Kama ni mabadiliko yata letwa na vijana!

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
Najua sasa hivi wengi wana jiuliza ni chama gani kita leta mabadiliko. Baadhi wata sema CCM, Chadema au chama chochote wao wanacho kiamini. Mimi binafsi naamini mabadiliko hayata kuja kutoka kizazi hichi cha uongozi tulio nao regardless ya vyama wanavyo toka.

Chadema na Mh. Slaa nawaona kama waasisi wa mageuzi. Kama vile kizazi kabla ya Nyerere ndicho kilicho anza vugu vugu za uhuru lakini hati mae ni kundi la vijana la wakina Nyerere ndiyo walio kuja kushika hatamu ya nchi.

Sasa basi kwa kufuatilia mtiririko huu wa mawazo mimi naona chama kita kacho dominate siasa za Tanzania ni kile ambacho kitaandaa vizuri vijana wake kushika hatamu ya uongozi. Hawa ndiyo wataibadilisha Tanzania for better or for worse.

CCM wao miaka yote imekua falsafa yao ya kuandaa vijana kuja kushika tatamu ya uongozi. Kama vile wakina JK walivyo andaliwa kuja kushika nchi (acha na ufanisi wao) basi na wao washaanza kuandaa vijana watakao fuata (japo sasa ni kurithisha watoto wao zaidi ya kuandaa vijana).

Sasa basi chama chochote kinacho taka kijulikane kama chama kilicho leta mabadiliko Tanzania haina budi kuandaa vijana sasa. Wazee wasiwe wabinafsi wa kudhani ni lazima matundi ya mabadiliko wale wao. Waandae vijana wao sasa.
 
Back
Top Bottom