HaMachiach
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 3,399
- 6,077
ASKOFU GWAJIMA: NAGOMBEA UBUNGE
"Kama mlivyosikia Mh. Rais na Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally alivyosema kuwa wale watu wanataka kumsaidia Rais kuwatimizia wananchi azma yao basi waanze kupitapita na kuangalia nini kinawezekana kwahiyo nikaaamua nipite pale nimwombe na Mungu nione kama ataniruhusu basi tunaendelea"
"Naishi Kawe, kama CCM kikinipa ridhaa naona Kawe pananoga, sijawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA, nimekuwa mwana CCM tangu mwaka 1994" Askofu Josephat Gwajima, Askofu Mkuu na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.
NOTE: Kama ni kweli Gwajima amekuwa mwanachama wa CCM tangu 1994 sasa naanza kuamini kuwa Lowassa hakuenda CHADEMA kwa bahati mbaya na yote yaliyotokea baada ya yeye kuja CHADEMA ikiwemo yeye na Wabunge na madiwani waliotoka naye CCM kuamua kurejea nyumbani it was a planned mission. No wonder alisema amerudi CCM, CCM ni nyumbani na hataki maswali kwa sababu hakuna mtu anayeweza kuulizwa kwa nini ameamua kurudi nyumbani. Mwenda kwao si mtumwa.
Sijui ni AKILI gani ilitumika hadi CHADEMA ikamuamini huyu "MSHENGA" wa Lowassa.
Beyond reasonable doubt sasa nakubaliana na hoja zote na maswali yote ya Wilbroad Slaa. The man was right kuuliza tunampokea Lowassa kama ASSET au LIABILITY? Swali hili waliompokea walishindwa kulijibu hadi lilipojijibu lenyewe na linaendelea hadi leo.
Kadhia zote, madhila zote na mtifuano wote unaoendelea kufukuta ndani ya CHADEMA hadi leo ni matokeo ya ujio wa Lowassa akiletwa na mshenga huyu Gwajima.
Katika makosa ambayo CHADEMA wanafaa kujilaumu na kujutia sana ni kumuamini Kachero mbobezi Gwajima kuingia mpaka vikao nyeti vinavyojadili mikakati ya CHADEMA. Hapa chama kilijisalimisha kwa adui chenyewe.
Unaweza kumbeza Gwajima kama Askofu wa Ufufuo na Uzima ila ni hatari sana kumbeza Gwajima kama Kachero mbobezi. Ni hatari zaidi kumbeza Gwajima ambaye CHADEMA kwa ridhaa yao wenyewe walimuamini awaletee mgombea "mshenga" na kisha wakamwagia siri zote za chama wakiamini kuwa Gwajima ni mpinzani mwenzao.
Mtego sawia na huu huenda ukainasa ACT-Wazalendo au CHADEMA endapo Kachero mbobezi Bernard Membe ataamua kujiunga na ACT-Wazalendo kisha ACT-Wazalendo wakaunda Muungano wa mashirikiano na CHADEMA.
Naona hoja za vide za ngono za Gwajima zinaanza kuibuliwa na CHADEMA. Mimi nasema hoja hiyo haina nguvu wala mashiko maana wakati video zile zimetoka CCM walikuwa mstari wa mbele kuzilaani na kuzikashifu vikali lakini vijana wa CHADEMA waliimbishwa wimbo kuwa wasema kuwa video zile ni feki tu, zimeeditiwa n.k. Leo ukisimama kusema Askofu mwenyewe huyu alicheza video za ngono watu wanakuona mwendawazimu tu.
Nimalizie kwa kusema iwapo CCM wataamua kumtumia kijasusi Gwajima kwenye uchaguzi Mkuu huu, CHADEMA itajuta upya kwa nini ilimuamini Gwajima. Nasema itajuta upya kwa sababu hadi sasa ipo kwenye majuto na maumivu makali.
Hakuna wakati wowote ambao mikakati na mipango ya kijasusi ya CHADEMA imefeli au kuvuja kama kipindi hiki cha 2015 hadi sasa baada ya Gwajima kumchumbia Lowassa kwa CHADEMA. Ule ushenga umezua jambo, umezua tafrani. Ndoa imevunjika ila bado mizimu ya Lowassa na Gwajima imekataa kutoka CHADEMA inaendelea kuiguguna na kuiwewesesha usiku na mchana.
Nini maoni yako?
Remmy Cameroon
Sauti ya wasio na sauti