Kama ni kwenda kusifia na kupongeza kila mtu anaweza kuwa Ubunge

Abby Newton

JF-Expert Member
Nov 12, 2017
1,227
2,197
Utitiri wa watu wanaochukua fomu za kuteuliwa ubunge imevunja rekodi mwaka huu. Baadhi wanajiuliza hii imetokana na nini? Jibu ni rahisi tu ni kwa sababu ubunge umekua kazi rahisi sana kuliko hata kulala kitandani. Bunge limekua ni sehemu ya kusifu, kupongeza na kunadi ilani. Je, ni nani asiyeweza kufanya hivo, kupiga makofi meza pwaa pwaa pwaa!! na kupiga vigelegele?

Kama umejaribu kuwasikiliza wanapohojiwa wakienda kuchukua fomu, kila mtu utaskia,"Rais John Joseph Pombe Magufuli kajenga reli, barabara, Stiglers, nk. Sasa mtu unajiuliza hayo kafanya Magufuli au wao, kwanini wasijisemee yao?

Kwanini wasieleze waliyoyafanya au watakayofanya? Kama kila kitu anafanya Magufuli kuna haja gani ya kuwa na wabunge?

Kumbe wengi wanatamani ubunge ili wakamsifie Magufuli. Yaani wakawe "Praise team" badala ya kwenda kuishauri na kuiwajibisha serikali. Tanzania bado hatujaendelea kufikia hatua ya kukosa cha kuikosoa serikali. Tunaenda kutengeneza Tanzania ya ajabu kupata kutokea.

Kuna watu wanaenda kuteuliwa ubunge kwa uhodari wao wa kusifia na si kwa uwajibikaji wao. Nawaona wabunge makini wanaukosa ubunge kwa sababu tu ya misimamo yao makini ya kuikosoa serikali. Maana awamu hii mtu akiikosoa serikali anaitwa eti kibaraka wa mabeberu.

Najiuliza hivi awamu ijayo tutakuwa na bunge au vitakuwa vikao vya chama? Ngoja niendelee kuitazama hii movie.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Mimi hua najiuliza tz tuna kasoro gani ?! Au ni kwa vile tumelelewa kijamaa zaidi. Vikao vya bunge vimekuwa kama mahudhurio ya drs la tatu. Ukiishauri serikali vinginevyo ataombwa miongozo, kanuni na utaratibu . Lakini ukianza kwa kuisifia serikali basi hapo ndiyo pake !. Yaani kazi ya mbunge imekuwa kinyume chake.

Tungelikuwa na spika kama yule mama wa Uganda mbona bunge lingekuwa safi. Sasa tunao ma spika wanaelekezwa wakawafukuze wabunge wanaoikosoa serikali, ili wakitoka nje washughulikiwe na dola ?! AJABU
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom