Kama ni Kweli Basi Kitendo Hiki cha Jeshi la Polisi na Magereza ni cha Kihuni

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Kama watanzania tunategemea wanajeshi wetu, kutia ndani Polisi na Magereza, kujiendesha kwa namna ambayo inaonyesha wao ni vinara wa uaminifu (integrity). Hutarajii hata siku moja kuona kwamba Polisi na Magereza wanatumia udanganyifu katika kazi zao. Pale inapotokea wanafanya kazi kwa udanganyifu basi tutatilia shaka kila linalosemwa na Jeshi la Polisi au Magereza, na hata kukubali dhana ya kwamba kesi nyingi zinazofunguliwa Polisi ni za kubambika.

Katika suala la kesi inayomkabili Mbunge Lema dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Gumbo, askari wa Jeshi la Polisi wakishirikiana na wale wa Jeshi la Magereza, waliwafukuza waandishi wa habari waliokuwa katika kazi zao rasmi hapo Mahakamani wakidai kwamba walifanya hivyo kwa maagizo ya Mahakama. Waandish wa habari walipoenda kumuuliza Hakimu Rwezile anayesimamia kesi hii, alipinga tamko hilo la Polisi na Magereza akisema kwamba Mahakama haikutoa agizo hilo na alitambua kwamba waandishi wa habari walikuwa na barua za utambulisho kufanya kazi yao Mahakamani.

Kama ni kweli Polisi ma Magereza walitumia udanganyifu katika kuwafukuza waandishi wa habari, basi hiki ni kitendo cha kihuni sana kwa upande wa Polisi na Magereza. Na ina maana Tanzania tuna tatizo kubwa na la kutisha kwamba tuna Polisi na Magereza ambao kwao kusema uongo ni jambo dogo sana. Sasa ikiwa wao ndio walioaminiwa hata katika masuala ya kufungua mashitaka dhidi ya uhalifu na kutoa ushahidi mahakamani, tutaaminije kwamba hawafanyi hivyo kwa njia ya udanganyifu, ikiwa wanaonyesha wamezoe kusema uongo kirahisi tu?

Si jambo dogo, ni jambo linalotakiwa kutolewa maelezo na Wakuu wa Polisi na Magereza na hata Waziri wa Mambo ya Ndani.
 
Ni kweli ila nilitaraji na waandishi habari hii wangeipa kipaumbele lakini haikuwa hivyo.

Waandishi wangekuwa wanajitambua habari ya wao kufukuzwa ndio ilipaswa kuwa headlines (leading story) katika vyombo vyao vya habari ila cha kusikitisha waandishi wenyewe hawajitambui!
 
Godbless Lema ana kesi nyingi za kujibu. Katika nchi za wenzetu, leo hii tungekuwa tunasema mengine. Ila hapa Tanzania demokrasia inatawala
 
Godbless Lema ana kesi nyingi za kujibu. Katika nchi za wenzetu, leo hii tungekuwa tunasema mengine. Ila hapa Tanzania demokrasia inatawala

Huyu jamaa anaweza kuwa na kesi za kujibu, ila kwa hii kesi ya ujumbe wa sms, mawakili wa serikali iwasipokuwa makini wataangukia pua na kuumbuka sana. Kesi za namna hii ni rahisi sana kuzishinda, unahitaji mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa IT kuonyesha kwamba mashitaka hayana mshiko.
 
Back
Top Bottom