Kama ni kweli CHADEMA hawajatumia hata shilingi moja ya ruzuku itokanayo na wabunge 19 basi wamekomaa kisiasa

Kifaurongo

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
4,086
2,000
Kwanza kabisa nitoe pongezi za awali kama ni kweli CHADEMA haijagusa ruzuku itokanayo na wabunge 19 wa viti maalumu kwa kuamini wale siyo wabunge halali.

Hapo CHADEMA inaweza kujitofautisha na ACT wazalendo kwa ukomavu na kujiamini.

Maendeleo hayana vyama!
Msimlazimishe mgawa Ruzuku, Msajili wa vyama, atoke kuongea
 
Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
13,838
2,000
Wabunge wa viti maalumu hawana ruzuku mkuu. Ruzuku inatokewakutokana na wabunge wa kuchaguliwa. Chukua elimu hiyo!
Kwanza kabisa nitoe pongezi za awali kama ni kweli CHADEMA haijagusa ruzuku itokanayo na wabunge 19 wa viti maalumu kwa kuamini wale siyo wabunge halali.

Hapo CHADEMA inaweza kujitofautisha na ACT wazalendo kwa ukomavu na kujiamini.

Maendeleo hayana vyama!
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
53,822
2,000
Tuonyeshe kifungu hicho cha katiba, vinginevyo ni utoporo tu.
2: kwa hiyo mnatambua kuwa ushindi wa magufuli ni halali na nyie mlifikisha zaidi ya hiyo % 5? Na kama hamkubali ushindi huo kwa nini mkubali hiyo % ili mpate ruzuku?
Lete majibu hayo mawili zidi ya hapo ni njaa inawasumbua mkikubali kula ruzuku kwa namna yoyote.
Ruzuku ni mali ya dikteta au ni kodi za watanzania? kwa hiyo ukifungwa kwa uonevu utagoma kula kisa umefungwa kwa uonevu?
 
This is...

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
3,144
2,000
Sasa kama hata mambo madogo tu ya ruzuku huyajui unafanya nini hapo Ufipa?

Nyie ndio mh Naibu waziri Katambi aliwaita " Bavicha makarai"
Ila mkuu tuwe wakweli,ktk kujenga hoja ww ni low sana.umekaa kiumbea mbea,udaku so udaku.Sijui hata mkeo km unae anamudu vipi kuishi na mwanamme mbea. Mtu usiyejua hata mambo ya msingi,ya maana muda wote ni mtu wa hoja nyepesi nyepesi. Upuuzi upuuzi tu.

Inaonekana Ni mtu mwenye hali ngumu sana kimaisha.hata maji ya kunywa yaliyo safi tu ni shida achilia mbali mlo wa siku.Ninakufahamu sana.
 
Samiaagain2025

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
1,832
2,000
Kwanza kabisa nitoe pongezi za awali kama ni kweli CHADEMA haijagusa ruzuku itokanayo na wabunge 19 wa viti maalumu kwa kuamini wale siyo wabunge halali.

Hapo CHADEMA inaweza kujitofautisha na ACT wazalendo kwa ukomavu na kujiamini.

Maendeleo hayana vyama!
Hela ya ruzuku hutokana na idadi yakura au idadi ya wabunge?Naomba ujibu kwa reference,siyo kukariri.
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
15,391
2,000
Kwanza kabisa nitoe pongezi za awali kama ni kweli CHADEMA haijagusa ruzuku itokanayo na wabunge 19 wa viti maalumu kwa kuamini wale siyo wabunge halali.

Hapo CHADEMA inaweza kujitofautisha na ACT wazalendo kwa ukomavu na kujiamini.

Maendeleo hayana vyama!
Huwa najitahidi kukuamini hata unapocheza nje ya mstari. Aliyekwambia Ruzuku inatokana na Wabunge wa viti maalum ni nani?
 
Tz mbongo

JF-Expert Member
Mar 12, 2015
8,244
2,000
Ruzuku ni mali ya dikteta au ni kodi za watanzania? kwa hiyo ukifungwa kwa uonevu utagoma kula kisa umefungwa kwa uonevu?
Hata uchaguzi pamoja na bunge ni vitu ambavyo vipo kikatiba na si mali wala matakwa ya Dikteta.
 
artch2311

JF-Expert Member
Jan 5, 2016
1,158
2,000
Kama ndivyo,inamaana CDM ruzuku ilipungua nusu nzima!Kitu ambacho si kweli!
Asili ya kura za urais unazopata ndizo huamua kiwango cha ruzuku!Ndio maana NEC ikaja na sheria kuwa kama vyama vitasimamisha mgombea mmoja wa urais basi waandae mkataba wa namna gani watagawana ruzuku!
Nimegoogle na kukuta taarifa hiyo iliyoandikwa na gazeti la mwananchi kwamba kufuata ile hamahama CCM iliongeza ruzuku kea takriban one billion. Kweli kwamba Wabunge nao huchangia ruzuku inayopatikana chamani
 
Attachments

  • Screenshot_2020-12-29-17-10-37-79.jpg
    File size
    176.9 KB
    Views
    0

SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
33,480
2,000
Nimegoogle na kukuta taarifa hiyo iliyoandikwa na gazeti la mwananchi kwamba kufuata ile hamahama CCM iliongeza ruzuku kea takriban one billion. Kweli kwamba Wabunge nao huchangia ruzuku inayopatikana chamani
Hiyo ruzuku inayoongelewa hapa ni wabunge wa kutoka majimboni wale waliokuwa wananunuliwa kama njugu na siyo hao wa viti maalum.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom