Kama ni kweli Rwanda inawasaidia waasi wa M23, kwanini isitengwe Afrika Mashariki?

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Feb 18, 2016
1,261
1,222
Rais Paul Kagame anasemwa kuwa nchi yake inawasaidia waasi wa M23 ambao wanashikiria eneo lenye utajiri mkubwa wa madini ndani ya ardhi ya CONGO DRC.

Tuhuma hizi aliwahi kuzirusha Rais Joseph Kabila wa CONGO DRC na hata Umoja wa Mataifa(UN). waasi hawa wamesababisha CONGO DRC isiwe na amani hasa eneo la mashariki. madini ya Wakongomani yamekuwa yakiporwa na na rasilimali zingine haziwafikii wananchi wa taifa hili. vita vimeua wengi na kusababisha hasara kubwa kwa Wakongomani.

Najiuliza, kwanini kama njia ya kuishinikiza Rwanda isiwasaidie na kuwafadhili waasi, isitengwe na jumuia ya Afrika Mashariki? naona kama kuendelea kushirikiana nayo ni kushiriki kuwaonea na kuwatesa Wakongomani.
 
Back
Top Bottom