie kikosi kazi kiwachunguze kutoka nywele za utosi hadi kutumia darubini kuangaza nywele na vimelea vilivyo kwenye nyayo.
Hawezi kufanya hivyo. Alishawaahidi siku anaapishwa pale uwanja wa taifa kuwa atawaheshimu na hatawaangusha watangulizi wake. Akawa anamtaja mmoja mmoja na kumpa ahadi hiyo.
 
Back
Top Bottom