Kama ni kweli Simba SC inamsajili Edward Manyama, Mwenzake Mohammed Hussein aonywe 'asimroge' tafadhali

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,073
107,565
Nimezipokea hizi 'Tetesi' kwa Furaha kubwa mno na kama itakuwa ni kweli kwani Edward Charles Manyama ni Beki Bora wa Pembeni anayecheza 'Kisasa' zaidi tena kuliko aliyeko Mohammed Hussein Tshabalala.

Uzuri wake Edward Charles Manyama ni kwamba haishii tu kukupa Faida ya Kukaba vyema bali pia ana uwezo wa Kupanda (Kushambulia) na ni mfungaji mzuri hata Rekodi za VPL zinambeba.

Kwa nia njema tu nikiwa naheshimu Uwezo mkubwa alionao Beki Mohammed Hussein Tshabalala wa Simba SC ila niuombe tu Uongozi wa Simba SC kama kweli ' Watansajili 'Edward Charles Manyama (kutokea Ruvu Shooting FC) basi wawakalishe chini wote Wawili kuwa ' wasirogane ' na 'Kuumizana' ila mkazo mkubwa uwe kwa Tshabalala ambaye anajulikana kwa ' Miba ' Simba SC na ' Kuogopwa ' mno japo ana 'Kipaji 'kikubwa.

Ikiwa ni kweli nitafurahi kwani anatufaa.
 
Mohamed huseni miba yake ni kiwango chake tu gadiel anapambana sana kwa shabalala ila kwa Edward charz manayama hapa shabalala ajipange yule jamaa header corner timu yake inapo shambulia yuko poa sana
Kumbukumb zangu final fa simba vs namungo alifunga goal la kichwa mpira wa kona juzi na ruvu alikosa shabaha tena ya kufunga mpira wa kona mipira ya juu yupo vizuri sana.
 
Gadiel hakupigwa misumari wala nini ni yeye tu alishindwa kujiongeza. Anakaba vizuri mno ila alikuwa muoga wa kwenda kushambulia akiuona tu mstari wa katikati ya uwanja mbio anarudisha mpira kwa mabeki wa kati hata kama wachezaji wa timu pinzani wapo golini kwao. Kitu kingine kikubwa kilichomuangusha ni upigaji wake wa krosi. Sijui alikuwa akikaa benchi alikuwa anajifunza nini kwa wenzake waliopo uwanjani. Na mbaya zaidi kwake alikata tamaa mapema sana kiasi alikuwa akipewa nafasi badala "awaprove wrong"waliokuwa wanamzodoa na kumsahihisha yeye alikuwa anazubaa baaridi kabisa uwanjani uchangamfu sifuri. Siku hizi hakuna tena ule uchezaji wa kizamani wa mabeki wa pembeni kukaa umsubiri winga timu pinzani aje uokoe basi. Beki wa pembeni siku hizi ana kazi mbili kama sio tatu kukaba, kushambulia na hata ikiwezekana kuchezesha timu.
 
Huyu huku kwa wanaojua nini maana ya usajili
IMG-20210610-WA0196.jpg
 
Nimezipokea hizi 'Tetesi' kwa Furaha kubwa mno na kama itakuwa ni kweli kwani Edward Charles Manyama ni Beki Bora wa Pembeni anayecheza 'Kisasa' zaidi tena kuliko aliyeko Mohammed Hussein Tshabalala.

Uzuri wake Edward Charles Manyama ni kwamba haishii tu kukupa Faida ya Kukaba vyema bali pia ana uwezo wa Kupanda (Kushambulia) na ni mfungaji mzuri hata Rekodi za VPL zinambeba.

Kwa nia njema tu nikiwa naheshimu Uwezo mkubwa alionao Beki Mohammed Hussein Tshabalala wa Simba SC ila niuombe tu Uongozi wa Simba SC kama kweli ' Watansajili 'Edward Charles Manyama (kutokea Ruvu Shooting FC) basi wawakalishe chini wote Wawili kuwa ' wasirogane ' na 'Kuumizana' ila mkazo mkubwa uwe kwa Tshabalala ambaye anajulikana kwa ' Miba ' Simba SC na ' Kuogopwa ' mno japo ana 'Kipaji 'kikubwa.

Ikiwa ni kweli nitafurahi kwani anatufaa.
Manyama hajasajili simba
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom